Mwisho wa Uharibifu
Na Mleta Habari Wa Amkeni! Katika Uingereza
“Thuluthi moja ya viumbe asili vya ulimwengu vimeharibiwa na shughuli za binadamu kwa miaka 25 iliyopita.”
NDIVYO lilivyoripoti Shirika la Hazina ya Ulimwengu ya Viumbe Asili. Idadi hiyo yenye kushtusha ilifunuliwa wakati wa kutolewa kwa Living Planet Index, mchanganuo mpya wa mazingira ya ulimwengu.
Wahifadhi waliripoti upungufu wa asilimia 10 katika maeneo yenye misitu ya sayari. Lakini tarakimu hii haifunui hasara nyingi zaidi katika misitu ya mvua na maeneo ya misitu iliyokauka, bila kutaja kupotea kwa viumbe wa misitu, ambako labda kwapita asilmia 10, lasema gazeti la habari The Independent la London. Mazingira ya ndani ya maji yamepoteza asilimia 30, iliyo dhahiri katika kupungua kwa aina za wanyama kama vile tuna ya bluefin katika bahari ya Atlantiki na kobe aitwaye leatherback katika bahari za Asia. Mbaya zaidi ni ule upungufu wa asilimia 50 wa viumbe wa maji baridi katika ule mchanganuo wa mfumikolojia uitwao Freshwater Ecosystems Index, ambao umesababishwa hasa na ongezeko la uchafuzi wa kilimo na kiviwanda pamoja na kutumiwa kwa maji mengi sana.
“Kuhifadhiwa kwa mifumikolojia ya asili si anasa ya matajiri peke yao,” akaeleza Bwana Ghillian Prance, mkurugenzi wa Royal Botanical Gardens huko Kew, London, Uingereza, “lakini ni muhimu kuhakikisha udumishaji wa utendaji mbalimbali wa ikolojia ya sayari yetu ambayo katika hiyo sisi sote huitegemea ili kuendelea kuishi.” Kila mkazi wa sayari hii anahusika. Kwa hiyo, suluhisho lenye kudumu la tufeni pote laweza kupatikanaje?
Kwa kupendeza, kitabu cha mwisho cha Biblia, Ufunuo, hutaja wale wanaoiharibu dunia. Hicho hutabiri wakati ambapo watu kama hao wenyewe wataharibiwa. (Ufunuo 11:18) Je, kutakuwako waokokaji? Ndiyo, kwa sababu hilo litatimizwa wakati “Yehova Mungu, Mweza-Yote,” atakapoingilia kati, kwa kuwa yeye ndiye mwenye suluhisho pekee la matatizo ya mazingira ya dunia hii na uwezo wa kulitekeleza. (Ufunuo 11:17) Ufunuo 21:3 hufafanua wakati ambao Mungu “atakaa pamoja na [wanadamu], nao watakuwa vikundi vya watu wake.”
Wewe wawezaje kuwa mmoja wa ‘watu wake’ na uwe na tazamio la kuona kuzorota kwa mazingira kwa siku hizi kukibatilishwa? Tafadhali wasiliana na Mashahidi wa Yehova katika eneo lenu kwa kuwaandikia ukitumia mojawapo ya anwani zilizo kwenye ukurasa wa 5. Au zungumza nao wakati ujao wanapokutembelea nyumbani kwako. Watafurahi kukusaidia ujifunze mengi zaidi juu ya jambo unaloweza kufanya sasa ili kuwa tayari wakati Mungu achukuapo hatua hivi punde.