Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 7/8 kur. 26-27
  • Kuvuta Sigareti—Hatari Zilizopo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuvuta Sigareti—Hatari Zilizopo
  • Amkeni!—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Hasara Kubwa!
  • Kuchanganua Udhuru Mbaya Ulivyo
  • Kuwa Mwenye Hali Bora Kabisa Kiroho
  • Kwa Nini Uache Kuvuta Sigareti?
    Amkeni!—2000
  • Watetea Tumbaku Waanzisha Puto la Hewa-Joto
    Amkeni!—1995
  • Unaweza Kuyavunja Mazoea ya Tumbako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Wauzaji wa Kifo—Je! Wewe Ni Mnunuzi?
    Amkeni!—1990
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 7/8 kur. 26-27

Maoni ya Biblia

Kuvuta Sigareti—Hatari Zilizopo

KATIKA miaka ya 1950, kampuni moja ya sigareti ilitangaza aina ya sigareti yayo kuwa ni “kitu kile hasa kilichoagiziwa na daktari.” Zikitoa uhakika mwingi, shime hizo zilitukuza sigareti kuwa misaada kwa afya na nguvu—lakini zimekoma! Hizi ni siku ambazo serikali hutaka pakiti za sigareti zionyeshe vibandiko vinavyoonya juu ya hatari nzito za kiafya.

Hata hivyo, watu fulani walio wavutaji-sigareti hushikilia sana wazo la kwamba ‘sigareti hunisaidia kufikiri na kufanya kazi vizuri zaidi.’ Huenda wakapuuza tisho la afya kuwa si baya sana kuliko lile la kula vitamutamu ili kupata nishati za haraka au kunywa kahawa ili kuwa na mwanzo mzuri asubuhi. Au huenda wakasema hatari ya kuvuta sigareti huwa ya kimwili tu. Je! wangeweza kuwa wanasema kweli? Je! kuna sababu ya kubishania kwamba sigareti—ijapokuwa hatari zote zile—ingeweza kuwasaidia wafanye mambo vizuri zaidi?

Hasara Kubwa!

Kama kwa kweli sigareti huthawabisha mvutaji kwa kumfanya awe chonjo zaidi na kumfanya aweze zaidi mambo au humfanya tu awazie-wazie hivyo, hakuna shaka kwamba thawabu hiyo huja kwa hasara kubwa. Zaidi ya hatari ya kupata kansa na ugonjwa wa moyo hatimaye, fikiria tokeo lililo la mara hiyo: Mnamo sekunde saba hadi kumi za kila mpulizo, mvutaji huhisi raha ya dawa fulani ya kulevya, nikotini: “Hiyo huwa ya utumizi wa kibinafsi,” asema Nina Schneider tabibu wa uhusiano wa dawa za kulevya na hali za akilini kwenye Chuo Kikuu cha Kalifornia, “nayo hudhibiti tabiamoyo na utendaji. Hiyo ndiyo hufanya iwe yenye kuzoeleza sana utumizi.”

Je! huwa yenye kuzoeleza sana kama heroini na kokeni? Ndiyo, akasema mpasuaji mkuu wa United States katika onyo lililotolewa Mei 16, 1988. Alieleza kwamba, uzoelevu huu wa kimwili ndio hufanya wavutaji fulani ‘waendelee tu kujapokuwa na matokeo mabaya ya kimwili, ya kiakili au ya kijamii.”

Nayo ni matokeo yaliyoje! Kufikia 1985 uvutaji sigareti ulisababisha vifo 100,000 kwa mwaka katika Uingereza, 350,000 kwa mwaka katika United States, na theluthi moja ya vifo vyote katika Ugiriki. Ni vigumu kulitolea udhuru dhara kubwa hivyo kwa afya ya umma. Mhalifu mwenyewe, ambaye ni moshi wa tumbako, si kwamba tu hana mafaa yoyote ya kuwa chakula au kinywaji mwilini bali ni mwenye kudhuru kindani.

Basi, je! nikotini iliyo katika moshi wa tumbako ni mbaya kuliko kafeni iliyo katika kahawa, chai, au chokoleti? Kutokana na maoni ya kitiba, hakuna ulinganisho. Asema hivi Dakt. Peter Dews, mtafiti wa kafeni kutoka Chuo Kikuu cha Harvard: “Kwa ujumla, kafeni si kisababishi kikubwa cha afya mbaya katika taifa kama vile uvutaji sigareti ulivyo.” Lakini hilo shtaka la kitiba kuhusu uvutaji sigareti ni mwanzo tu.

Kuchanganua Udhuru Mbaya Ulivyo

Ili kuona kwa nini uvutaji sigareti umo katika hali tofauti kabisa na chakula na vinywaji, fikiria umbo la mwili wako. Mhubiri 7:9 husema kwamba “Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi.” Ingawa kula ni utendaji wa kiasili wa mwili wako kutoka kwa Mungu, matumizi mabaya ya dawa zisizo za kitiba ni uvumbuzi wa kibinadamu. Vitu hivi vyenye kuzoeleza utumizi haviwezi kuwa na utumizi wa kiasili ulio wa kiasi. Viwe vinavutwa, vinamezwa kama vibonge, au vinadungwa mishipani kwa sindano, hivyo huchochea na kupotosha utendaji mbalimbali wa kimwili kwa njia zilizo kinyume cha asili.

Tofauti na hivyo, karibu chakula au kinywaji chochote kitakupa baadhi ya mahitaji yako ya kawaida ya mwili yawe ya fueli (mafuta-nishati), ukuzi, na urekebishaji wa tishu. Ni kweli kwamba watu walio na matatizo fulani ya afya ni lazima waepuke chakula chenye vihifadhi, shahamu zilizoshikamana sana, au kafeni. (Kwa mgonjwa wa sukari, sukari ya kawaida ni hatari.) Lakini kwa watu walio wengi, hata vyakula hivi vina thamani fulani ya kulisha mwili na, vikitumiwa kwa kiasi, havina madhara. Lakini uvutaji sigareti ni jambo tofauti kabisa.

Hata sigareti moja au mbili ina ushawishi hatari, kama vile kutumia kokeni mara moja ili kuona raha. Uchunguzi mmoja wa serikali ya Uingereza ulipata kwamba vijana walipovuta mara chache kama vile sigareti mbili, walikuwa na uwezekano wa asilimia 15 tu wa kubaki bila kuwa wavutaji sigareti.

Kuwa Mwenye Hali Bora Kabisa Kiroho

Kwa uhakika huwezi kuwa mwenye hali bora kabisa ukiwa mtumwa hoi mwenye kutegemea kimwili dawa za kulevya—ile “michocheo isiyokinzika” ya nikotini kama ilivyoelezwa na mpasuaji mkuu wa United States. Badala ya kuacha mwili wako ukuongoze wewe kama mtumwa wao, Biblia hutaka kujidhibiti, ile nguvu ya ‘kuutumikisha.’—1 Wakorintho 9:24-27.

Si kwamba tumbako hushambulia tu mnofu wa mvutaji sigareti—kukiwa na hatari ya kupata kansa, msakamo wa hewa mapafuni, na ugonjwa wa moyoni—bali pia hushambulia nguvu zake za hiari. Hivyo, kwa kumchafuza kwa njia isiyoonekana wazi, tabia hiyo hukaribia kutumikisha kabisa utu au nia ya mvutaji sigareti. “Kwa miaka 26,” akakiri mwandikaji mmoja katika gazeti Time, “Mimi nimekuwa mtumwa kwa sigareti. Kwa angalau [miaka] kumi, nimekuwa nikijaribu kujikomboa. Mahohehahe wa nikotini ambao wamejaribu-jaribu kuondolea mbali tabia hiyo na kushindwa ndio pekee wawezao kuthamini kabisa jinsi ilivyo vigumu kuiacha.”

Biblia hutupa wajibu, sisi tupendwao na Mungu, “tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho.”—2 Wakorintho 7:1; Kingdom Interlinear.

Kwa nini Mungu apaswe kujali tutumiapo vibaya miili yetu wenyewe na nguvu za akili? Sababu ya wazi kabisa ni kwamba yeye ndiye Muumba wetu mwenye upendo, mwenye kuhangaikia kwamba tuishi kulingana na uwezo wetu kamili wa kuwa uumbaji wake. Akivutia akili yetu ya kusababu, asema hivi: “Mimi ni BWANA [Yehova, NW], Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida [si ili ujidhuru].”—Isaya 48:17.

Basi, wito halisi wa ushindani ni kwamba kwa faida yetu wenyewe tuchunguze maoni yetu kwa unyoofu. Ni kazi bure kutetea uvutaji sigareti kwa sababu hutuliza mtu au kwa sababu ya “faida” nyinginezo ambazo huwa tu ni kutaka kuepa yale maumivu makali yatokeapo kwa kuacha nikotini. Kitiba, uvutaji sigareti umekuwa balaa kwa afya ya umma; lakini kidini, uvumbuzi huu wa kibinadamu wa kuingiza nikotini katika mkondo wa damu kupitia mapafuni umepuuza viwango safi vya Muumba wetu na huchafuza na kushusha hadhi ya mwili wa kibinadamu. Kwa hiyo mbona ukaribishe matata? Ni vizuri zaidi kutii mithali hii: “Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; bali wajinga huendelea mbele wakaumia.”—Mithali 22:3.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 26]

Vincent van Gogh, Skull With Cigarette (Fuvu la Kichwa Lenye Sigareti), 1985, Kwa Hisani ya National Museum, Amsterdam, Uholanzi

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki