Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 9/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1998
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1998
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1998
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 9/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Je, Njia ya Uwasiliano ya Morse Yakaribia Kutoweka? Habari katika makala “Njia ya Uwasiliano ya Morse Yakaribia Kutoweka Ikiwa na Miaka 150,” iliyochapishwa katika “Kuutazama Ulimwengu,” ingeweza kupotosha. (Agosti 8, 1997) Njia ya uwasiliano ya Morse bado yatumika katika vipitisha-ishara vya kuongoza ndege na katika upitishaji wa mawimbi ya masafa mafupi.

H. K., Uholanzi

Asante kwa kutaja jambo hili. Kama vile msomaji wetu anavyosema kwa usahihi, kutoweka kwa Njia ya Uwasiliano ya Morse tulikoripoti kulirejezea hasa utendaji wa baharini.—Mhariri.

Kifua Kikuu Nilifurahia makala “Kifua Kikuu—Kurudi kwa Muuaji.” (Desemba 22, 1997) Katika mwaka wa 1988 niliambukizwa kifua kikuu na nikapona. Hamukukosea kusema kwamba lazima wagonjwa watumie dawa zao “kwa ukawaida bila kukosea.”

Y. L., Ufaransa

Mama-mkwe wangu, asiyependezwa na dini, aliiona makala hiyo ikiwa juu ya meza yangu na kuisoma. Alitaka kwenda nayo kwake. Nilimtolea matoleo mengine mawili ya Amkeni! Asanteni kwa kazi ngumu mnayofanya ili kutokeza kila gazeti.

L. N., Marekani

Miaka 11 iliyopita niliambukizwa kifua kikuu. Habari iliyotolewa ilikuwa sahihi kwelikweli. Nyakati nyingine, kuisoma kulikuwa kama kurudia tena jambo lililonipata. Namshukuru Yehova kwa zawadi ya uhai na kwa shauri tunalopokea kwa ukawaida katika Amkeni! ili kulinda afya yetu.

G. B., Italia

Nilipata matibabu kwa muda wa miezi sita nilipoambukizwa maradhi haya. Makala yenu ilinisaidia kujifunza mengi kuhusu maradhi haya yenye kuua. La maana zaidi, imenisaidia kujenga imani yangu kwamba Ufalme wa Mungu utaleta suluhisho la tufeni pote kwa tatizo hili.

P. P., Indonesia

Simulizi la Maisha Makala “Kubaliana na Mteja Sikuzote” iligusa moyo wangu kwa kina kirefu. (Desemba 22, 1997) Nilikuwa na watoto 11 kama vile Wei Tung Chin. Nilitiririkwa machozi alipokuwa akisimulia simulizi lake. Najua anaonea fahari watoto wake na familia zao. Watoto wangu wanne bado hawajaukubali Ukristo kuwa njia yao ya maisha. Labda siku moja nitapata shangwe kama yeye.

E. H., Marekani

Sikuzote mimi hupata masimulizi ya maisha katika Amkeni! kuwa yenye kutia moyo sana. Simulizi la Wei Tung Chin lilinigusa moyo sana. Twaweza kufurahi kama nini kwamba watu walio na thamani kama hao ni sehemu ya watu anaokusanya Yehova.

I. T., Ujerumani

Kibandiko Chenye Kosa! Nataka kuwashukuru kwa makala zenye kupendeza “Umaridadi wa Mbuga za Taifa za Milimani.” (Novemba 22, 1997) Nimefurahia kuona na kupiga picha wanyama wote walioelezwa katika makala hii kwa kuwa mimi hupenda milima na kupiga picha. Hata hivyo, naamini kwamba kuna kosa katika maelezo ya picha iliyo sehemu ya juu ya ukurasa wa 15. Nafikiri kwamba wanyama wanaoonyeshwa hapa, si paa-mbuzi, bali ni mbuzi-mwitu wa kike.

M. D. M., Italia

Tungependa kumshukuru msomaji wetu kwa kuona kosa hili.—Mhariri.

Moscow Asanteni kwa makala “Moscow—Ukumbusho Wake wa Miaka 850.” (Desemba 22, 1997) Warusi ni wakaribishaji na ni wenye urafiki sana. Katika mwaka wa 1989 wakati Warusi 3,000 walipokuja kwenye mkusanyiko wa Kikristo katika Poland, nilipata kujionea jambo hilo. Nilichochewa sana na ukurasa wa mwisho wa toleo hilo ulioonyesha dada Mrusi akihubiri katika sehemu za mashambani za Urusi. Yehova na awaruhusu watu wengi zaidi wasemao lugha ya Kirusi wawe waabudu wake!

I. L., Ujerumani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki