Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 10/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Otizimu—Kukabiliana na Magumu ya Kasoro Tatanishi
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 10/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Mazungumzo Asanteni kwa ile makala “Mazungumzo Ni Usanii.” (Aprili 8, 1995) Nimeng’ang’ana na haya kwa muda mrefu. Lakini sasa nafahamu kwamba si mimi peke yangu mwenye tatizo hili. Nitayatumia vizuri madokezo yenu.

A. L., Marekani

Dokezo lenu la kusoma makala katika Mnara wa Mlinzi na Amkeni! kweli ni lenye matokeo. Utashangaa kuona kuna mengi ya kuzungumzia ukifanya hivyo!

V. M. J., Marekani

Kambi ya Mateso Rafiki wangu mmoja alisoma ile makala “Chuki Yangu Iligeuka Kuwa Upendo.” (Januari 8, 1995) Yeye adai kwamba kinyume na vile hiyo makala ilitaarifu, hakukuwa na ishara “Arbeit Macht Frei” (Kazi Huweka Huru) katika kambi ya Buchenwald.

H. J. Z., Ujerumani

Tafadhalini tuwieni radhi kwa hilo kosa. Ile ishara katika mwingilio wa Buchenwald yaweza kuonekana huko hadi leo hii, na kwa hakika inasomeka “Jedem das Seine” (Kila Mtu Atapokea Kulingana na Thawabu Yake). Kambi za Auschwitz na Sachsenhausen zilikuwa na ishara “Arbeit Macht Frei.”—Mhariri.

Otizimu Asanteni sana kwa ile makala “Otizimu—Kukabiliana Na Magumu ya Kasoro Tatanishi.” (Februari 8, 1995) Hatimaye, naweza kuelewa ugonjwa unaomsumbua binti yangu na kujua kwamba haukutokana na malezi yangu. Utumishi wangu kwa Yehova hunipa nguvu kushughulika na hali yake.

M. H., Uswisi

Visababishi vingi vya kishirikina vimehusianishwa na otizimu, kama vile laana kutoka kwa wazazi wa kale ama adhabu ya matendo ya wakati uliopita. Kile ambacho mmeandika kitasaidia kutokeza uelewevu bora wa tatizo hili. Asanteni kwa makala kama hizo zenye kuelimisha.

M. A., Nigeria

Okidi Mimi ni mpenda okidi! Kwa hakika, nina okidi katika bustani yangu na mkusanyo wa picha zazo. Asanteni kwa kuchapisha ile makala “Kutafuta Okidi Katika Ulaya.” (Januari 22, 1995) Natumaini makala hiyo haitakuwa yenu ya mwisho kuchapisha kuhusu habari hii.

R. M., Filipino

Kuendesha Gari Salama Umri wangu uko katikati ya miaka ya 40 na sikuruhusiwa kamwe kuendesha gari kwa sababu ya kifafa. Baada ya upasuaji wa kichwa, nilipata idhini kutoka daktari wangu wa ubongo ya kuomba leseni ya dereva! Ile makala “Je, Wewe Ni Dereva Salama?” (Februari 8, 1995) ilinisaidia kuthamini umuhimu wa kuwa na mtazamo ufaao unapoendesha gari. Ilikuja mara tu baada ya mimi kupokea leseni yangu!

G. S., Marekani

Dhambi Isiyosameheka Nawashukuru kwa ile makala “Vijana Huuliza . . . Je, Nimetenda Ile Dhambi Isiyosameheka?” (Novemba 8, 1994) Nilikuwa na machozi machoni pangu nilipokuwa nikiisoma kwa sababu mimi pia hung’ang’ana na zoea hili chafu la punyeto. Nilifuata vielelezo vya Marco na Alberto, waliotajwa katika hiyo makala, ambao kila mmoja wao alikuwa na ujasiri wa kuzungumza na mzee fulani. Jambo hili lilinisaidia sana.

A. M. C., Brazili

Punyeto ni mojapo pigano lililo gumu zaidi ambalo kijana Mkristo angeweza kupata. Mara nyingi nimejihisi kutofaa na kuvunjika moyo. Hiyo makala ilinitia moyo kuendelea kupigana ili kushinda vita hii.

F. G. M., Mexico

Nilijihusisha na mwenendo mlegevu na kijana mvulana niliyetumaini kuolewa naye; huo uliharibu uhusiano wetu. Nilishuka moyo sana nami nililia mchana na usiku. Kwa kweli nilifikiri singesamehewa. Kusoma makala hizi kulirudisha imani yangu kwa Yehova na uwezo wake wa kuweza kusamehe na kusahau.

L. C., Australia

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki