Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 9/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Otizimu—Kukabiliana na Magumu ya Kasoro Tatanishi
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1999
  • Mtoto Alaleje?
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 9/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kijana Mwenye Ujasiri Nina umri wa miaka 15, na nataka kuwashukuru kwa ile makala ya Januari 22, 1995, iliyokuwa na kichwa “Imani ya Joshua—Ushindi kwa Haki za Watoto.” Iligusa moyo kama nini kusoma kuhusu mtu aliye na umri kama wangu ambaye ana imani na upendo kama huo kwa Yehova! Kusoma makala hii kulinifanya nitambue kwamba nahitaji kuchukua uhusiano wangu pamoja na Yehova kwa uzito zaidi.

M. S., Marekani

Nina umri wa miaka 16 na naona ikiwa vigumu sana kupata wakati wa kusoma magazeti yetu yote. Lakini nilisoma ile makala kuhusu Joshua, na sijapata kuhisi nikiwa nimeguswa moyo jinsi hiyo na kitu chochote. Msimamo wake dhidi ya kukubali utiaji-damu mishipani ulikuwa wenye nguvu sana! Singeweza kujizuia ila kulia. Sasa natambua kwamba nahitaji kusoma kila kitu niwezacho kinachotoka katika tengenezo la Yehova.

T. S., Uingereza

Mimi ni Mwanglikana, lakini hufurahia kusoma Amkeni! Siwezi kujizuia ila kulia kwa kile alichopitia Joshua na kwa wakati uleule kumsifu Mungu kwamba kuna watu wenye imani kama hiyo katika Yeye.

P. O., Nigeria

Mimi ni mhudumu wa wakati wote mwenye umri wa miaka 17 na nina ugonjwa unaosababisha upungufu mbaya sana wa damu. Daktari wangu alitaka kunipendekezea damu, lakini ninashughulikia tatizo hili. Niliisoma hiyo makala mara kadhaa, na kila wakati ilinipa ujasiri zaidi.

I. L. M., Brazili

Hata kifo cha wapendwa hakijapata kunigusa kufikia kiwango cha kumwaga machozi. Lakini nilijipata nikimwaga machozi nilipokuwa nikisoma ono la Joshua. Imani, ujasiri, na uaminifu-maadili wake vilinigusa.

T. M., Zimbabwe

Kulala Pamoja na Mtoto Tuligundua katika toleo lenu la Julai 22, 1994, dondoo lililoripoti utafiti wa Dakt. James McKenna. (“Kuutazama Ulimwengu”) Lilidokeza kwamba akina mama kulala na watoto wao kutapunguza SIDS (Kifo cha Ghafula cha Mtoto Mchanga). Uchunguzi wa New Zealand wa Vifo vya Watoto umeonyesha kwamba kuna hatari iliyoongezeka zaidi ya SIDS ikiwa wazazi wanakuwa na mtoto kitandani wanapokuwa wamelala.

Dakt. S. L. T., New Zealand

Asante kwa habari hiyo. Dakt. McKenna hivi majuzi alirekebisha msimamo wake na kukubali hatari ya kusongwa pumzi kiaksidenti kwa kitoto mama alalapo pamoja na mtoto wake. (Linganisha 1 Wafalme 3:19.) Kwa hivyo madaktari wengi hukataza mtu kulala pamoja na mtoto wake na walipendekeza kuweka kitoto kilale katika kitanda kidogo cha mtoto ambacho hakina mito au matandiko mazito ya juu ya kitanda.—Mhariri.

Nyuki Dhidi ya Kompyuta Ni lazima tu nionyeshe shukrani zangu kwa ile makala “Nyuki Dhidi ya Kompyuta.” (Februari 8, 1995) Hiyo makala ilinigusa kwa kina sana. Muumba wetu Mtukufu alifanya hata viumbe vidogo mno kama nyuki viwe vya kiajabu na vya kipekee.

C. K., Ujerumani

Otizimu Asanteni sana kwa ile makala “Otizimu—Kukabiliana na Magumu ya Kasoro Tatanishi.” (Februari 8, 1995) Kuna mvulana mwenye otizimu katika kutaniko langu, na nimempenda sana. Hiyo makala ilinisaidia kuelewa otizimu. Sasa najua kwamba naweza kuwa mwenye usaidizi kwa kutumia tu wakati pamoja naye na mama yake.

A. F., Japani

Binti yetu si mwenye otizimu, lakini ana vitabia vilivyo sawa na vya otizimu. Twafurahi kwamba nyinyi mwapasha watu habari kuhusu matatizo waliyo nayo watoto wengi. Inatia moyo sana watu wanapowatendea watoto hao kama binadamu wanaostahiki uhai. Maelezo kama vile ‘nakusikitikia sana’ au ‘singeweza kamwe kufanya vile ufanyavyo’ si yenye kujenga. Binti yetu anafurahi, na nyakati fulani watoto wetu wengine hutupatia mkazo zaidi. Hatughairi kuzaliwa kwake.

L. H., Marekani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki