Hasara Kubwa ya Utumiaji wa Vileo
Utumiaji wa vileo na magumu yanayohusiana nao unaletea United States hasara ya pesa nyingi mno. Kulingana na habari za karibuni, hasara yenyewe ni zaidi ya shilingi mamilioni milioni 175 kwa mwaka. Kiasi hiki kikubwa sana ni mara tano za kiasi cha pesa kinachohitajiwa kuwapa chakula wote wanaotaabishwa na njaa nchini. Pia, kingetosha kujenga karibu nyumba 1,750,000 za bei ya chini. Utumiaji wa vileo ni wenye bei kweli kweli.