Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 3/8 kur. 5-7
  • Je! Kweli Kweli Tunahitaji Serikali?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Kweli Kweli Tunahitaji Serikali?
  • Amkeni!—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Asili ya Utawala wa Kibinadamu
  • Zote Zafanana—Lakini Zatofautiana
  • Kuwa Raia wa Serikali ya Mungu
    Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani
  • Mahitaji Wanayotazamia Watu Kutimiziwa na Serikali
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Namna Mahitaji Yetu Yatakavyojazwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Utawala wa Kibinadamu Wapimwa Katika Mizani kwa Nini?
    Amkeni!—1991
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 3/8 kur. 5-7

Utawala wa Kibinadamu Wapimwa Kaitka Mizani

Je! Kweli Kweli Tunahitaji Serikali?

ANARKI: Kutokuwapo umbo lolote la mamlaka ya kisiasa, kunakotokeza jamii ya watu mmoja mmoja wasio na serikali, ambao hujidaia uhuru kamili.

MWANAFALSAFA Mgiriki Artistotle alisema maumbo yote ya serikali za kibinadamu kwa asili si thabiti na kuwa ya muda. Yeye alidai, kulingana na mwandikaji mmoja, kwamba “uthabiti wa tawala zote umepotolewa na uwezo wenye kuharibu wa wakati.”

Kwa sababu ya hali hizo, haishangazi kwamba watu fulani wametetea kutokuwapo kwa serikali yoyote, au angalau kuwapo kwa serikali kwa kadiri ndogo iwezekanavyo. Lakini kutetea ‘kutokuwapo kwa serikali’ kwa halisi ni kutoa wito wa anarki, usemi unaotokana na neno la Kigiriki linalomaanisha “kutokuwa na mtawala.”

Neno “anarki” lilitumiwa katika 1840, miaka 150 hivi iliyopita, na Pierre-Joseph Proudhon, mwandikaji wa kisiasa Mfaransa. Lakini falsafa ya uarnaki ilionyeshwa waziwazi miaka 200 mapema na Mwingereza Gerrard Winstanley. Kama inavyoelezwa katika The New Encyclopædia Britannica, “Winstanley alitokeza zile ambazo baadaye zilikuja kuwa kanuni za msingi miongoni mwa waarnaki: kwamba mamlaka hupotoa; kwamba hakuna upatano kati ya mali na uhuru; kwamba mamlaka na mali ndizo zitokezazo uhalifu; na kwamba ni katika jamii isiyo na watawala tu, ambapo kazi na mazao yayo hushirikiwa, ndimo watu waweza kuwa huru na wenye furaha, wakitenda si kulingana na sheria zilizofikilizwa kutoka juu bali kwa kulingana na dhamiri zao.”

Lakini je! tuliyojionea hayatufundishi kwamba kila kikundi huhitaji muundo fulani wa kutendea? “Tangu nyakati za mapema zaidi,” chasema The World Book Encyclopedia, “aina fulani ya serikali imekuwa sehemu muhimu ya kila jamii.” Chaeleza kwamba “kila kikundi cha watu—kuanzia familia hadi taifa—kina amri za mwenendo zinazoongoza maisha ya washiriki wacho.” Kama sivyo kingeweza kutimiza makusudi yacho kwa faida ya washiriki wacho wote kwa njia gani nyingineyo?

Kwa hiyo watu walio wengi watakubali mara moja wazo la kwamba matengenezo fulani yana haki halali ya kutumia mamlaka na kufanya maamuzi kwa faida ya wote. Bila kuwapo kwa serikali ya kufanya maamuzi kwa ajili ya jamii, kila mtu angeachwa afuate miongozo ya dhamiri yake mwenyewe, kama alivyodokeza Winstanley. Je! hilo lingetokeza umoja? Au je! haielekei zaidi kwamba kila mtu angefuatia faida zake mwenyewe, mara nyingi iwe ni kwa hasara ya haki za wengine ambazo ni zenye halali pia?

Majaribio ya anarki yameshindwa kufanya fungu la ainabinadamu liwe bora zaidi. Jitihada za maharamia wa karne ya 20 za kuondoa uthabiti wa jamii, kuharibu kile wanachodhania kuwa kinawaharibu, hazikupata kuwa na matokeo bora zaidi.

Kwa maneno rahisi, ‘kutokuwa na serikali’ hualika mchafuko. Kwa hiyo suala si ‘je! kuwepo serikali au kusiwepo?’ bali, badala yake, ni ‘je! kuwe serikali ya aina gani ili kuwepo matokeo bora zaidi?’

Asili ya Utawala wa Kibinadamu

Utawala wa Mungu ndio uliokuwa kigezo cha kwanza kilichowekewa mwanadamu katika shamba la Edeni miaka zaidi ya elfu sita iliyopita. Muumba alikazia utegemeo wa ainabinadamu juu ya mwelekezo wake wa mambo kwa kupatana na kanuni iliyoelezwa baadaye katika Biblia: “Njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu.” (Yeremia 10:23) Au ni kama mithali moja ya Kichina isemavyo: “Bila ya msaada wa Mbingu mwanadamu hawezi kutembea inchi moja.”

Binadamu wawili wa kwanza walikata kauli vingine. Walichagua kutembea “bila ya msaada wa Mbingu” na kwa hiyo wakalazimishwa watembee njia yao ya kutoka kwenye Paradiso ambayo Mungu alikuwa amewapa. Baadaye, kwa kadiri ambavyo familia ya kibinadamu ilivyoongezeka, uhitaji wa amri za serikali ya kuhakikisha amani na utaratibu ndani ya mpango huo uliongezeka pia. Mara tu utawala wa Mungu ulipokuwa umekataliwa, utawala wa kibinadamu, kwa lazima, uliingia kujazia pengo hilo.—Mwanzo 3:1-5.

Zote Zafanana—Lakini Zatofautiana

Kutokana na mwanzo huo mbaya, serikali za kibinadamu zimechukua maumbo mengi. Ziwe zenye mambo machache sana au mengi mno, zote zafanana kwa njia fulani. Hapa kuna chache:

Serikali hutunza mahitaji ya raia zazo. Serikali inayoshindwa kufanya hivyo hupoteza uhalali wayo.

Serikali huweka katiba ya mwenendo, ambao kama haikufuatwa na raia wazo, tokeo huwa ni adhabu. Katiba hiyo yajumlisha amri na sheria, na pia mapokeo ambayo yamesitawi kwa muda wa karne zilizopita. Kwa sehemu kubwa raia hutii katiba hiyo ya mwenendo ama kwa sababu wanafahamu manufaa zinazopatikana kwa kufanya hivyo, kwa sababu wanaona ‘hilo ndilo jambo la kufanya,’ kwa sababu wanakuwa chini ya mkazo wa wenzao, au kwa sababu tu wataadhibiwa wasipofanya hivyo.

Serikali hutoa utumishi wa kutunga sheria, kutoa usimamizi, na kutoa hukumu kupitia aina fulani ya tengenezo. Sheria hutengenezwa, haki hutekelezwa, na miongozo hufanyizwa.

Serikali hudumisha vifungo vya kiuchumi vyenye nguvu na ulimwengu wa biashara.

Serikali pia hujiunga mara nyingi na umbo fulani la dini, nyingine zazo kwa ukaribu zaidi ya nyinginezo. Hizo hufanya hivyo ili kuupa utawala wazo uhalali fulani—‘baraka ya mbingu’—ambayo kama sivyo hazingekuwa nayo.

Bila shaka, serikali mbalimbali hutofautiana. Wanasayansi wa kisiasa huzipanga na kuziweka kwa njia kadhaa. “Kwa kielelezo, kuna,” chaandika The New Encyclopædia Britannica, “tofauti ya msingi baina ya serikali kwa maana ya hesabu ya watawala—serikali ya binadamu mmoja (ya kifalme au kimabavu), serikali ya wachache (ya kikabaila au ya wachache), na serikali ya wengi (demokrasi).”

Nyakati nyingine serikali hupangwa kwa maana ya matengenezo yazo makuu (ubunge, serikali ya mawaziri), kwa kulingana na kanuni za msingi za mamlaka ya kisiasa (ya kimapokeo, ya haiba), kwa kulingana na muundo wazo wa kiuchumi, au kwa maana ya matumizi yazo mazuri au mabaya ya uwezo. “Ingawa hakuna yoyote inayotia ndani mambo yote,” chasema kitabu hicho cha marejezeo, “kila ya kanuni hizo za uchanganuzi inakubalika kwa kadiri fulani.”

Lakini bila kujali tunazipangaje, jambo la muhimu la kukumbukwa ni kwamba maumbo mbalimbali ya utawala wa kibinadamu—yote kwa ujumla—sasa yanapimwa katika mizani. Hilo litakuwa na matokeo makubwa kwetu sote.

[Sanduku katika ukurasa wa 6]

Akiandika juu ya mamlaka za kiserikali zinazotawala hadi wakati huu wa kisasa, mtume Paulo aliandika hivi: “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu.” (Warumi 13:1, 7) Kwa hiyo, Wakristo wanaofuata uongozi wa Biblia kwa kudhamiria hutii sheria zote za nchi wanamoishi, isipokuwa wanapotakwa wavunje sheria za Mungu, ambazo ndizo zilizo juu zaidi.

[Picha katika ukurasa wa 7]

Serikali ni ya lazima—kama vile ilivyo lazima magari yaongozwe—ili kuzuia mchafuko

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki