MAOMBOLEZO YALIYOMO 1 Jiji la Yerusalemu lafananishwa na mjane Limebaki ukiwa na kuachwa (1) Dhambi nzito sana za Sayuni (8, 9) Sayuni lakataliwa na Mungu (12-15) Hakuna wa kulifariji Sayuni (17) 2 Hasira ya Yehova dhidi ya Yerusalemu Hakulihurumia (2) Yehova ni kama adui yake (5) Machozi yamwagwa kwa ajili ya Sayuni (11-13) Wapita njia walidharau jiji lililokuwa maridadi awali (15) Maadui washangilia kuanguka kwa Sayuni (17) 3 Yeremia aeleza hisia na matumaini yake “Nitaonyesha mtazamo wa kungojea” (21) Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi (22, 23) Mungu ni mwema kwa wale wanaomtumaini (25) Ni jambo jema kwa vijana kubeba nira (27) Mungu aziba kwa wingu njia ya kumkaribia (43, 44) 4 Matokeo mabaya ya kuzingirwa kwa Yerusalemu Ukosefu wa chakula (4, 5, 9) Wanawake wawachemsha watoto wao wenyewe (10) Yehova amemwaga hasira yake (11) 5 Watu wasali warudishwe ‘Kumbuka yale ambayo yametupata’ (1) ‘Ole wetu; tumetenda dhambi’ (16) ‘Turudishe, Ee Yehova’ (21) “Zifanye siku zetu ziwe mpya” (21)