Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 1/22 uku. 3
  • Chakula Kinapokuwa Adui Yako

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Chakula Kinapokuwa Adui Yako
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nini Husababisha Matatizo ya Kula?
    Amkeni!—1999
  • Matatizo ya Kula—Ni Nini Kinachoweza Kusaidia?
    Amkeni!—1999
  • Kwa Nini Ninahangaikia Sana Uzito Wangu?
    Amkeni!—1999
  • Kujinyima Chakula na Kuwa na Hamu ya Chakula Isiyo ya Kawaida—Mambo Hakika, Hatari
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 1/22 uku. 3

Chakula Kinapokuwa Adui Yako

Akitafakari juu ya miaka alipokuwa tineja, Jean akumbuka waziwazi akitaniwa na kudhihakiwa. Sababu ilikuwa gani? Alikuwa msichana mrefu na mnene zaidi katika darasa lake shuleni. Lakini si hivyo tu. “Jambo lililokuwa baya zaidi ya kuwa mkubwa, ni kwamba nilikuwa mwenye haya na mwenye kujifikiria sana,” asema Jean. “Mara nyingi nilikuwa mpweke, nikitaka nikubaliwe, lakini mara nyingi nilihisi kama mgeni.”

Jean alisadiki kwamba ukubwa wa mwili wake ndio uliokuwa chanzo cha matatizo yake yote na kwamba kama angekuwa na umbo zuri jembamba matatizo yake yote yangekwisha. Si kwamba Jean alikuwa mnene kupita kiasi. Kinyume cha hilo, akiwa na urefu wa futi sita na uzito wa kilogramu 66, hakuwa amezidisha uzito. Hata hivyo, Jean alijihisi kuwa mnene, na alipokuwa na umri wa miaka 23 aliamua kupunguza uzito. Alifikiri hivi, ‘Nikiwa mwembamba, watu wengine watataka kuwa karibu nami. Mwishowe nitajiona kuwa ninakubalika na kuwa wa pekee.’

“Kusababu huko kwa kipumbavu kuliongoza kwenye mtego wa miaka kumi na miwili wa kuwa na tatizo la kujinyima chakula na kuwa na hamu ya chakula isiyo ya kawaida,” aeleza Jean. “Ni kweli nilikuwa mwembamba, mwembamba sana hivi kwamba nilikaribia kufa, lakini badala ya kuishi maisha yenye furaha, niliharibu afya yangu na kusababisha mshuko-moyo na taabu iliyodumu kwa zaidi ya mwongo mmoja.”

JEAN hayuko peke yake. Kulingana na kadirio moja, 1 kati ya wanawake 100 Wamarekani hupatwa na tatizo la kujinyima chakula akiwa tineja au kijana, na labda idadi inayozidi hiyo mara tatu wanakuwa na hamu ya chakula isiyo ya kawaida. “Nimefanya kazi shuleni na kwenye vyuo kwa miaka kadhaa,” asema Dakt. Mary Pipher, “na ninajionea moja kwa moja kwamba matatizo ya kula yameenea tu kama wakati wowote.”

Pia ni ya namna nyingi. Wakati mmoja yalifikiriwa kuwa tatizo la matajiri lakini sasa yanaonwa kuwa ya kawaida katika watu wa viwango vyote vya jamii na kiuchumi. Hata idadi ya wanaume wanaopatwa na tatizo hili inaongezeka, ikilifanya gazeti la Newsweek liyaite matatizo ya kula kuwa “yanayoshambulia wanaume na wanawake bila kubagua.”

Ingawa hivyo, jambo linalohangaisha zaidi hasa, ni kwamba wastani wa umri wa watu wanaotibiwa kwa matatizo ya kula unazidi kupungua. “Kuna wasichana chini ya umri wa miaka 10, hata wengine ni wachanga sana wakiwa na umri wa miaka 6, wanaolazwa hospitalini,” asema Margaret Beck, kaimu mkurugenzi wa kitivo cha matatizo ya kula katika Toronto. “Bado ni idadi ndogo,” aongezea, “lakini inakua.”

Kwa ujumla, matatizo ya kula huathiri mamilioni—hasa wasichana na wanawake vijana. “Hawafikiri juu ya chakula au kula chakula kama wafanyavyo watu wengi,” asema mfanyakazi wa huduma za jamii Nancy Kolodny. “Badala ya kula wanapohisi njaa, kula kwa sababu ya lishe na afya njema, kula kwa ajili ya kujifurahisha, au kula ili kufurahia ushirika unaofaa na wengine, wanakula chakula kupita kiasi na kufanya mambo ambayo hayaonwi kuwa ya ‘kawaida’—kama vile kusitawisha desturi zisizo za kawaida kabla hawajaanza kula, au kujilazimisha kutapika mara moja chakula walichokula.”

Acheni tuchunguze kwa makini matatizo mawili ya kula: kujinyima chakula na kuwa na hamu ya chakula isiyo ya kawaida.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki