Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 1/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “Ngono Salama”—Si Salama kwa Wanawake
  • Zoezi la Ubongo
  • Ujumbe wa Kunjo la Karatasi-Choo la Gari-Moshi
  • Tanakuzi ya Bunduki Marekani
  • Udaku Japani
  • UKIMWI Wafyeka Afrika
  • Kuvua Mno Kwazichosha Bahari
  • Mazoea Bora ya Kulala
  • Misa ya Katoliki Yatumikiwa na Wasichana wa Altare
  • Kidhehebu cha Matowashi
  • Naweza Kuepukaje Kupata UKIMWI?
    Amkeni!—1993
  • UKIMWI—Je! Nimo Hatarini?
    Amkeni!—1993
  • Kusaidia Wale Walio na UKIMWI
    Amkeni!—1994
  • UKIMWI— Shida kwa Matineja
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 1/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

“Ngono Salama”—Si Salama kwa Wanawake

Kujapokuwa kutangazwa kwingi kwenye kupendelea “ngono salama” na matumizi ya mipira ili kuepuka kuambukizwa UKIMWI, madaktari wanaanza kushuku ile hekima ya ushauri kama huo. Ripoti fulani ya kitiba iliyotokea katika gazeti la Paris Le Figaro yasema kwamba ingawa mipira hutoa kiasi fulani cha ulinzi kwa wanaume dhidi ya UKIMWI, hiyo hutoa ulinzi haba zaidi kwa wanawake kwani mwenzi aliyeambukizwa kwa urahisi aweza kuambukiza upande wa nje wa mpira. Wanawake wako pia katika hatari ya kuambukizwa wakati wa hedhi na wawapo na ambukizo lolote la uke au kidonda. Kitakwimu, sasa mipira yaonekana kuwa na matokeo ya chini ya asilimia 69 katika kulinda wanawake dhidi ya UKIMWI. Akieleza juu ya upungufu huu wa kitendeshi “salama,” daktari mmoja alionelea hivi: “Tungesemaje kuhusu eropleni ambayo ina uwezekano wa asilimia 69 tu wa kutoanguka kwa mwaka?”

Zoezi la Ubongo

“Kumbukumbu mbaya kwa kawaida si suala la ajali bali mazoezi mabaya,” charipoti DAK Magazin, kichapo cha bima ya afya cha Kijerumani. Kama vile misuli hunyong’onyea kwa kutotenda, ndivyo ubongo huchakaa na huhifadhi data kidogo zaidi ikiwa hupata mazoezi haba. Je, hili ni tatizo hasa kwa wazee-wazee? La hasha! “Kwa sababu kwa kawaida, kufikiri hufanywa kuwe rahisi kwetu au hata kupita kiasi,” gazeti hilo laeleza, hata vijana waweza kupatwa na hatari ya kuwa na kumbukumbu lililochakaa kwa kutotendesha akili zao ifaavyo. Ni nini kinachoweza kusaidia? Gazeti hilo ladokeza kufanyiza ubongo mazoezi, kwa kutumia michezo ya kiakili, kama vile mafumbo yanayotia ndani nambari na herufi za alfabeti, ili kuhamasisha akili na kumbukumbu. Pia, “fumbo la kujaza maneno laweza kusaidia.”

Ujumbe wa Kunjo la Karatasi-Choo la Gari-Moshi

Hadi kifaa cha kisasa kianzishwe, njia ya pekee ambayo kiongozi wa gari-moshi awezayo kuwajulisha wenye mamlaka dharura yoyote ile kwenye karibu kila gari-moshi ya Italia itaendelea kuwa kama ifuatavyo: Andika kijibarua, kiweke ndani ya kunjo la karatasi-choo, na ulitupe kutoka kwa gari-moshi inayoenda kasi kwenye kituo kinachofuata, kwa kutumaini kwamba litapatikana na wenye mamlaka wajulishwe. Mfumo huu, “wa kale kama reli zenyewe,” unapendekezwa na kanuni rasmi za reli. ‘Bado ni mbinu yenye matokeo, iliyojaribiwa na kuthibitishwa,’ asema ofisa wa Reli za Serikali ya Italia, ambaye hata hivyo anatambua kwamba “uwasiliani kwenye gari-moshi ni tatizo zito mno.” Wanapokabiliwa na ugonjwa wa abiria, mzigo unaoshukiwa kuwa hatari, tendo la ujeuri, au wizi, “waajiri wa Reli za Serikali hawana uwezo katika hilo,” lasema gazeti la Kiitalia Corriere della Sera, kwa sababu hawana mamlaka ya kuingilia. Ili kusuluhisha tatizo la uwasiliani, Reli za Serikali ya Italia zakusudia kuhodhi simu zenye kubebeka za masafa machache kwa wakati ujao wa karibuni.

Tanakuzi ya Bunduki Marekani

Ongezeko la idadi ya mauaji ya kimakusudi kwa bunduki-mkono katika Marekani, likiambatana na furiko la mifyatuo mingi, limetokeza wale wafikirio ni wakati wa kuzinyakua kutoka kwa wahalifu na pia wale wahisio ni wakati wa kununua bunduki wao wenyewe. “Kwa hakika, watu wengi huenda wakawa wanayafikiria yote mawili kwa pamoja,” lasema gazeti la Time. Na kujapokuwa na misongo iliyoongezeka ili kudhibiti bunduki, watu wengi wazinunua kuliko wakati uliopita. Wakati sheria ya Brady (sheria ya kudhibiti bunduki) ilipopitishwa, wauza bunduki waliripoti ongezeko la mauzo kabla haijaidhinishwa. Sasa kuna bunduki karibu milioni 211 katika Marekani. Katika jitihada za kupunguza kiasi hicho, programu zilianzishwa ambazo katika hizo watu wangeweza kurudisha bunduki na kupokea cheti cha zawadi cha dola 100—bila kuulizwa maswali. Kampeni hizo zilizoa mamia ya bunduki kutoka mitaani lakini pia ilichochea wengine kununua bunduki za bei rahisi ili kwamba wangeweza kuzirudisha na kufanya faida. Mwenye duka mmoja wa bunduki akasema hivi: “Naweza kuwahakikishia, wengi wa watu wazirudishao bunduki wakati wa asubuhi bado watakuwa na bunduki wakati wa alasiri.”

Udaku Japani

Ikiita udakuzi kuwa “kipitisha wakati cha kitaifa” cha Japani, Mainichi Daily News iliripoti kwamba “Japani ni mojapo ya mataifa yaliyo na vitega maongezi vingi zaidi ulimwenguni, ikiwa na maikrofoni ndogo sana za redio 60,000 zinazouzwa” kila mwaka. Vitega maongezi vingine ni vidogo hivi kwamba vyaweza kutoshea ndani ya kalamu za kuandikia. Kuna vidude ambavyo vyaweza kunasa mazungumzo meta 15 mbali na kuyapitisha mwendo wa kilometa tatu. Ni nani wadoeaji wa mazungumzo wa Japani? Kulingana na gazeti hilo, wadakuzi wengi wa mazungumzo wanatafuta “zile kasimawimbi ili kupata vidonge vitamu sana” vya porojo. Lakini wengi “ni wapenzi wenye wivu watakao uhakikishio wa shauku ya wenzi wao, au baba watakao kuangalia miendo ya binti zao.”

UKIMWI Wafyeka Afrika

Kulingana na makadirio yaliyofanywa na Shirika la Afya Ulimwenguni, ya vile visa vinavyojulikana ulimwenguni, zaidi ya milioni 15 vya UKIMWI, milioni karibu 10 viko Afrika, likiifanya kuwa ile kontinenti iliyoambukizwa vibaya sana. “Vigongo vidogo vya changarawe dhidi ya mito inayozidi kufurika,” ndivyo Profesa Nathan Clumek alivyofafanua hatua za sasa za kukumbana na kipuku cha UKIMWI. Katika mahoji yaliyoandikwa kwenye gazeti la kila siku la Paris Le Monde, Profesa Clumek alisema kwamba wakuu wa serikali za Afrika bado hawajang’amua kikamili ule uharibifu ambao virusi hiyo itasababisha katika Afrika. Katika 1987, wakati Profesa Clumek aliposema kwamba asilimia 10 ya kontinenti wangeambukizwa na UKIMWI, wengi walifikiri alitia chumvi. Leo yakadiriwa kwamba kila mahali kutoka asilimia 20 hadi 40 ya idadi ya watu wa Afrika itaambukizwa na virusi hiyo yenye kuua.

Kuvua Mno Kwazichosha Bahari

“‘Samaki baharini wako chekwa-chekwa,’ huambwa ule msemo. Lakini si kweli,” laandika The Economist. “Ule utele wa bahari umetanuliwa kupita mipaka yawo.” Tangu upeo wawo katika 1989, uvuvi wa samaki wa baharini umekuwa ukipungua. Sababu ni sahili hivi: “Ni samaki wachache mno wamesalia kwenye bahari kuweza kudumisha akiba za kuendelea kuanguliana. Wavuvi wamevuka mipaka, kwa kumeza rasilimali ambayo inapaswa kutokeza uvuo wao.” Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, 13 za zile sehemu kuu 17 za uvuvi wa samaki za ulimwengu ziko matatani—4 zikiwa zimepangwa kuwa zisizo na samaki kibiashara. Tekinolojia iliyo tata—kama vile sona na mawasiliano ya setelaiti—imefanya iwezekane kwa wavuvi kutambua samaki hata katika maeneo ya mbali na kurudi katika maeneo yaleyale hususa ya uvuvi. Nyavu kubwa zilizotengenezwa viwandani za kukokota chini-chini baharini zilizo saizi kama ya nyanja za mpira wa miguu, zenye nyavu hata kubwa zaidi, huvua kwa wingi kiasi cha samaki. Serikali ndizo za kulaumiwa kwa uharibifu huo, lasema The Economist, kwa sababu asilimia 90 ya uvuvi wa ulimwengu wapatikana mnamo kilometa 370 za baadhi ya fuo za nchi fulani, maji ambayo zayamiliki. Serikali huzuia mashua za mataifa mengine bali huruhusu mashua zazo zipanuke, na hata huwasaidia kifedha.

Mazoea Bora ya Kulala

“Kukosa usingizi huenda kukaonekana kwenye kuzaa matunda kwa watu wengi, lakini matokeo ya kunyima mwili saa za usingizi huishia kuwa bila matunda sana,” lasema gazeti la Brazili Exame. Mwananiuroni Rubens Reimão aeleza hivi: “Mwili hautasahau saa za kulala ambazo wamwia mtu. Kinyume, sikuzote utakumbuka na utadai kwa ghafula gharama iwezayo kutafsiriwa kwa kupotewa-potewa na kumbukumbu, matatizo ya ukolezi, na uwezo wa kufikiri wa polepole.” Ili kujiepusha na mahangaiko yasiyo ya lazima, Dakt. Reimão apendekeza hili: “Wacha usuluhishaji wa matatizo ya kazi au kuyafikiri kubakie kazini.” Ili upumzike na kulala vizuri zaidi, Exame ladokeza mazoezi ya kawaida, muziki mwororo, mwangaza uliopungua, na mawazo mazuri.

Misa ya Katoliki Yatumikiwa na Wasichana wa Altare

Matumizi ya wasichana ili kusaidia mapadri wakati wa msherehekeo wa Misa, mpaka sasa, umevumiliwa na baadhi ya mamlaka za kanisa. Katika barua iliyokubaliwa na Papa John Paul 2 na kupelekwa kwa wasimamizi wa makongamano ya maaskofu Wakatoliki kote ulimwenguni, Kutaniko la Ibada ya Kimungu na Kanuni ya Sakramenti limewapa maaskofu mmoja-mmoja uchaguo wa kuidhinisha wasichana wa altare ili kusaidia kutumikia Misa. Kulingana na Corriere della Sera, alipokuwa akitoa tangazo hilo na ili “kuondoa hata umulimuli ulio mdogo zaidi wa tumaini kwa matamanio ya kike,” msemaji wa Vatikani Joaquin Navarro Valls alionyesha waziwazi kwamba fursa hiyo kwa njia yoyote hairekebishi mwelekeo wa kanisa kuelekea mapadri wanawake. Basi, kwa nini wasichana wa altare? “Hainishangazi,” akasema mwanasosholojia Franco Ferrarotti. “Kanisa haliwezi kupata mapadri, na inaonekana kwamba wala haliwezi kupata wavulana wa altare.”

Kidhehebu cha Matowashi

Indian Express la Bombay laripoti kwamba katika India kuna zaidi ya matowashi milioni moja. Bila shaka, ni asilimia 2 tu ambao walizaliwa katika hali hiyo. Wale wengine walihaswa. Kulingana na Express, wavulana wenye sura ya haiba wanashawishiwa au kuibiwa na kupelekwa kwenye kimojapo vitovu vingi vya kufanya watu matowashi katika India. Huko hao wavulana hutiishwa kwa sherehe itiayo ndani “kutendewa kifalme” nayo hufikia upeo kwa kutolewa mapumbu yao. Baadaye, towashi mpya aliyefanyizwa huchukuliwa kulelewa na towashi aliye mkubwa zaidi, wakisitawisha uhusiano “wa mama na binti.” Matowashi hawa hupewa majina ya kike na hatimaye hutenda na huvaa kama wanawake. Matowashi walio wengi hupangwa kuwa kidhehebu chenye mungu mwangalizi. Kuna mahekalu kotekote India ambayo katika hayo matowashi huheshimiwa na kustahiwa kama viumbe vya kimungu wakati wa sherehe fulani ya kila mwaka.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki