Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 11/22 kur. 21-23
  • Roki ya Badala—Je, Inanifaa?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Roki ya Badala—Je, Inanifaa?
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Unavutia?
  • Neno la Tahadhari
  • Uwe Mteuzi
  • Jilinde na Muziki Usiofaa!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Ninaweza Kuwa na Usawaziko Jinsi Gani Kuhusu Muziki?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Muziki Waweza Kweli Kuniumiza?
    Amkeni!—1993
  • Ninaweza Kuwekaje Muziki Mahali Pao Panapofaa?
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 11/22 kur. 21-23

Vijana Huuliza . . .

Roki ya Badala—Je, Inanifaa?

“Naweza kupenda nyimbo hizo zinazozungumzia matatizo na mambo mbalimbali ambayo sisi vijana hupata.”—George mwenye umri wa miaka 15.a

“Hiyo iko katikati ya muziki upendwao sana na muziki wa mdundo mzito.”—Dan mwenye umri wa miaka 19.

“Ni mpya. Ni tofauti. Si muziki wa kawaida, wenye kutokezwa kwa wingi.”—Maria mwenye umri wa miaka 17.

ROKI ya badala. Vijana wengi hufurahia kuisikiliza. Watu fulani wazima husumbuliwa nayo. Na wazazi wengi wanaielewa kidogo au hawaielewi kabisa.

Kwa kweli, si rahisi kufafanua roki ya badala. Mwanzoni, ilikuwa muziki wa vijana ambao walitaka kitu tofauti, kibadala cha muziki wa kawaida ambao huchezwa katika redio. Wengine husema kwamba ilianza wakati vituo vya redio vya chuo za mahali-mahali vilipotangaza vikundi fulani vya muziki ambavyo havikujulikana kabisa—vikundi vya muziki ambavyo havikupiga muziki kwa makusudi ya biashara. Kizazi hicho kipya cha wanamuziki kiliepuka makampuni mashuhuri ya kurekodi muziki na mbinu za kuuza muziki kwa wingi, kama vile kutumia muziki wa video. Pia kiliandika mambo ambayo ni nadra kutajwa na nyimbo 40 Bora.

Tofauti na muziki wa mdundo-mzito au rapu, roki ya badala haitambuliki au kuainishwa kirahisi. Hata wataalamu katika muziki hawakubaliani muziki wa roki ya badala ni nini hasa. Sababu ni kwamba, kama jina layo lidokezavyo, hiyo hutia ndani aina nyingi za sauti, hali ya moyoni, na hisia. Kijana mmoja mwanamume alisema: “Ni vigumu sana kuiainisha. Hiyo hutia ndani sehemu kubwa ya muziki wa leo.” Kijana mwingine alitoa maelezo haya: “Roki ya badala nyakati zote siyo mdundo mzito au usio mzito, wa kasi au wa polepole, wenye furaha au wa huzuni.” Kijana mmoja alikiri hivi: “Sina uhakika ikiwa ninaweza kusema napenda roki ya badala kwani sina hakika hiyo ni nini.”

Kwa vyovyote, kupendwa kwa roki ya badala kumekua kufikia kiwango ambacho wasanii wayo wengi wenye kupendwa wanafikiriwa kuwa sehemu ya muziki wa kawaida. Pia wazazi waonekana hawaelekei kuipinga kama wanavyopinga muziki wa mdundo mzito au roki za aina nyingine zenye kuharibu masikio. Kwa kweli, hata ni wazazi wachache wanaoonekana kujua kikundi au vichwa vya viwekeo ambavyo vinaitwa roki ya badala. Hata hivyo, kuna uhitaji wa wewe kuchukua hatua za tahadhari muziki huu unapohusika.

Kwa Nini Unavutia?

Kwa mfano, fikiria ni kwa nini vijana wengi wanavutiwa na muziki huu. Kwa wengi, ni suala tu la kufuata maoni ya marafiki. Pia hiyo huandaa mambo ya kuzungumzia au utendaji wa pamoja, kama vile kubadilishana kanda na diski songamano.

Lakini, kwa vijana wengi mtindo maalumu wa muziki na ujumbe wa roki ya badala ndio hufanya hiyo ivutie sana. Kimahususi, vijana wengi hujishirikisha na mambo na hisia za watunzi wa nyimbo. Makala kuu za gazeti Time kuhusu jambo hilo zilisema: “Ingawa nyimbo zipendwazo sana kwa kawaida huzungumzia mapenzi, maneno ya nyimbo za roki ya badala kwa kawaida huzungumzia hisia zisizo na wororo: kukata tumaini, tamaa kubwa ya ngono, kuchanganyikiwa. . . . Ikiwa uko katika miaka ya utineja au ya 20, upo uwezekano kwamba familia yako imetaliki. Muziki wa badala umekuwa muziki wa kihisia-moyo, ukiongea moja kwa moja juu ya masuala ambayo huachwa bila kutatuliwa na ukosefu wa haki.” Hivyo, mpiga rekodi mmoja wa chuo mwenye umri wa miaka 21 asema: “Hunifurahisha mimi na marafiki wangu kwa sababu kizazi chetu hakijali ulimwengu. Tumalizapo shule hamna matumaini mazuri mbele yetu.”

Baadhi ya vijana Wakristo pia wamekuwa wapenzi wa roki ya badala. Kwa kawaida, wengi wameepuka nyimbo zenye mdundo-mzito sana, zenye kuasi sana, zenye jeuri, au zenye ukosefu wa adili. Hata hivyo, baadhi ya vijana hawa Wakristo wamekataa nyimbo zionekanazo kuwa hazina madhara. Kijana Dan alieleza: “Baadhi ya waimbaji wanajulikana kuwa wagoni jinsia-moja na wasago au watumiaji wa dawa za kulevya, na maneno ya nyimbo zao huonyesha mtindo-maisha wao.” Kijana mwingine, aitwaye Jack, asema: “Baadhi ya vikundi vya muziki vina wazo la kwamba hamna anayewajali vijana, matatizo yao, au wakati ujao wa vijana wa leo, hivyo wanaeleza haya katika nyimbo zao. Wengi hawana kusudi au tumaini.”

Neno la Tahadhari

Biblia yatuambia kwamba “dunia yote pia hukaa katika yule mwovu,” Shetani Ibilisi. (1 Yohana 5:19) Basi, isikushangaze kwamba muziki ni moja ya njia atumiazo Shetani katika kudanganya vijana. Makala za nyuma za gazeti hili na gazeti jenzi lake, Mnara wa Mlinzi, kwa kurudia-rudia zimeonyesha ukweli huu.b Maonyo ambayo yametolewa kuhusu muziki wa mdundo mzito na rapu pia yanafaa roki ya badala. Kama vile Biblia isemavyo, “mwenye busara huangalia sana aendavyo.”—Mithali 14:15.

Kwa mfano, si jambo la akili kufuata halaiki kwa upendezi wako wa muziki. Angalia kanuni hii ya Biblia: “Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii?” (Warumi 6:16) Kwa kijana Mkristo, suala si kipi kinachokubalika miongoni mwa marika bali “ni nini impendezayo Bwana.” (Waefeso 5:10) Zaidi ya hayo, ni vijana wa aina gani wanaovutiwa kwa roki ya badala? Je, ni vijana waonekanao kuwa wenye furaha, usawaziko, na kupendezwa na mambo ya kiroho? Au wasikilizaji wayo wakuu ni miongoni mwa vijana ambao hawajaridhika, wasio na furaha, au hata wenye hasira?

Kweli, baadhi ya vijana wenye furaha, wenye kutazamia mambo mazuri bado wanaweza kuvutwa na roki ya badala. Lakini fikiria hili: Wakristo, vijana kwa wazee, wana wakati mzuri ajabu unaowangoja. (2 Petro 3:13) Mtume Paulo atukumbusha uhakika wa utimizo wa ahadi za Mungu, akisema: “Mungu hawezi kusema uongo.” (Waebrania 6:18) Kuna faida gani, basi, kujihatarisha kwa maoni hasi yasiyofaa juu ya wakati ujao ambayo baadhi ya nyimbo za roki ya badala hueleza? Je, yawezekana kwamba kumezwa na muziki ambao hueleza hofu, kukata tumaini, na ukosefu wa tumaini kunaweza kudhoofisha imani yako? Isitoshe, ujilishaji wa muziki wa aina hiyo utaathirije mtazamo wako wa kihisia moyo?

Uwe Mteuzi

Hii si kusema kwamba muziki wote uitwao “badala” lazima uwe na madhara au ni mbaya sana. Tuseme umegundua kwamba mtu fulani alikuwa anajaribu kukulisha sumu. Ingawa hutaacha kula, bila shaka ungechunguza kwa uangalifu chakula chako, sivyo? Ukijua kwamba Shetani anajitahidi kufisidi mtazamo na mwelekeo wako itakufanya pia kuwa mwangalifu kuhusu muziki uchaguao. Kama vile Biblia isemavyo, “kwa kuwa sikio huyajaribu maneno, kama vile kaakaa lionjavyo chakula.” (Ayubu 34:3) Badala ya kufuata halaiki bila kujua, ujaribu muziki uupendao.

Waweza kufanyaje hilo? Sanduku lenye kichwa “Mwongozo Katika Kuchagua Muziki” lina madokezo yanayofaa ambayo waweza kujaribu. Pia, jaribu kuuliza wazazi wako Wakristo wanaonaje muziki wako. (Mithali 4:1) Waweza kushangazwa na majibu yao! Ni wazi, wazazi wako wana umri mkubwa kukuzidi. Kwa kueleweka, huenda wasipende muziki upendao. Lakini kama hawaupendi muziki wako kufikia kiwango cha kuuona kuwa wenye kuchukiza sana, wenye kushusha tabia, au wenye kukirihisha, je, utadharau kile ambacho wanasema? Biblia yasema: “Mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu.”—Mithali 1:5.

Fikiria muziki wakuathirije. Je, unakufanya ujisikie kuwa mwenye hasira, mwasi, au mwenye kushuka moyo? Ikiwa ni hivyo, hizi ni ishara ambazo hupaswi kuzidharau! Kwa nini usitafute muziki unaokustarehesha au kukutuliza au unaokuchangamsha?

Mielekeo katika muziki hubadilika daima. Karibuni, aina nyingine ya muziki itakuwa ndiyo ya kisasa zaidi na yenye kupendwa sana. Usipeperushwe pamoja na mawimbi haya yenye kubadilika-badilika. Uwe mwenye utambuzi na mteuzi katika muziki. Hakikisha kwamba kila usikilizacho ni chenye kufaa na kujenga. (Wafilipi 4:8) Ndipo, muziki uwezavyo kuwa sehemu yenye thamani na yenye kufurahisha ya maisha yako!

[Maelezo ya Chini]

a Baadhi ya majina yamebadilishwa.

b Ona makala za “Vijana Huuliza . . . ” katika matoleo ya Amkeni! ya Februari 8, Februari 22, na Machi 22, 1993. Pia angalia “Jilinde na Muziki Usiofaa!,” katika toleo la Mnara wa Mlinzi la Aprili 15, 1993.

[Blabu katika ukurasa wa 22]

“Ingawa nyimbo zipendwazo sana kwa kawaida huzungumzia mapenzi, maneno ya nyimbo za roki ya badala kwa kawaida huzungumzia hisia zisizo na wororo: kukata tumaini, tamaa kubwa ya ngono, kuchanganyikiwa.”—Gazeti Time

[Sanduku katika ukurasa wa 23]

Mwongozo Katika Kuchagua Muziki

◆ Chunguza kifurushi cha kiwekeo. Hiki kitakueleza mengi kuhusu muziki na wanamuziki wenyewe. Jihadhari na vifuniko vya viwekeo ambavyo huonyesha jeuri, alama za Kiibilisi, mavazi na kujipamba kwa kupita kiasi au yenye kuonyesha uchi.

◆ Fikiria ujumbe wa maneno. Huu hutambulisha mawazo na mtindo-maisha wa wanamuziki. Ni mawazo gani wanayotaka uyapate?

◆ Sauti ya ujumla ya muziki huonyesha hali ya moyoni na hisia ambazo wanamuziki wangetaka uhisi—huzuni, shangwe, ukaidi, kuamshwa kingono, utulivu au kukata tumaini.

◆ Wafikirie wasikilizaji kwa ujumla ambao wanavutwa na kikundi cha muziki. Je, ungependa utambuliwe miongoni mwa kikundi hicho cha watu na mitazamo yao?

[Picha katika ukurasa wa 23]

Vijana wengi hupenda maneno ya nyimbo za leoy

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki