UKIMWI na Watu Mashuhuri
WATU ambao husoma orodha ya watu waliokufa mara nyingi hushangazwa na idadi ya watu mashuhuri ambao hufa kutokana na UKIMWI. Gazeti Newsweek la Januari 18, 1993, lilithibitisha kwamba watu wengi kama hao wanakufa, likisema hivi: “Katika kila tawi la utamaduni—kucheza dansi, jumba la michezo, fasihi, muziki, upambaji, mitindo ya mavazi, sanaa, televisheni, sinema—uharibifu kutokana na UKIMWI waendelea.”
Newsweek lilitaja hivi pia: “Paris inafanana sana na New York au Los Angeles: uchunguzi mmoja ulionyesha kwamba zaidi ya asilimia 60 ya vifo vya wakazi wanaume wa Paris wenye umri wa kati ya miaka 25 na 44 wanaofanya kazi za uandikaji wa habari, usanii, na kutumbuiza vilisababishwa na UKIMWI.”
Gazeti People la Januari 23, 1993, katika makala yalo “Hofu Katika Barafu” lilieleza juu ya uharibifu mkubwa ambao UKIMWI umefanya katika mchezo wa kulipwa wa kuteleza juu ya barafu. Lilisema hivi: “Mchezo wao ukiwa umeharibiwa kabisa na vifo zaidi ya 40, wachezaji mashuhuri wa kuteleza juu ya barafu wa Amerika Kaskazini wana huzuni nyingi juu ya kupoteza rafiki zao na idadi yenye kuhuzunisha ya wanaouawa na UKIMWI.”
John Curry, Mwingereza aliyepata nishani ya dhahabu katika Olympiki, alitambuliwa katika gazeti hilo kuwa “mchezaji wa kuteleza juu ya barafu mashuhuri zaidi aliye na UKIMWI.” Yeye alinukuliwa akisema hivi: “Rafiki zangu wote wa karibu walikufa kwa UKIMWI.” Ni kwa nini wachezaji wengi wa kuteleza juu ya barafu wamepatwa na UKIMWI?
Sababu ni mtindo wao wa maisha. Gazeti People lilifunua jambo hilo liliposema hivi: “Watelezeaji juu ya barafu, makocha na maofisa wanapoendelea kuomboleza kwa ufaragha juu ya vifo vya rafiki zao, wao waendelea kubaki katika hali ya kuvurugika akili na wenye hofu juu ya kushughulikia UKIMWI hadharani na lile suala la ugoni wa jinsia-moja katika [mchezo wa] kuteleza juu ya barafu.”
Kwa kweli, ngono ya ovyo-ovyo—zote mbili ya jinsia-moja na ya jinsia-tofauti—ndicho kisababishi kikuu cha UKIMWI. Katika Desemba 1991, madaktari wawili katika Kanada walifunua kwamba mwanamke mmoja aliyekuwa amekufa kwa UKIMWI alitaja majina ya wachezaji wa Ligi Kuu ya Magongo wanaofikia 70 ambao alikuwa amefanya ngono nao. “Tukio hilo limesababisha wasiwasi mwingi kwa baadhi ya timu za [Ligi Kuu ya Magongo],” likaripoti The New York Times la Desemba 5, 1991. “Jambo hilo lilionekana katika vikundi vyenye huzuni vya wachezaji na makocha waliokusanyika ili kujadili suala hilo wakati wa mazoezi leo.”
Ni jambo gani lipaswalo kufanywa? “Ujumbe tunaopaswa kupelekea watoto si ngono salama, bali wapasa uwe hifadhi ngono,” akasema mmoja wa wachezaji wa mpira wa magongo wa timu ya Montreal Canadiens. “Usifanye ngono mpaka ufunge ndoa.” Hilo si shauri jipya, kwa sababu Biblia yahimiza hivi: “Ukimbieni uasherati.”—1 Wakorintho 6:18, NW.
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]
Kuitazama Michezo