Farasi Mweupe-Mweupe Asonga Mbele
NABII Yohana alivuviwa na Mungu kutabiri wakati ambapo vipuku vya magonjwa vingeenea sana sehemu zote za dunia kama farasi mweupe-mweupe mwenye kwenda shoti akiwa amepandwa na kifo. (Ufunuo 6:8) Mweneo wa kugutusha wa UKIMWI ni uthibitisho mkali zaidi wa kwamba tunaishi wakati huo. Kwa uhakika, maofisa wa afya wa Jiji la New York waeleza vuvumko la UKIMWI kuwa “kipuku ambacho kingekuja.”
Katika Thailand, 70 ya mikoa 73 sasa ni mahali pa vairasi ya UKIMWI. Katika 1987 asilimia 1 tu ya watumiaji wa dawa za kulevya katika Bangkok walikuwa na UKIMWI; kufikia katikati ya 1989 zaidi ya asilimia 40 walikuwa nao. Brazili yatarajia visa vilivyothibitishwa 75,000 vya UKIMWI katika muda wa miaka mitatu, kukiwa na wengine milioni 1.5 walioambukizwa. Kati ya benki za damu 1,200 za Brazili, ni asilimia 20 tu zilizokuwa zimechunguza kwa ugavi wa damu katika 1988, na asilimia 14 ya wenye kuteswa na UKIMWI walipata ugonjwa huo kutokana na damu yenye ambukizo. Katika Rio de Janeiro na São Paulo, karibu asilimia 75 ya wagonjwa wenye hitilafu ya damu kutogandamana huambukizwa. Katika Côte d’Ivoire, kufikia asilimia 10 ya wanawake wenye mimba na asilimia 10 ya wachangaji damu wana UKIMWI.
Ofisa mmoja wa tiba Amerika alisema hivi kwenye mkutano wa mataifa 87 kuhusu UKIMWI: “Kipuku cha HIV [vairasi ya UKIMWI] kimeruka mipaka ya udhibiti katika United States na katika ulimwengu.” Vitovu vya United States vya Udhibiti wa Magonjwa vyakadiria kwamba kufikia 1998 Waamerika milioni mmoja watakuwa na ugonjwa huo ukiwa umekomaa kabisa, huku wengi zaidi wakiwa na vairasi hiyo. Makadirio ya hesabu ya ambao tayari wana vairasi hiyo ilichunguzwa upya hivi majuzi ikawa ya juu ajabu. Katika Jiji la New York, UKIMWI sasa ndicho kisababishi cha tatu kinachoongoza cha kifo, ukipitwa tu na ugonjwa wa moyo na kansa.
Benki za damu zimeshtakiwa kwa kugawa damu yenye ambukizo la UKIMWI ili itiwe mishipani. Kadhaa zimeagizwa zilipie hasara. Huenda bado zikakabili mashtaka zaidi sheriani. Wakili mkuu wa Shirika la Kiamerika la Benki za Damu aliomboleza hivi: “Wakati ujao una nini? Mimi sijui. Kisa kibaya zaidi kiwezacho kuwaziwa ni kumalizika kabisa kwa vitovu vya damu.”
Karibuni, kwa kweli kutakuwako mwisho wa benki za damu zote za ulimwengu kwa sababu tunaukaribia wakati wenye ulimwengu usio na UKIMWI, ulimwengu usio na hospitali, magonjwa, au kifo. Yohana, aliyeeleza juu ya kusonga mbele kwa farasi mweupe-mweupe, alirekodi pia ahadi ya Mungu ya “dunia mpya,” jamii ya kibinadamu yenye kuwekwa huru na pigo la ugonjwa. (Ufunuo 21:1-4) Ni jambo la hima kukadiria ubora wa ahadi hiyo sasa, kwa maana kwa sasa farasi mweupe-mweupe asonga mbele.