Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 10/22 uku. 31
  • Magenge ya Wanawake—Mwelekeo wa Kutisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Magenge ya Wanawake—Mwelekeo wa Kutisha
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Nijiunge na Genge?
    Amkeni!—1992
  • Tatizo Laenea
    Amkeni!—1998
  • Mambo Tupaswayo Kujua Kuhusu Magenge
    Amkeni!—1998
  • Kuwalinda Watoto Wetu na Magenge
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 10/22 uku. 31

Magenge ya Wanawake—Mwelekeo wa Kutisha

“NI WAKATILI, wakali na wa kinyama” ndiyo maneno yaliyotumiwa na gazeti la habari The Globe and Mail kufafanua magenge ya wasichana katika shule za sekondari za Kanada. Wakiwa wamechoka kuwa washiriki wa magenge ya wanaume, idadi yenye kuongezeka ya wasichana wanaonyesha hali yao ya kujitegemea. Polisi mmoja mpelelezi wa Toronto, anayechunguza hasa magenge ya vijana, alionelea kwamba wasichana “wanajitokeza kwa njia yenye jeuri sana.” Wako tayari “kutumia silaha na nguvu za ‘kupita kiasi’” na mara nyingi “wao ni wakatili na wakali kuliko wenzao wa kiume,” akasema Dakt. Fred Mathews katika Globe. Kwa nini? Ufahamu wenye kuenea miongoni mwa vijana hao wavunjao sheria, kulingana na konstebo mmoja wa polisi, ni kwamba “wasichana wanaelekea zaidi kufungwa gerezani muda mfupi wakikamatwa.” Msemaji mmoja wa polisi aliliambia Globe kwamba “wasichana hata wa miaka 11 wanahusika katika kuvunja sheria ndogo-ndogo na kulangua dawa za kulevya na silaha katika shule za sekondari.”

Dakt. Mathews, aliye mwanasaikolojia mmoja mwenye mamlaka juu ya ujeuri huo, aliwahoji washiriki wa magenge ya wanawake kwa kipindi cha miaka kumi na kuwapata kuwa “wenye hasira na wakaidi, hasa kwa sababu ya familia yenye kuwatenda vibaya au iliyovunjika.” Ni nini kiwavutiacho vijana hao kwa magenge hayo? Magenge yawapa “hisia ya kuwa salama akiwa sehemu ya kikundi fulani,” asema mshiriki wa zamani. Walakini, alipohojiwa na lile gazeti la habari, alikiri kujaribu kujiua mara mbili ili kuponyoka lile genge naye aliongezea hivi: “Nyingi za zile ziitwazo isivyofaa, vifo vya kiaksidenti na kule kujiua kimakusudi katika viunga hasa ni uuaji wa kimakusudi wa magenge. Mnalindana dhidi ya magenge mengine mnapokuwa katika genge. Tatizo ni kwamba hamwezi kulindana dhidi ya washiriki wa genge lenu wenyewe.”

Mwalimu mmoja mwenye hangaiko wa shule ya sekondari alisema hivi: “Hali ya wasichana wajeuri tunaoshughulika nao haijulikani kabisa. Wanapokuwa na hasira huwezi kujua ni tendo gani la jeuri watakalofanya. Na ukiwa mwalimu hilo linaogopesha sana.” Kuhusu “siku za mwisho,” Biblia ilitabiri kwamba nyakati zingekuwa “ngumu kushughulika nazo” kwa sababu watu, kutia ndani na vijana, wangekuwa “wasio na hali ya kujidhibiti, wakali.”—2 Timotheo 3:1-5, NW.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki