Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w76 7/1 kur. 291-292
  • Uhuru wa Ibada Msumbiji Wamalizwa Kikatili

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uhuru wa Ibada Msumbiji Wamalizwa Kikatili
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Habari Zinazolingana
  • Wakosa Kuvumiliwa Kwa Mara Nyingine
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Mungu Amekuwa Msaidiaji Wetu
    Amkeni!—1999
  • Watu Wakaidi Wapuza Katiba ya Malawi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Kumtumikia Yehova Katika Majira Yenye Kupendeleka na Katika Yenye Matata
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
w76 7/1 kur. 291-292

Uhuru wa Ibada Msumbiji Wamalizwa Kikatili

GIZA linaingia katika eneo kubwa la Afrika. Lakini kwa makumi ya miaka kumekuwa kukipazwa sauti za kutaka nuru ya “Uhuru!”

Kwa karne nyingi mataifa ya nchi nyingi za Kiafrika yalikuwa chini ya nira ya mataifa ya bara nyingine. Mataifa hayo ya kwanza yametafuta yakapata uhuru kwa wanasiasa na wanauchumi wenye kuwaweka chini ya nira hiyo. Lakini sasa, ndani ya nyingine za nchi hizo zilizopata uhuru, jaribio linafanywa kufutilia mbali uhuru wa msingi wa watu: Uhuru wa ibada.

Wakati mmoja wakoloni walilaumiwa juu ya kutumia mamlaka na uwezo wa kijeshi kwa kutenda wenye nchi kikatili ndiyo wakubaliane na madai yao, bila ya kuwapa nafasi ya kutoa maoni yao wala ya kutumia dhamiri zao. Sasa mamlaka ile ile na uwezo wa kijeshi unatumiwa kikatili kushambulia haki ya kuabudu kulingana na dhamiri ya mtu.

Walakini, wakati huu Waafrika ndio wanaoshambulia Waafrika wenzao, wananchi wenzao! Gazeti hili Mnara wa Mlinzi limetoa hivi karibuni habari za shambulio hilo juu ya uhuru wa ibada katika Malawi.a Sasa shambulio kama hilo linafanywa katika nchi jirani ya Msumbiji.

Mtu akishinda mpinzani wa kutisha katika mpambano mrefu, watazamaji wanaweza kuvutwa na ushujaa na uvumilivu wake, wawe wanamhurumia katika mpambano huo au sivyo. Lakini je! wangeendelea kumheshimu zaidi au wangekosa kumheshimu baadaye wakimwona akigeukia mtoto mdogo, kumpiga na kumfunga mtoto huyo, akidai kwamba mtoto ni “hatari kwa usalama” wake? Hilo ndilo limetokea katika nchi ya Afrika Mashariki ya Msumbiji. Fikiria hili:

Kwa karne tatu Msumbiji ilitawaliwa na Wareno. Lakini miaka kumi iliyopita majeshi maasi yalipiga vita vikali kufanya nchi hiyo iwe huru. Mwishowe, katika kiangazi cha 1975, nchi ya Ureno iliacha utawala wote wa nchi hiyo mikononi mwa chama kikuu cha maasi, “Front for the Liberation of Mozambique” (kinachofupizwa kwa kawaida kuwa Frelimo​—“Kikosi cha Kukomboa Msumbiji.”) Ule mpambano mrefu ukaisha. Msumbiji ikawa na kipindi kipya.

Lakini, kati ya miezi minne baada ya utawala kubadilishwa, shughuli ilianzwa ya kumaliza wachache wa nchi hiyo​—Mashahidi wa Yehova. Wao ni karibu 7,000 tu kati ya wakaaji 8,000,000 wa Msumbiji. Wakilinganishwa na taifa zima, wachache hao ni kama mtoto mdogo, asiye na ulinzi wa kimwili, nao sasa wamenyimwa ulinzi wa kisheria wa uhuru wao wa msingi.

Ripoti zilizopokewa kutoka Msumbiji, kuanza na sehemu ya mwisho ya Oktoba 1975, zaonyesha kwamba wengi sana wamekamatwa. Karibu Mashahidi wote wa Yehova 7,000 wa Msumbiji wamefungwa. Kila nyumba iliingiwa kutafuta na kukamata wanaume, wanawake na watoto. Wanaume walikamatwa kazini pao bila ya kuweza kwenda kuonana na jamaa zao. Mara nyingi walikamatwa kwa kupigwa-pigwa vibaya sana. Inaelekea kwamba kusudi la kufanya hivyo ni kumaliza kabisa Mashahidi wa Yehova na ibada yao katika nchi yote ya Msumbiji. Wakifaulu kufanya hivyo jambo moja laweza kutokea: Kukataza uhuru wa ibada, kanuni ambayo imewekwa imara katika katiba ya nchi iliyo huru sasa ya Msumbiji.

Lakini kwa sababu gani? Kwa sababu gani wajaribu kufutilia mbali watu wanaojulikana duniani pote kuwa wenye kutaka amani na wasiodhuru kisiasa? Mashahidi wa Yehova wamefanya nini ndiyo watendwe hivyo? Matendo yao Msumbiji yaonyesha nini? Ukweli unapofunuliwa kwa kuondoa porojo-porojo, wanaonekana kuwa wenye kusifika sana, hasa katika hiki kiitwacho “Kizazi cha Elimu.”

(Itaendelezwa)

[Maelezo ya Chini]

a Tazama Mnara wa Mlinzi wa Mei 15, 1976, na Juni 15, 1976 upate ripoti ndefu zaidi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki