Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 7/22 uku. 31
  • Fira Katika Sri Lanka Wanaosikia Sauti

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Fira Katika Sri Lanka Wanaosikia Sauti
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Ungependa Kukutana na Fira?
    Amkeni!—1996
  • “Sikio” la Fira
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Uwongo wa Kawaida Kuhusu Nyoka
    Amkeni!—1998
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
Amkeni!—1993
g93 7/22 uku. 31

Fira Katika Sri Lanka Wanaosikia Sauti

“Mfano wao ni fira kiziwi azibaye sikio lake. Asiyeisikiliza sauti ya waganga.”—Zaburi 58:4, 5.

Katika The New York Times, la Januari 10, 1954, chini ya kichwa “Je! Nyoka ‘Hugangwa’ na Muziki?” ripoti ifuatayo juu ya Zaburi 58:4, 5 yapatikana: “Dakt. David I. Macht, mtafiti wa madawa wa Hospitali ya Mount Sinai katika Baltimore [U.S.A], ni mmojapo wenye ujuzi zaidi wa sumu ya nyoka fira. (Mathalani, sumu ya fira ni tiba inayokubalika, katika matatizo ya damu.) Dakt. Macht aliripoti kwamba kwa kufanya kazi na fira na sumu ya fira alikuja kufahamiana na baadhi ya matabibu Wahindu, wenye elimu ya juu, na kutoka sehemu tofauti-tofauti za India. Wote walikubali kuwa fira husikia sauti fulani za muziki kutoka kwa zomari au filimbi. Aina fulani za muziki husisimua wanyama hao kuliko aina nyingine, wakaripoti matabibu hao. Watoto wa India wachezao gizani sehemu ya mashambani, huonywa wasiimbe ili sauti zao zisije zikavutia fira, akasema. Dakt. Macht alisema kwamba Shakespeare, ambaye kwa kurudiarudia alirejezea nyoka kuwa viziwi . . . alirudia tu kutoelewa kwa kawaida kwa wakati huo. Kwa upande ule mwingine Dakt. Macht alisema, mtunga Zaburi alikuwa sahihi aliyedokeza kwa utofauti, katika Zaburi 58, Mstari 5, kwamba nyoka wanaweza kusikia.”

Vivyo hivyo, katika makala iliyochapishwa Ujerumani kwenye gazeti la wanyama Grzimeks Tier, Sielmanns Tierwelt (Mnyama wa Grzimek, Ulimwengu wa Wanyama wa Sielmann), la Julai 1981 kurasa 34 na 35, mwandikaji anasema juu ya fira aliyekuwa akiishi kwenye kilima cha mchwa kwenye eneo lake katika Sri Lanka. Aliuliza mganga wa nyoka ashike nyoka wa porini na aifanye icheze. Mwandikaji huyo aliripoti: “Baada ya kumhakikishia mgeni wangu kwamba kweli kulikuwa na fira aliyeishi pale, aliketi mbele ya kilima cha mchwa na akaanza kupiga zomari yake. Baada ya muda mrefu—sikuamini tena kwamba chochote kingetendeka—fira aliinua kichwa chake sentimeta kadhaa kutoka shimoni. Kabla ya nyoka kufungua mdomo wake mganga huyo aliharakisha na kushika kichwa chake katika kidole-gumba chake na vidole vyake viwili.” Mhindi huyo hatimaye kwa kweli alimfanya nyoka acheze.

Kwa hiyo, kuna ushuhuda kwamba fira “husikiliza sauti ya waganga.”—New World Translation of the Holy Scriptures—With References, nyongeza 7A, ukurasa 1583.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki