Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 1/8 kur. 3-4
  • Ulimwengu Wetu Umebadilikaje?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ulimwengu Wetu Umebadilikaje?
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Jamii ya Wanunuzi Iliyobadilika
  • Mabadiliko Katika Sayansi
  • Mabadiliko ya Kisiasa
  • ‘Na Ukuta Ukaanguka kwa Kishindo’
    Amkeni!—1992
  • Berlin—Wonyesho wa Jinsi Ulimwengu Wetu Ulivyo?
    Amkeni!—1991
  • Ulimwengu Wetu—Unaobadilika Huo Waelekezwa Wapi?
    Amkeni!—1993
  • Ni Nini Kinachotendeka Kwenye Umoja wa Mataifa?
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 1/8 kur. 3-4

Ulimwengu Wetu Umebadilikaje?

JE! ULIMWENGU wako umebadilika? Mwanafalsafa wa kale Mgiriki Heracleitus alisema: “Hakuna jambo linalodumu ila mabadiliko.” Mabadiliko yanaendelea kuwako katika maisha ya kila mmoja wetu.

Unapotazama nyuma miaka 10, 20, 30, au zaidi iliyopita, umeona mabadiliko gani? Huenda ikawa umeona mabadiliko yakija kwa namna ya usitawi na kutupilia mbali kanuni za kidesturi. Bila shaka, unaona mabadiliko mengine yakifaa na mengine yakiwa hayafai.

Ikiwa una umri wa miaka zaidi ya 70, umeona mabadiliko gani tangu ulipokuwa kijana? Unakumbuka wakati ambapo TV (televisheni) haikuwapo, wakati ndege ziliporuka kwa mwendo wa polepole wa kilometa 150 kwa saa, wakati usafiri mwingi wa kimataifa ulipokuwa kwa meli kubwa, wakati dawa za kulevya zilipotumiwa mafichoni mwa wavuta bangi tu, wakati magari yalipokuwa machache sana. Naam, kwa kweli ulimwengu wako umebadilika.

Jamii ya Wanunuzi Iliyobadilika

Lakini ulimwengu umebadilika hata kwa vijana. Miaka 45 tu iliyopita, masoko ya ulimwengu yalijaa bidhaa na ustadi wa nchi za Magharibi. Sasa, mataifa ya Mashariki yanayopakana na bahari Pasifiki yamekuja kuongoza katika uundaji wa magari, kompyuta, kamera, TV, na vifaa vingine vingi vya kielektroni.

Hilo linaonyeshwa na yale ambayo msafiri mjuzi Mchina aliliambia Amkeni!: “Miaka 30 au 40 tu iliyopita, ndoto ya Mchina wa wastani ilikuwa ni kupata baiskeli na cherahani. Hizo ndizo zilizoonyesha usitawi wa mtu siku hizo. Sasa ndoto ni kupata TV ya rangi, vidio, friji, na pikipiki.” Jamii ya wanunuzi, iwe iko Uchina au kwingineko, imebadilisha mapendezi yayo na uhitaji wayo.

Aina hiyo ya badiliko la maoni limetukia katika mataifa mengi kwa kadiri ambavyo uchumi wayo umeendelea. Pedro, Mkatalani aliye katika miaka ya mapema ya 40, alisema: “Miaka 30 iliyopita katika Uhispania, mradi ulikuwa ni kupata angalau kigari kidogo cha [Fiat] kiitwacho Seat chenye silinda zenye uwezo wa sentimeta za kyubiki 600. Sasa Wahispania hutamani kupata BMW ya Ujerumani!” Jagdish Patel, mkazi katika Unites States, alieleza kuhusu safari yake ya hivi karibuni katika India alikozaliwa: “Nilistaajabishwa na hesabu ya magari yaliyomo sasa katika barabara za India. Kwenye njia kuu bado waweza kuona magari aina ya Hindustan, lakini sasa kuna magari ya ki-siku-hizi, skuta, na pikipiki zilizoundiwa India kwa leseni kutoka makampuni ya nchi za kigeni.”

Mabadiliko Katika Sayansi

Miaka 25 tu iliyopita, wengi bado waliuona mwezi kuwa fumbo lenye kutatanisha. Tangu wakati huo, mwanadamu ametembea na kuacha vyombo vya kisayansi kwenye eneo hilo geni la mwezi na kurudi na sampuli za miamba ili zichunguzwe. Safari za vyombo vya angani vya Amerika ni jambo la kawaida sasa, na wanasayansi wa U.S. wanasema juu ya kuanzisha stesheni ya angani ya kudumu na juu ya kwenda Mihiri (Mars).

Ni nani aliyekuwa amesikia juu ya UKIMWI miaka 15 iliyopita? Sasa huo ni tauni ya ulimwenguni pote, na mamilioni huishi wakiuogopa.

Mabadiliko ya Kisiasa

Miaka minne tu iliyopita, ukuta ulioonekana kana kwamba hauwezi kupenyeka uligawanya jiji la Berlin; kulikuwa na Muungano wa Sovieti wa Ukomunisti na Vita Baridi. Sasa Berlin limechaguliwa kuwa jiji kuu la Ujerumani iliyounganika, na jamhuri 11 kati ya zile 15 zilizokuwa za Muungano wa Sovieti zimefanyiza Jumuiya ya Mataifa Huru.

Miaka michache tu iliyopita, Umoja wa Mataifa ulikuwa hasa uwanja wa mng’ang’ano kati ya nchi za ubepari na za Ukomunisti, huku nchi ziitwazo eti zisizofungamana na upande wowote zikiepuka kuhusika na kuwa kama watazamaji. Sasa mataifa ya Mashariki na Magharibi yanasema kuhusu amani na usalama, na Umoja wa Mataifa una uwezo mwingi zaidi. Unaweza kutuma majeshi kwenye sehemu za vita kotekote ulimwenguni. Miaka mitatu iliyopita, kulikuwa nchi zilizoitwa Yugoslavia na Chekoslovakia. Sasa zote mbili zimegawanyika kuwa Majimbo madogo yaliyo huru.

Kukiwa na mabadiliko hayo yote, je! ulimwengu umesonga mbele sana kuelekea amani ya kweli, haki, na ugawanyaji wa chakula na nyenzo bila upendeleo? Je! ulimwengu umestaarabika zaidi? Je! unaweza kutembea barabarani bila kuogopa wahalifu? Je! tumeelimishwa hivi kwamba hatuwachukii wengine tena kwa msingi wa rangi, dini, siasa, mtindo-maisha, au lugha yao? Je! mabadiliko yanaongoza kwenye maendeleo halisi kwa familia ya kibinadamu kwa ujumla na kwa makao yetu, dunia? Sisi tunaelekezwa wapi? Makala zifuatazo zitachunguza maswali hayo na mengineyo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki