Habari Za Kitheokrasi
◼ Hivi majuzi Jumba la Ufalme la Oyugis, Kenya, liliwekwa wakfu.
◼ Ofisi za tawi kadhaa za visiwani ulimwenguni zimeripoti vilele vipya vyenye kutokeza vya wahubiri katika Januari. Baadhi yazo zilikuwa Filipino, Haiti, Jamhuri ya Dominika, Martinique, Mauritius, Taiwan, na Trinidad.
◼ Ongezeko katika Shelisheli lilikuwa asilimia 18 kuliko wastani wa mwaka jana, na katika St. Maarten ongezeko lilikuwa asilimia 16.
◼ Jumba la Ufalme la kwanza kujengwa haraka Taiwan lilimalizwa Februari.