Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 5/15 uku. 27
  • Kujua Yaliyo Katika Habari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kujua Yaliyo Katika Habari
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • UKIMWI—Kupatwa na Matokeo ya Ubaya
  • Amani na Usalama—Je, Ni Karibuni?
  • Kulipa Kisasi kwa Kutumia Nyukilia—Je, Ndiyo Njia ya Mungu ya Kulipa Kisasi?
  • Amani Kutoka kwa Mungu Wakati Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Tisho la Nyukilia—Laondolewa Milele!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Hatimaye Wakati Ujao Ulio Salama!
    Amkeni!—1999
  • Umoja wa Mataifa—Njia Bora Zaidi?
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 5/15 uku. 27

Kujua Yaliyo Katika Habari

UKIMWI—Kupatwa na Matokeo ya Ubaya

Shirika la Vituo vya Serikali ya United States vya Kuzuia Magonjwa linakadiria kwamba wastani ya gharama za hospitali kwa siku katika kutibu wagonjwa wa UKIMWI ni dola 830—mara mbili ya zile za kutibu wagonjwa wengine. Na wataalamu wanakadiri kwamba jumla ya gharama za kutibu kila mgonjwa zingeweza kuwa na wastani ya dola zaidi ya 100,000. jambo hilo na ongezeko kubwa sana la hesabu ya wenye kupatwa na UKIMWI wanaotafuta matibabu linahangaisha maafisa wa hospitali na wa bima.

Shirika na Hospitali Amerika linasema mweneo wa haraka sana wa UKIMWI ni kama “kombora lililotegewa saa za kulipuka” kwa hospitali za taifa, kwa maana karibuni gharama za dola zitakuwa maeIfu ya mamilioni kila mwaka. Afisa mmoja wa bima ya uhai alionya hivi: “Mimi naiona ikielekea kuwa ndiyo hasara kubwa zaidi ya kifedha ambayo biashara ya bima ya afya na uhai imewahi kukabili katika nchi hii.” Ni nani atakayeubeba mzigo huo mkubwa sana wa kifedha?

Watu wengi wanaopatwa na UKIMWI ni wale wanaolalana na watu wa jinsia yao na waliozoelea matumizi ya dawa za kulevya, ambao mtindo wao wa maisha wa kufuatia anasa uliwaletea ugonjwa huo. Lakini sio watakaopata hasara ya kifedha. Bali, maafisa wa serikali na bima wanaonyesha kwamba waliofanya mkataba wa bima na wenye kulipa kodi watalazimika kuubeba mzigo huo kwa kuongezewa kiasi cha kulipa. Tena, “kutakuwa na hasara katika mahitaji ya elimu, usalama wa watu na ya mahitaji makubwa,” ikasema makala ya mhariri katika gazeti New York Post.

Hapo kwanza, watu wenye UKIMWI waliopatwa na ugonjwa huo kwa sababu ya mtindo wao wa maisha wanaweza kuwa walifanya dhihaka juu ya maadili ya Biblia ili kutetea namna yao ya kujitosheleza nyege. Ni maumivu na gharama kubwa kama nini ambazo wangaliweza kuepuka zisiwapate wao wenyewe na watu wengine! Lakini, huenda isiwe kuchelewa mno kwa wo wote wa watu hao kugeukia sasa viwango vya Biblia vivyoandikwa kwa uongozi wa roho kutokana na ‘akufundishaye ili upate faida, akuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.’—Isaya 48:17.

Amani na Usalama—Je, Ni Karibuni?

Maandishi yanayojulikana sana yaliyoandikwa katika ukuta wa Njia Kuu ya Umoja wa Mataifa yanasema: “Watafua panga zao ziwe majembe. Na mikuki yao iwe miundu: Taifa halitainua upanga juu ya taifa. Wala hawatajifunza vita tena.” Kwa kujawa na tumaini la kuzaa matunda yenye kutimiza maneno hayo ya kiunabii, Umoja wa Mataifu umeutangaza mwaka 1986 kuwa ndio “Mwaka wa Amani ya Kimataifa.” Je, kuna sababu ya kuamini kwamba UM utafanikiwa katika mradi ambao imejitokeza waziwazi kuufikia ikiwa ndiyo mtunzaji aliyejitangaza mwenyewe wa “amani na usalama wa kimataifa? ”

Hata uwe ni mchango gani utakaofanywa na UM wa kuelekea kutokeza tangazo linalokaribia la “amani na salama,” hakika amani yo yote yenye kuletwa na wanadamu inategemea msingi unaoweza kulipuka. (1 Wathesalonike 5:3) Matumizi ya kifedha katika mambo ya kijeshi sasa yanakadiriwa kuwa yanafikia dola trilioni moja kila mwaka ulimwenguni pote. Tangu Vita ya Ulimwengu ya Pili, gharama ya kujenga mabohari ya silaha za nyukilia, bila kutia ndani silaha zile za kikawaida, imekadiriwa kuwa dola trilioni tatu mpaka nne—kiasi ambacho kisingetazamiwa kamwe kitumiwe wakato ambao UM unataka watu wajielekeze kwenye amani na usalama wa ulimwengu! Kwa kweli, Vernon Walters, balozi wa U.S. kwa Umoja wa Mataifa, anasema, “Umoja wa Mataifa umepeperuka ukaliacha daraka lao la kuwa chama cha kuleta suluhisho ili kusiwe na mapigano,” hiyo ikabomoa matumaini ya wale walioamini kwamba “U.M. ungefanya mengi kuliko yale uliyoyafanya kwa kuleta suluhisho kusiwe na mapigano.”

Hata hivyo, maneno yaliyoandikwa ukutani ya Isaya 2:4 ambayo yametangulia kutajwa yatatimizwa — lakini si katika mwaka 1986, wala wakati wo wote, kupitia jitihada za tengenezo lililofanywa na wanadamu. Bali, amani na usalama wa kweli utaletwa karibuni na serikali ya kimbingu, ambayo kiongozi wayo asiyeonekana ni “Mwana-Mfalme wa Amani” kweli kweli.—Isaya 9:6, 7, NW

Kulipa Kisasi kwa Kutumia Nyukilia—Je, Ndiyo Njia ya Mungu ya Kulipa Kisasi?

Je, matumizi ya silaha za nyukilia yangeweza kuonwa kuwa sawa tu kwa kujibu shambulio la nyukilia? Ndiyo, linasema Free Church of Scotland katika toleo la hivi majuzi la gazeti lao la kanisa, The Monthly Record. Makala hiyo ilisema kwamba ulipaji kisasi huo ungeweza mwishowe kuwa “ufikilizaji halali wa hasira kuu ya Mungu” kwa sababu ya “amri ya kimungu ya kufikiliza hasira kuu juu ya uovu.” Gazeti Record linadai pia kwamba ushahidi wao ni kutia ndani tangazo la hukumu ya Mungu juu ya “taifa lili . . . linalokuwa la kwanza kushambulia katika vita ya nyukilia.”

Ni hakika kwamba kutakuwa na “siku ya kisasi cha Mungu wetu” (Isaya 61:1, 2) Lakini kisasi cha Mungu juu ya mataifa ya kijeshi kitaonyeshwa katika wakati na njia ambayo yeye anachagua. Badala ya mataifa ya kidunia kuonyesha hasira kuu, “hasira” ya Mungu mwenyewe ndiyo “itakayowaharibu hao waiharibuo nchi.” Jinsi gani? Kwa kumpeleka “Mfalme wa wafalme,” Bwana Yesu Kristo ‘akahukumu na kufanya vita kwa haki.’ Ufalme wake wa kimbingu “utavunja falme zote hizi vipande vipande na kuziharibu.”—Ufunuo 11:18; 19:11-21; Danieli 2:44.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki