Kutoka kwa Wasomaji Wetu
Kupokea Uchambuzi Mapema Leo nimepokea uchambuzi kwa ajili ya mradi niliokuwa nikifanya kwa majuma fulani. Ingawa uchambuzi huo ulikuwa na faida, msimamizi wangu alikuwa mkali. Niliudhika sana. Nilipofika nyumbani, nikasoma makala “Je! Unachukia Kupokea Uchambuzi?” (Novemba 8, 1991) Lilibadili mtazamo wangu.
D.B., United States
Makala hiyo ilikuwa yenye kusaidia sana. Nikiwa nimechambuliwa hivi karibuni, nilihisi nimeshuka moyo na nikiwa nimekata tamaa. Hata hivyo, kwa kusoma makala tena na tena, nilisaidiwa kushinda tatizo langu.
N.O., Japan
Unywaji na Uendeshaji Gari Nilichochewa sana na makala juu ya “Unywaji na Uendeshaji Gari—Mchanganyiko Hatari.” (Februari 8, 1992) Dada yangu mchanga wa miezi tisa aliuawa katika aksidenti ya gari miaka 31 iliyopita. Bado namwombolezea. Dereva mlevi alijipondesha kwenye gari letu. Bado naweza kumwona mama yangu akiwa amefunikwa na damu na dada yangu mdogo akiwa mfu juu ya kiti chake. Nina furaha kuwa na imani katika ufufuo, lakini natumaini sana kwamba makala hiyo itafanya wengine wafikiri upya ikiwa watakunywa na kuendesha gari.
K.N., United States
Nina umri wa miaka 16. Makala “Wakosaji Wakabili Wenye Kupatwa na Msiba” ilikuwa na yaliyoonwa yenye kuchochea na yakanifanya nitokwe machozi. Ninahisi kwamba makala hii itasaidia wengi wa vijana kama mimi kuwafikiria wengine na kutokuwa wazembe katika utumiaji wa kileo.
R.G., Ujerumani
Kuwatunza Wazee Wazee Makala juu ya “Utunzaji wa Wazee-Wazee—Tatizo Lenye kukua” (Oktoba 8, 1991) ilinipa kitia moyo kingi sana. Baba yangu mwenye miaka 86 sasa ana ugonjwa wa Alzheimer, na nilitaka kumtunza nyumbani badala ya kumpeleka hospitali. Kwa kuwa hali yake imekuwa mbaya zaidi, magumu na mkazo wa akili unaotia ndani utunzaji wake yameongezeka! Nilifikia kuwa hoi kabisa. Lakini nikasoma makala zenu. Nikiwa nimefarijiwa zaidi, machozi yalinitoka. Kuna matatizo mengi sana na nyakati ngumu mbele, lakini azimio langu la kumtunza baba yangu hadi mwisho limepata nguvu.
T.H., Japani
Kuwaheshimu Wazee-Wazee Asanteni kwa makala “Je! Unawaheshimu Wazee-Wazee?” (Oktoba 8, 1991) Baada ya miaka 40 ya utumishi mshikamanifu kwa Mungu, mama yangu alihitaji utunzi mwingi kwa sababu ya ugonjwa wa Alzheimer. Kalenda iliyochapishwa na Watch Tower Society imekuwa ya msaada mkubwa, kwa sababu wageni waliomtembelea walikuwa wakiandika majina yao siku ile waliomtembelea. Kwa hivyo nilimkumbusha kwamba si mimi peke yangu niliyekuwa nimemtembelea, kwa kuwa zaidi ya nusu ya tarehe zilijawa na majina! Pia, yeye alitunzwa vizuri sana na wafanya kazi wa nyumba ya utunzi kwa sababu walijua watu wengi sana walipendezwa naye. Asanteni kwa kutujali.
W.J.H., United States
Mama yangu, akiwa amepooza kuanzia kiuno hadi chini, huenda haja pale pale alipo kwa kutojiweza. Kila asubuhi ni lazima tumwoshe na kubadilisha matandiko yake kabisa. Ni lazima avishwe na alishwe, na mara nyingi anahitaji utibabu wa kitiba. Mume wangu na watoto wangu ni msaada mkubwa, lakini sehemu kubwa ya daraka lanikalia. Wakati mwingine kuna kuvunjika moyo, na roho ya kujikana inahitajiwa wakati wote. Ilikuwa basi shangwe kusoma makala zenu. Asanteni sana kutoka moyoni.
L.D., Italia
Mfano kwa Ndugu Wachanga Makala yenu “Vijana Wanauliza . . . Nawezaje Kuwa Mfano kwa Ndugu na Dada Zangu Wachanga?” iliniathiri sana. (Aprili 8, 1991 Kiingereza) Nikiwa mkubwa kwa watoto watatu, naweza kusema tu kwamba ingalikuwa vizuri kama ningalisoma makala hiyo katika ujana wangu. Sasa nina watoto wangu mwenyewe na nafurahi kwamba watakuwa na shauri zuri la kufuata.
L.K., Ujerumani