Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w82 4/15 uku. 3
  • Kurithi Kwetu Ugonjwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kurithi Kwetu Ugonjwa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Habari Zinazolingana
  • Ugonjwa—Kuna Tumaini Gani la Kupata Faraja?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Yabisi-kavu Ni Ugonjwa Unaolemaza
    Amkeni!—2001
  • Wakati Mshiriki wa Familia Ni Mgonjwa
    Siri ya Furaha ya Familia
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
w82 4/15 uku. 3

Kurithi Kwetu Ugonjwa

MUME na mke wachanga walikuwa wamesisimuka sana! Ilifurahisha kutazama shauku yao ya kutazamia walipokuwa wakingojea kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza. Kisha kitoto hicho kikazaliwa, kisichana. Walakini kilikuwa na kasoro kubwa sana. Hakingepata kuishi maisha ya kawaida kamwe. Mzazi mwingine tu ndiye angeweza kufahamu mshtuko na huzuni kubwa yao.’

Yeye ni mwanafunzi wa shule ya masomo ya juu, anayeheshimiwa na waalimu wake, na anapendwa na wenzake. Kila mtu alikuwa ametabiri kwamba yeye angekuwa na wakati ujao mzuri sana na wenye kufanikiwa sana. Wakati huu, katika mwaka wake wa mwisho katika shule, yeye amepatwa na maumivu katika miguu yake. Uchunguzi umeonyesha kwamba ameambukiwa na maradhi makali ya kushupaa kwa mishipa. “Sababu gani mimi?” ndivyo anavyouliza. “Sababu gani sasa?”

Je! unaumwa kichwa, kama mwanamke huyu? Au wewe ni mmoja kati ya watu wengi sana wanaosumbuliwa na tumbo, wanaopata maumivu ya misuli, kuumwa sana mgongo, mdundo mwingi wa moyo, machafuko ya akili, baridi yabisi au kitu kama hicho? Ni mara chache matatizo hayo yanapoua, walakini yanatuzuia tusifurahie maisha. Na yanafanya maisha yawe magumu sana siku fulani.

Je! kuna tumaini kwamba hali kama hizo huenda zikaondolewa siku moja? Je! utakuja wakati ambapo wanadamu hawatataabishwa na adui zao wa muda mrefu, ugonjwa na kifo? Au hayo ni sehemu ya kudumu ya hali ya kibinadamu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki