Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w83 2/1 uku. 23
  • “Sikio” la Fira

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Sikio” la Fira
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Habari Zinazolingana
  • Fira Katika Sri Lanka Wanaosikia Sauti
    Amkeni!—1993
  • Je, Ungependa Kukutana na Fira?
    Amkeni!—1996
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
  • Uwongo wa Kawaida Kuhusu Nyoka
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
w83 2/1 uku. 23

“Sikio” la Fira

Kifungu cha Biblia kinachotaja kwa njia ya mashairi “sikio” la fira (nyoka mkubwa) kimepingwa mara nyingi. (Zaburi 58:4, 5) Lakini gazeti la Kijeremani la sayansi ya maumbo ya wanyama linaloitwa Grzimeks Tier, Sielmanns Tierwelt (yaani, Ulimwengu wa Wanyama wa Grzimek na wa Sielmann) limechapisha makala ambayo linakiri ‘inapingana kabisa’ na maoni ‘ya kwamba fira ni bubu,’ kisha linaendelea kuuliza hivi: “Ni nani anayesema kweli​—yale maoni yanayofuatwa kisayansi au mwandikaji wetu?”

Mwandikaji anaeleza habari za fira aliyeishi katika uwanja wake katika Sri Lanka akiwa katika kichuguu cha mchwa. Alimwomba mtumbuiza-nyoka amkamate nyoka huyo asiye wa kufugwa kisha amfanye acheze dansi. Mwandikaji anasema hivi: “Nilipokwisha kumhakikishia mgeni wangu huyo kwamba kwa kweli fira aliishi hapo, yeye aliketi mbele ya kichuguu hicho cha mchwa akaanza kupiga filimbi yake. Baada ya muda mrefu​—kwa sababu nilikuwa nimechoka na sikuamini lo lote litatukia​—fira yule alitokeza kichwa chake sentimeta kadha nje ya shimo moja. Kabla nyoka huyo hajaweza kufungua kinywa chake mtumbuizaji alienda haraka akamshika kichwa kati ya kidole gumba na vidole vingine viwili.” Halafu Mhindi huyo akamfanya nyoka yule acheze dansi. Angalau katika kisa hicho fira kwa kweli ‘aliisikiliza sauti ya mtumbuizaji.’

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki