Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 6/8 kur. 23-27
  • Je! Wewe Huumwa na Mgongo?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Wewe Huumwa na Mgongo?
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mzunguko wa Maumivu
  • Sababu Inayofanya Mgongo Uume
  • Unaloweza Kufanya Ili Utulize Maumivu
  • Kutafuta Tiba
  • Maumivu Ambayo Hayatakuwapo Tena
    Amkeni!—1994
  • Ni Nani Anayehitaji Maumivu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Maendeleo Katika Kutibu Maumivu
    Amkeni!—1994
  • Jitihada Yangu ya Kukabiliana na RSD
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 6/8 kur. 23-27

Je! Wewe Huumwa na Mgongo?

“Maumivu hayo yalikuwa makali sana. Nilihisi kana kwamba mtu fulani alikuwa na kiberiti naye akawasha moto mgongoni mwangu! Ninachokumbuka tu ni kwamba nilikuwa nikiinama ili nimsogeze mwana wa dada yangu mbali na bilauri iliyovunjika, na ghafula nikahisi kana kwamba mgongo wangu wote umewashwa moto. Nilibaki kwenye kikao hicho kwa siku kadhaa, nikishindwa kujinyorosha. Sikuwahi kupata maumivu kama hayo awali,” asimulia Karen, umri wa miaka 32, mke-nyumbani na mama wa watoto wawili.[1]

NI MAUMIVU ya kichwa tu ndiyo yapitayo maumivu ya mgongo katika idadi ya watu wanaoathiriwa nayo Marekani.[2] Ni kisababishi kinachoongoza cha kasoro ya muda mrefu kwa watu wenye umri unaopungua miaka 45 na cha tatu miongoni mwa watu wenye umri uzidio 45.[3] Wenye kuumwa hutumia zaidi ya dola bilioni 24 kwa mwaka wakitafuta kitulizo—mara nne ya zile zilizotumiwa kwa matibabu ya UKIMWI katika 1991.[4]

Kulingana na Dakt. Alf L. Nachemson, mtafiti wa kisayansi kwa matatizo ya mgongo, wagonjwa bilioni 2 ulimwenguni pote wameteseka kwa kuumwa na mgongo kwa mwongo uliopita. “Wakati mwingine kipindi cha maisha yetu yenye utendaji asilimia 80 kati yetu tutapatwa na maumivu ya mgongo kwa kadiri fulani,” yeye alisema.[5]

Mzunguko wa Maumivu

Maumivu ya mgongo hayachagui. Wafanyakazi wa viwandani na wa ofisini pia waelekea kupatwa na maumivu ya mgongo. Wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee, waweza kupatwa na maumivu haya. Maumivu hayo yanaporudirudi na kufuliza, yanaweza kuathiri kazi, mapato, familia, na daraka la mtu katika familia, yakileta maumivu ya ki-hisiamoyo vilevile. Jinsi gani?

Watu hujipata wakiwa kwenye mzunguko wa maumivu, chaandika kitabu The Fight Against Pain. Maumivu ya kimwili husababisha hangaiko na mshuko wa moyo ambao huenda nao ukaongoza kwenye maumivu mengi hata zaidi na yenye kuendelea.[7] Kwa mfano, mzazi mmoja mchanga au mwenye kuandaa riziki huenda akapaswa kushughulika na mbano kazini, na familia, na marafiki kwa sababu ya kasoro ambayo yaweza kutokana na matatizo ya mgongo.

“Niliona kwamba tatizo kubwa zaidi ni ukosefu wa kuelewa na huruma kwa upande wa familia na marafiki. Watu huelekea kupunguza kadiri ya maumivu, wakikosa kuelewa jinsi unavyoumia hasa,” akasema Pat, mwenye umri wa miaka 35, sekretari aliyepata mojapo matatizo yake ya mgongo kwa mara ya kwanza katika 1986. “Kwa kuwa hujui ni lini au wapi maumivu yatakapokuja kwa ghafula, unaelekea kutofanya mipango mingi. Unaweza kuonekana ukiwa usiyependa ushirika, kutokubali ukaribishaji, kutomshika mtoto aliyezaliwa wa mtu fulani, kutotabasamu, yote hayo kwa sababu unaumwa. Ukiyaruhusu maumivu yako, yanaweza kukudhibiti.”[8]

Sababu Inayofanya Mgongo Uume

Je! maumivu ya mgongo ni yasiyoepukika? Waweza kufanyaje ili uyatulize au uyazuie? Ni wakati gani unapaswa kutafuta msaada wa kitiba kwa ajili ya mgongo wako? Ijapokuwa maumivu ya mgongo yanayoendelea yanaweza kutokeza dalili ya magonjwa mengi ya ndani, mazungumzo haya yatakazia vyanzo viwili vya maumivu ya mgongo—mkazo wa mifupa ya uti wa mgongo na mpindano wa misuli.[9]

Mifupa ya uti wa mgongo yenye kupenyeza ni visababishi vikubwa vya ugonjwa wa mgongo miongoni mwa vijana na watu wazima wa makamo. Wakati mtu anapofikia umri wa miaka yake ya 20, sehemu ya ndani ya yavuyavu ya uti wa mgongo huanza kupoteza mnyumbuko wake na umajimaji wayo, ikisababisha mifupa ya uti wa mgongo ijikunyate. Lakini jambo hilo halisababishi maumivu. Hata hivyo, kwa watu fulani, maumivu hutokea wakati sehemu ya ndani ya yavuyavu inapopenyeza, au inapobenuka, kupitia mviringo wa nje wa mnofu wa nyuzinyuzi.[11]

Gazeti Fortune laeleza kuhusu mifupa hii ya uti wa mgongo: “Inapodhoofika kufikia kiwango fulani, mkazo mdogo zaidi—jambo duni kama kupiga chafya au kuinama ili kusogeza chombo cha muziki—laweza kuwa kisababishi cha maumivu.”[12]

Mifupa ya uti wa mgongo hutumika ikiwa vimeza mishtuko kati ya mifupa 24 ya uti wa mgongo. Mifupa hii imejipanga mmoja juu ya mwingine na kuunda shimo la wimawima, njia ya uti wa mgongo, ambao kupitia kwayo uti wa mgongo washikiliwa. Kati ya kila mifupa miwili-miwili ya mgongo, kuna nafasi ambayo kupitia kwayo bumba la neva, liitwayo neva kuu, huacha njia, bumba moja katika pande yoyote ile.[13] Mifupa ya uti wa mgongo yaweza kupenyeza na kujisukuma dhidi ya neva hususa. Mkazo huu huu waweza kuhitilafiana na ishara za neva ambazo hutoa hisi kuelekea na kutoka sehemu nyinginezo za mwili.[14]

Hali ya maumivu makali mno yajulikanayo kuwa siatika (ugonjwa wa mshipa wa nyuma ya paja), kwa mfano, waweza kutokea ikiwa kuna mkazo unaoingizwa kwenye mizizi ya neva ya siatika. Baadhi yazo zikiibuka kutoka sehemu ya chini ya uti wa mgongo hufanyiza neva ya siatika. Kuna moja katika kila upande, ikipita chini ya nyuma ya kila paja hadi kwenye goti na kisha kukata njia kuelekea neva nyinginezo. Maumivu ya siatika kwa kawaida huanza chini ya mgongo na kuelekea kwenye nyonga na matako na chini ya nyuma ya paja, wakati mwingine hata kwenye shavu la mguu na wayo.[15] Kama tokeo, mtu aweza kupatwa na kulegea kwa wayo—hali ambayo wayo hujikokota kwa sababu misuli ya mguu haiwezi kuinua vidole vya mguu. Mwenye kuumia pia huenda akapatwa na hisi ya pini na sindano, ganzi, na udhaifu wa misuli katika mguu ulioathiriwa.[17]

Mifupa ya uti wa mgongo ikijisukuma kwenye mizizi ya neva katika cauda equina, kikundi cha neva kilicho chini tu ya kiuno ambacho hutumikia kibofu na matumbo, mtu huenda akawa na matatizo ya kukojoa au kwenda choo. Watu walio na matatizo hayo wapaswa kumwona daktari mara moja, kwa kuwa zaweza kuwa dalili kubwa za matatizo ya mishipa.[18]

Inapokunjamana na kulegea, misuli hiyo iliyo nyuma hujiunga na mishipa katika kutegemeza wajibu, kuona kwamba uti wa mgongo hauanguki na kuuwezesha uiname na kupindika. Ikiwa chini ya mkazo, hata hivyo, misuli isiyokuwa sawasawa kimwili yaweza kwenda kwenye mpindano wa mishipa, ikikaza sana hivi kwamba yawa bonge gumu. Ikitokea bila onyo na ikimfanya mtu asisonge kwa muda, mfululizo wa mpindiko wa mishipa ya mgongo waweza kuwa wenye uchungu sana.[19] Mtu mmoja mwenye kuumizwa asimulia maumivu hayo kuwa kama “mfululizo wa matetemeko ya ardhi yakilipuka mgongoni mwako.”[20]

Madaktari wanakubali kwamba mpindiko wa mishipa hutokea ili kulinda mtu asilete uharibifu zaidi kwa misuli dhaifu. Kitabu cha kampuni ya Time-Life, The Fit Back, chasema hivi: “Kwa kufanya mgongo usisonge, mpindiko wa mishipa hukulazimisha uchukue msimamo unaofaa wa kutenda na kulala. Kikao hicho hakiweki kiwango kidogo cha mkazo kwenye mgongo wako tu, bali pia huruhusu mnofu uliochochewa ujirekebishe upya wenyewe.”[1]

Ili kuzuia maumivu ya mgongo ambayo kwa kawaida huanzisha mpindiko wa mishipa, misuli ya mgongo, tumbo, na mapaja yahitaji kubaki yakiwa yametulizwa na imara. Kwa mfano, misuli ya tumbo, huenda ikatokeza mkazo wa mgongo kwa sababu haipeani tegemezo lifaalo nayo haiwezi kukinza uvutano wa uzito wa mwili kwenye uti wa mgongo.[22] Ikiwa misuli ya tumbo ipo katika hali nzuri, hiyo hufanyiza “mshipi wa msuli” ambao huzuia mgongo wa chini kutokana na kikao cha kupepesuka. Kikao cha kupepesuka, kujikunja kupita kiasi kwa mgongo wa chini, huvuta mifupa ya uti wa mgongo ya mgongo wa chini kutoka kwenye usawaziko.[23]

Unaloweza Kufanya Ili Utulize Maumivu

Kikao kibaya, unene kupita kiasi, misuli dhaifu, na mkazo ni mambo manne yawezayo kuchangia maumivu ya mgongo wa chini. Utendaji wa kawaida unaofanywa vibaya, kama vile kuketi, kusimama au kuinua, ni mambo mengine yenye kuyaletea.[24]

Kuna uhusiano kati ya kikao kizuri na misuli ya tumbo na ya mgongo yenye nguvu. Kikao kizuri huruhusu misuli ifanye kazi vizuri, ilhali misuli mizuri ni muhimu kwa ajili ya kikao kizuri. Usawaziko ufuatao upindo S wa asili wa uti wa mgongo unahitajiwa kwa kikao kizuri. Hakimaanishi uti wa mgongo ulionyooka kabisa.[25]

Kikao kibaya kikirekebishwa, maumivu ya kikao cha kwanza yaweza kuondolewa, aandika Robin McKenzie katika kitabu Treat Your Own Back, akiongezea hivi: “Hata hivyo, wakati unapopita, ikiwa hakijasahihishwa, kikao kibaya cha mazoea husababisha mabadiliko kwa muundo wa viungo, kuchakaa sana, na kuzeeka kwa viungo mapema yakiwa ndiyo matokeo.”[26]

Uzani wa kupita kiasi, hasa katika tumbo, waweza kukaza mgongo kwa sababu unafanyiza uvutano kwenye misuli ambayo huegemeza mgongo. Programu ya mazoezi ya kawaida ndio ufunguo wa mgongo ulio sawa na wenye afya. Hata kama maumivu hayapo tena, mazoezi ni muhimu kwa sababu maumivu ya mgongo yaliyotoweka huelekea kurudi bila kutazamiwa.[27] Uchunguzi kamili wa kitiba unapendekezwa kabla ya kuanza programu ya mazoezi. Daktari aweza kupendekeza mazoezi yafaayo kwa tatizo la mgongo la mtu mmoja-mmoja.[28]

Watafiti wengi huamini kwamba mkazo waweza kumfanya mtu ashindwe na tatizo la mgongo. Mkazo waweza kupiga mishipa iliyopindika kwa watu fulani kwa sababu mkazo usiotulizwa hukaza misuli, ikisababisha maumivu ya mgongo. Kuwezana au kuondoa vyanzo vya mkazo kwaweza kupunguza hatari ya maumivu ya mgongo.[29]

Watu ambao hutumia wakati mwingi wakikaa kazini au wakisafiri kwa mwendo mrefu huenda wakapatwa na maumivu ya mgongo. Uzito mwingi huelekezwa chini ya mgongo wanapoketi, kulingana na uchunguzi uliofanyiwa Sweden.[30] Kwa kusikitisha, hatari hii imeongezeka kwa utumizi wa viti vya ofisi vilivyo na egemezo la mgongo lisilofaa sana. Huenda ikasaidia kukatiza kuketi kwa kusimama na kutembea kidogo kwa dakika chache kwa ukawaida.[31]

Watu wanapoinua vitu vizito au hata vyepesi, wanapaswa kulinda dhidi ya kutumia misuli yao ya mgongo. Kupiga magoti kwapendekezwa unapoinua kitu ili misuli ya mgongo isiwe na mkazo wote.

Mtu anayefanya kazi kwa kikao kisichofaa pia ataelekea kupata matatizo ya mgongo. Wafanyakazi wa viwanda, wauguzi wa kike, wanaumeme, watunza-nyumba, na wakulima wote wahitajika kuinama kwa muda mrefu wakifanya kazi yao. Ili kupunguza hatari ya kuumizwa mgongo, wastadi wa mwili wanapendekeza kupumzika kwa ukawaida au kubadilisha vikao. Watu wanaosimama kwa muda mrefu wanashauriwa watumie kibago kidogo au kipumzishaji kinginecho nao wapandishe wayo mmoja ili kunyoosha mgongo.[32]

Kutafuta Tiba

Kwa wengi ambao hupatwa na maumivu ya mgongo yanayosababishwa na misuli, madaktari hupendekeza tiba ya kawaida—kupumzika, kutumia joto, kukandakanda, mazoezi, na mbeleni, dawa za kutuliza maumivu. Kuhusu dawa hizo, Dakt. Mark Brown wa Chuo Kikuu cha Shule ya Madawa cha Miami atoa onyo. Yeye aona kwamba katika Marekani, matumizi marefu ya dawa hizo ndio kisababishi kikubwa cha maumivu ya mgongo, yaani, matokeo ya baadaye ya madawa. Watu wapaswa kujihadhari dhidi ya kutumia dawa kwa muda mrefu, kunakoweza kusababisha vibonge vyenye kuongezeka, vikiwa na uwezekano wa kusababisha uzoelevu.[34]

Kuwaona madaktari wa mwili na mishipa kwaweza pia kuwasaidia wanaoumia. Utibabu wa mishipa huwa na karibu theluthi mbili hivi za ziara zote za wagonjwa wa mgongo Marekani, laandika jarida HealthFacts.[35]

Upasuaji huenda ukawa wa lazima ili kurekebisha matatizo au kutuliza maumivu yanayohusiana na mifupa ya uti wa mgongo iliyochomoza. Hata hivyo, mara nyingi zaidi, madaktari watapendekeza tiba ya kutuliza kwa watu wengi wenye kuumizwa na maumivu ya mgongo. Watu wanaoambiwa kwamba wanahitaji upasuaji watafanya vema kupata maoni ya daktari wa pili au wa tatu.[38]

Kwa mamilioni ya waumiaji, maumivu ya daima lakini yanayoweza kuvumilika ni sehemu ya maisha. Wengi hushindwa na maumivu lakini wanajitahidi kutokatizwa na shughuli za siku kwa siku. Wanajua mambo yanayoleta maumivu nao huchukua hatua ili kuzuia au kuwezana nayo. Wao hufanya mazoezi kwa ukawaida, husitawisha uzani unaofaa, hushughulikia kikao chao, na hupunguza mikazo katika maisha zao. Kujapokuwa kurudi mara kwa mara kwa maumivu ya mifupa iliyochomoza ya uti wa mgongo na kupindika kwa mishipa, Karen, aliyetajwa mwanzoni, hushikilia kwa shangwe ratiba iliyojaa shughuli, akitumia wakati mwingi katika utendaji wa kuhubiri wa Mashahidi wa Yehova. Kama vile Karen, wagonjwa wengi huwa na mwelekeo chanya na hushughulikia kudhibiti maumivu yao ya mgongo.

[Sanduku katika ukurasa wa 24]

Misaada Fulani ya Kuzuia Maumivu ya Mgongo

☞ Epuka kuinua kitu haraka, kwa ghafula. Badala ya kuinama kuanzia kiuno, inama kwa magoti.[1]

☞ Omba msaada unapoinua vitu vizito.[2]

☞ Unapobeba mizigo fulani, sawazisha mzigo kila upande. Unapobeba mzigo mmoja mzito, beba kwa mikono yote miwili ikiwa mbele, mbele ya mwili. Ikiwa unabeba upandeupande, badili upande.[3]

☞ Kwa ajili ya kusafiri, tumia kibebaji cha mizigo kinachojikunja vyepesi/au mzigo mwepesi wenye kanda za kubebea.[4]

☞ Unapotoa vifurushi kutoka kwenye buti la gari, weka vifurushi karibu na mwili kabla ya kuviinua.[5]

☞ Unapofagia, tumia ufagio wenye kishikio kirefu. Badala ya kuinama kuanzia kiunoni ili kufagia vitu vilivyo mvunguni, piga goti moja ukitumia vitambaa vya magoti. Ikiwa ni lazima uiname kuanzia kiunoni, kisha, inapowezekana tumia mkono mmoja kujitegemeza kwenye kitu fulani.

☞ Unapofanya kazi ya ofisi, badili kuketi kwenye dawati kwa kunyooka kuanzia kiuno.[7]

☞ Piga magoti unapofanya kazi ya bustani, na ugawanye kazi katika sehemu fupifupi. Unaposimama usiiname kuanzia kiunoni.[8]

☞ Fanya mazoezi ya mgongo kwa ukawaida hata kama ni kwa dakika 10 hadi 15 tu kwa siku. Fanya mazoezi ya kiasi ikiwa wewe ni mzee.[9]

☞ Unapotandika vitanda, piga goti moja kwenye kitanda, na utandike kwa mkono mmoja ukiegemeza mwili na ule mwingine. Unaponyoosha au kuingiza shuka, piga magoti sakafuni katika kila upande wa kitanda.[10]

☞ Unapoendesha gari mwendo mrefu, tua ili upumzike. Ikiwa nyuma ya kiti cha gari haistareheshi, tumia mto ujazie nafasi mahali ambapo kiti hakitoshei vizuri nyuma.[11]

☞ Usifanye mazoezi ya kukimbia juu ya mahali pagumu. Vaa viatu vifaavyo vya kufanyia mazoezi.[12]

☞ Tumia mto au kitu chochote cha kuegemea nyuma unapokalia kiti cha starehe au sofa. Inuka polepole, ukitumia miguu yako kuinuka.[13]

☞ Ikiwa unatumia saa nyingi kuketi kazini, tumia kiti ambacho kina tegemezo la mgongo lifaalo. Simama mara nyingine, na uzunguke-zunguke.[14]

☞ Usiiname kwenye droo za kabati kwa kipindi chochote kirefu, bali kaa kwenye kiti unapofanya kazi ya faili unapoweza.[15]

☞ Ikiwa ni lazima uvae viatu vyenye visigino virefu wakati wa siku, leta viatu vya kustarehesha ili kuvibadili inapowezekana.[16]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki