Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 6/8 uku. 31
  • UKIMWI Katika Afrika Onyo kwa Ulimwengu!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • UKIMWI Katika Afrika Onyo kwa Ulimwengu!
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • UKIMWI—Je! Nimo Hatarini?
    Amkeni!—1993
  • Kusaidia Wale Walio na UKIMWI
    Amkeni!—1994
  • UKIMWI— Shida kwa Matineja
    Amkeni!—1992
  • UKIMWI—Matokeo Yenye Msiba Mkubwa kwa Watoto
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 6/8 uku. 31

UKIMWI Katika Afrika Onyo kwa Ulimwengu!

“IKIWA una mpenzi 1 kila mwaka kwa miaka 6, nao wapenzi wako wafanye vivyo hivyo, yaelekea utakuwa umefanya ngono na watu 45 000.” Hesabu hii sahili iliyofanywa na Dakt. K. E. Sapire, iliyonukuliwa katika jarida Continuing Medical Education la Afrika Kusini yafafanua uwezekano mkubwa wa ambukizo la UKIMWI ambao upo kwa wenye uovyo-ovyo wa kingono.

Kwa hivyo, kwa nini kukazia uangalifu katika Afrika?

Kwa sababu yanayotukia huko ni onyo kwa ulimwengu. Afrika si ndiyo mahali pekee ambapo uovyo-ovyo wa ngono umeenea. Hiyo ni kawaida ya tufeni pote. “Hatimaye,” asema mtaalamu wa UKIMWI Dakt. Dennis Sifris, “kila mtu mwenye kutenda kingono katika ulimwengu aliye na mpenzi zaidi ya mmoja yuko hatarini.” Vivyo hivyo, kulingana na gazeti U.S.News & World Report, kwa viwango vya sasa hata “ndoa si hakikisho la ngono ya kawaida—ama la uaminifu—na hivyo si kinga kamili dhidi ya UKIMWI.”

Hivyo basi, likiwa na sababu nzuri, jarida African Affairs laonya hivi: “Ugonjwa huu ungeweza kujitokeza kwingineko.” Ishara zote ni kwamba masaibu ya Afrika yako tayari katika mkondo wa kurudiwa tena katika sehemu nyingine nyingi za ulimwengu.

Kwa kielelezo, gazeti la Newsweek laripoti kwamba katika Brazili, “idadi zenye kupanda za wafanya ngono wa kawaida zimepata UKIMWI kutoka wapenzi wao walioambukizwa.” Wizara ya afya ya nchi hiyo yakadiria kwamba tayari nusu milioni wana virusi ya HIV. “Ikiwa jambo fulani halitafanywa,” asema Dakt. Carlos Alberto Morais de Sá, mkurugenzi wa utafiti wa UKIMWI kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Gaffrée e Guinle katika Rio de Janeiro, “tutakabiliwa na angamizo la afya ya umma.”

Marekani pia yahatarishwa. “Ingawa idadi ya visa vya ngono ya kawaida kwa kulinganishwa ni ndogo,” laripoti gazeti la Time, “iliruka 40% mwaka uliopita [1990], kwa kasi mno kuliko aina nyingine yoyote.” Lile juma baada ya kufunuliwa kwamba mwanariadha mashuhuri Magic Johnson alikuwa ameambukizwa UKIMWI kupitia mahusiano ya ngono ya kawaida, simu za watu walioshikwa na wasiwasi zilimiminika kwenye huduma za kitiba wakitaka kujua habari zaidi kuhusu huo ugonjwa.

Asia pia inatoa ishara zenye kutisha za msiba uelekeao kuifika. Eneo hilo la tufe limepatwa na ongezeko la wenye HIV kutoka yapata sufuri katika 1988 hadi zaidi ya milioni moja leo! “Viwango vya Afrika vya maambukizo vitaonekana kuwa vya kiasi kwa kulinganisha,” atabiri Dakt. Jim McDermott, akiripoti baada ya ujumbe wa kuchunguza uhakika wa mambo katika Asia. Yeye aongezea hivi: “Nimesadiki Asia ni jitu lililolala la ulimwenguni pote la ugonjwa wa Ukimwi.”

Kujaribu kuweka lawama kwa chanzo na usambaaji wa UKIMWI juu ya kontinenti moja hususa ama kikundi cha kitaifa ni bure na ubatili. Dakt. June Osborn, msimamizi wa Shule ya Afya ya Umma kwenye Chuo Kikuu cha Michigan, Marekani, aiweka hali hiyo waziwazi hivi: “Si kile ulicho wewe bali kile ufanyacho.”

Je, UKIMWI utaendelea kusababisha uharibifu wawo mkubwa kila mahali? Je, kuna suluhisho fulani, ama UKIMWI hatimaye utafyeka idadi ya watu katika maeneo makubwa ya kontinenti ya Afrika na sehemu nyingine za ulimwengu?

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

Picha ya WHO na H. Anenden; nyuma: picha ya NASA

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki