Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 11/22 kur. 3-4
  • Kuvutiwa Sana na Malaika

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuvutiwa Sana na Malaika
  • Amkeni!—1999
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Malaika Wapendwa Sana
  • Mamia ya Vitabu
  • Namna Malaika Wanavyoweza Kukusaidia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Kuthibitisha Masimulizi Hayo
    Amkeni!—1999
  • Malaika—Je! Wao Wanaathiri Maisha Yako Wewe?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Je, Una Malaika Mlinzi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 11/22 kur. 3-4

Kuvutiwa Sana na Malaika

“‘Sote’ tuna malaika wanaotuongoza, wanaotulinda . . . Tusipowasumbua na tukijiendesha kama watoto, kwa kutumaini na kupenda kikamili na kushukuru kwa unyenyekevu, ndipo watakapotubariki kupita kiasi. Wao hucheza nasi. Wanatutunza. Wanatuponya, wanatugusa, wanatufariji kwa uchangamfu pasipo kuonekana, na sikuzote wao hujaribu kutupa vitu tunavyotaka.”—Kutoka kwa kitabu “Angel Letters.”

NI SHARTI ukiri kwamba maoni hayo yaliyoenea sana kuhusu malaika huvutia sana. Kulingana na ile hali ambayo watu fulani wanaiita “hali mpya ya kiroho,” kila mmoja wetu amepewa angalau malaika mmoja, aliye na jukumu la kutufariji na kutulinda kutokana na madhara. Inasemekana kwamba malaika wako ana nguvu nyingi na ni mwenye upendo. Yeye hataki umtii wala umwabudu, na hatawahi kamwe kukuhukumu wala kukukemea. Sikuzote yuko nawe, akijitoa mwenyewe kwa ajili ya hali yako njema na akiwa tayari kutimiza matakwa yako yote. Watu wengi leo huamini kwa dhati mambo haya.

Bila shaka kuamini malaika si jambo jipya. Wametimiza fungu kubwa katika itikadi za kidini za watu tangu nyakati za kale. Hili hudhihirishwa na sanaa. Mifano ya makerubi, aina ya malaika, ilipamba tabenakulo na hekalu la kale la Kiyahudi. Makanisa mengi ya Jumuiya ya Wakristo yamepambwa kwa malaika. Majumba ya makumbusho yamejaa michoro na sanamu za kuchongwa za malaika.

Malaika Wapendwa Sana

Katika nyakati za karibuni, malaika wamepata kupendwa sana katika nchi fulani. Mara nyingi sinema huonyesha malaika wakiwa kama wanadamu waliokufa ambao wamerudi duniani kutenda mambo mema. Katika filamu moja, malaika waisaidia timu ya besiboli inayoshindwa. Katika nyingine, malaika-mlinzi amsaidia mvulana tineja kulipiza kisasi uuaji kimakusudi wa rafikiye wa kike. Kichwa cha malaika-msaidizi kinakaziwa sana katika kipindi kinachopendwa sana kwenye televisheni huko Marekani.

Kuna nyimbo chungu nzima kuhusu malaika. Katika miongo ya majuzi huko Marekani, wimbo 1 kati ya 10 zinazopendwa sana unataja malaika. Kufikia miaka ya kati ya 1900, zaidi ya “maduka ya nguo ya malaika” 120 yalikuwa yamefunguliwa katika Amerika. Maduka hayo huuza sanamu ndogo za malaika, jebu, na vifaa vya kuandikia vyenye malaika—hata vichezeo vya watoto vilivyorembwa kwa mifano ya malaika. Semina na vijarida vinadhaniwa kuwafunza watu jinsi ya kuwasiliana na viumbe hao wa kimbingu. Magazeti, magazeti ya habari, na vipindi vya mazungumzo husimulia jinsi ambavyo watu walikutana na malaika.

Mamia ya Vitabu

Kisha kuna vitabu. Duka moja kubwa la vitabu katika New York City huuza zaidi ya aina 500 za vitabu vinavyozungumzia malaika, hasa malaika-walinzi. Vitabu vya aina hii huahidi kuwaonyesha wasomaji jinsi ya kuwasiliana na malaika-walinzi, kujifunza majina yao, kuongea nao, na kupata msaada wao. Vitabu hivyo huwa na masimulizi mengi ya jinsi ambavyo malaika wameonekana wakati wa uhitaji, wakiwanusuru watu kutokana na magari yaliyoko barabarani, kutibu maradhi hatari, kufariji wanaosononeka, na kuwalinda askari-jeshi katika uwanja wa mapigano. Malaika hao hutumikia “bila kudai ishara ya kutubu, kugeuzwa imani, au ya kuwa mwaminifu kwa mafundisho ya kidini.” Lakini masimulizi haya ya kisasa ya “kukutana na malaika” huchochea watu kwa nadra sana wafanye mabadiliko maishani mwao. Kwa kawaida wale wanaodai walikutana na malaika huwa tu na hisia changamfu.

Masimulizi haya yaweza kuonekana kuwa habari njema ajabu katika enzi yenye mikazo na matatizo. Lakini je, yaweza kutumainiwa? Je, ni jambo la kuhangaikia?

[Blabu katika ukurasa wa 4]

Wengi huhisi kwamba wamekutana na malaika

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki