Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 5/8 kur. 3-4
  • Kuvumbua Jinsi Ulivyo Hasa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuvumbua Jinsi Ulivyo Hasa
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Tabia Zilizorithiwa Hufanyiza Sehemu Kubwa
  • Vipi Juu ya Ulaji, Mizio, Mazingira?
  • Dini Ina Sehemu Gani?
  • Jinsi Unavyoweza Kubadili Namna Ulivyo
    Amkeni!—1992
  • Kwa Nini Ubadili Jinsi Ulivyo?
    Amkeni!—1992
  • Kulea Mtoto Aliye Mgumu
    Amkeni!—1994
  • Dhibiti Maisha Yako Sasa!
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 5/8 kur. 3-4

Kuvumbua Jinsi Ulivyo Hasa

UANGALIAPO kwenye kioo, unaona nini? Rudisho la umbo lako la kimwili. Lakini je! hilo lakuambia jinsi ulivyo hasa? Je! lakuambia jinsi wengine wanavyokuelewa ukiwa mtu? Je! kweli unajua jinsi ulivyo? Unajua jinsi tabia yako ilivyo tangu mwanzoni? Naam, wewe ulikuaje ukawa na utu ulio nao?

Unapotua ili kuchanganua mambo yote yaliyofanyiza utu wako, huenda ukatambua kwamba umepashwa mambo mengi yaliyokuathiri—iwe ni kutoka kwa watu wengine au mambo mengine. Katika miaka ya mapema ya kufanyizwa kwetu, wengi wetu hatukuweza sana kujiamulia tabia na njia ambazo zingeimarika ndani yetu. Kwa hivyo acha tuangalie baadhi ya mavutano hayo yenye kufanyiza utu yaliyowekwa juu yako—baadhi yayo yakiwekwa muda mrefu kabla hujaweza kufanya lolote kuhusu tabia yako mwenyewe.

Tabia Zilizorithiwa Hufanyiza Sehemu Kubwa

Je! umeathiriwa kadiri gani na tabia zilizorithiwa? Vichukua tabia, vinavyopatikana katika kromosomu zinazopisha tabia za urithi, hubeba maelezo na maagizo yaliyofupizwa kwa ukuzi wa kila mtu. Kwa hivyo ni kadiri gani ya tabia yako iliyoathiriwa na urithi? Inaonekana bado ni vigumu kuthibitisha ufungamano wowote kati ya urithi na utu. Hata hivyo, kuna maoni fulani yanayoonekana kustahili. Kwa kielelezo, tabia kadhaa ulizorithi zinaleta matokeo ya mara iyo hiyo juu ya tabia yako. Hivyo, watu wengine hurithi tabia za unyamavu, hali wengine ni wenye kutokeza sana.

Mwanamke mwenye mimba anaweza kufaidi mtoto wake asiyezaliwa au kumdhoofisha kwa matendo yake mwenyewe, fikira, na hisia. Ni amani au usumbuo wa kadiri gani uliopata ulipokuwa katika tumbo la uzazi la mama yako? Ulijifunza kadiri gani kutokana na hali ya sauti ya wazazi wako, muziki waliosikiliza? Uliathiriwa kadiri gani na chakula ambacho mama yako alikula? Kama alikunywa kileo au akatumia dawa za kulevya, aliathiriwa nazo kadiri gani? Kufikia wakati ulipozaliwa, mengi ya maelekeo yako yalitokezwa na labda ni vigumu kuyabadilisha.

Vipi Juu ya Ulaji, Mizio, Mazingira?

Kadiri ulivyoendelea kukua katika utoto, vyakula fulani vilikuwa na athari kwa tabia yako. Vitia-utamu, rangi zinazoongezwa chakulani, na vihifadhi chakula—vyote vyaweza kuathiri sana tabia bila kugundulika. Kucheza-cheza kunakopita kiasi katika watoto, mkazo ulioongezeka, unyeti, maumivu ya neva, na matendo ya kukosa kiasi na yasiyozuilika ni baadhi tu ya matokeo. Uchafuzi wa hewa kutoka kwa magari na viwanda, na sumu nyingine za mazingira pia huunda tabia. Au, katika hali ya kibinafsi, huenda ukawa na kiathiri-kibaya ambacho hukuathiri vibaya lakini kisiwe na madhara kwa wale walio karibu nawe.

Pamoja na mavutano haya, tabia ya wazazi wako, mambo wanayopenda na wasiyopenda pamoja na machukio yao ambayo umeishi nayo kutoka utotoni, yana athari kwako na yameunda utu wako kwa kiwango fulani. Tokeo ni kwamba nyingi za njia zako na mtazamo wako wa jumla kwa maisha unafanana na wao. Unaelekea kukasirishwa na mambo ambayo huwakasirisha. Unaelekea kuvumilia mambo ambayo wanavumilia. Na hutambui kwamba unaigiza tabia yao mpaka mwingine akuambie kwamba unatenda tu kama baba au mama yako. Hali yao ya kifedha na ya kijamii ilikuathiri na vilevile ujirani na mazingira ya shule. Marafiki na mashirika yako pia yamekuwa na athari kubwa kwako. Labda aksidenti mbaya (kwako au kwa rafiki wa karibu), msiba fulani wa mahali unapoishi, au hata matukio yenye kusumbua ya ulimwengu yamekuathiri wewe. Au labda msiba fulani, kama vile talaka au ugonjwa mbaya, umeacha kovu juu ya utu wako.

Unapofikiria ya nyuma je! unaweza kutambua uvutano wowote kama huo?

Dini Ina Sehemu Gani?

Kwa kudhania, dini inapaswa kukusaidia uwe mtu bora, kufanya tabia yako ya adili, adabu zako, na maisha ya kila siku yapate maendeleo. Hasa ni kadiri gani ya thamani na matendo yako imeathiriwa na dini? Ingawa dini inapaswa kutenda kama kizuizi kwa tabia ya kihalifu, ya kutojali, watu wengi wanapohusika na dini wanaathiriwa katika njia tofauti. Wanatambua unafiki na kukazia kwa makanisa vitu vya kimwili badala ya thamani za kiroho na hivyo huona uchungu. Hata huenda waache kuwa watu wa dini, hali ya kiroho na tumaini.

Huenda ukaweza kufikiria mavutano mengine ya nje ambayo yanaweza kuunda tabia. Hebu tumia dakika chache tu ukiwazia mambo ambayo huenda yamekuathiri sasa. Je! unaweza kuorodhesha baadhi yayo? Si rahisi kuona mambo jinsi yalivyo hasa na kufikiri kwa njia hiyo, lakini jitihada hiyo inastahili na huenda ikakusaidia. Katika njia gani?

Ikiwa unaweza kutambua uvutano fulani au kisababishi cha mwelekeo fulani usio mzuri katika tabia yako, ikiwa unaweza kuutenga, utakuwa katika hali nzuri zaidi ya kuudhibiti, labda hata kuubadili. Ikiwa unaweza kuudhibiti, au hata kuondoa uvutano usiofaa, ungeweza kuwa mtu tofauti, ukienenda katika njia inayofaa kuelekea wengine.

Bila shaka, huo ni mwito wa ushindani. Lakini kwa vile mengi wa mavutano katika tabia yako yametwikwa juu yako na watu wengine au na hali ambazo hukuweza kuzidhibiti, kwa nini usichukue hatua ya kwanza kujirekebisha mwenyewe hali hiyo? Ikiwa utapata maendeleo, kwa nini usibadili jinsi ulivyo?

[Blabu katika ukurasa wa 4]

Matendo na hisia za mwanamke mwenye mimba zaweza kuathiri mtoto wake asiyezaliwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki