Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g01 11/8 uku. 31
  • Mwanadamu Amemkandamiza Mwanadamu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwanadamu Amemkandamiza Mwanadamu
  • Amkeni!—2001
  • Habari Zinazolingana
  • Wanawake wa India—Wakisonga Kuingia Katika Karne ya 21
    Amkeni!—1995
  • Je, Wahindi wa Brazili Wanakabili Hatari ya Kutoweka?
    Amkeni!—2007
  • Jinsi Ulimwengu Wao Ulivyopotea
    Amkeni!—1996
  • Wakati Wao Ujao Una Nini?
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2001
g01 11/8 uku. 31

Mwanadamu Amemkandamiza Mwanadamu

HISTORIA yathibitisha ukweli wa maneno ya Mhubiri 8:9 (Chapa ya 1989): “Mtu mmoja anayo mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasara yake.” Au kama Jerusalem Bible ya Katoliki isemavyo, “mwanadamu amemkandamiza mwanadamu na kumuumiza.” Mamilioni ya watu wamedhulumiwa. Hali hiyo imekuwepo katika karibu kila mfumo wa serikali za wanadamu. Hotuba iliyotolewa na katibu-msaidizi anayeshughulika na Mambo ya Ndani ya Wahindi Wamarekani katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani ilionyesha tena dhuluma hiyo. Hotuba hiyo ilitolewa wakati wa sherehe ya kuadhimisha mwaka wa 175 tangu kuanzishwa kwa Ofisi ya Mambo ya Ndani ya Wahindi Wamarekani.

Alisema kwamba, huo haukuwa wakati wa kusherehekea bali ulikuwa “wakati wa kusema kweli zenye kuhuzunisha, wakati wa majuto.” Alikubali kwamba jukumu la kwanza la Ofisi ya Mambo ya Ndani katika miaka ya 1830 lilikuwa kufukuza mataifa ya kikabila ya kusini-mashariki kutoka kwenye mashamba yao. Makabila hayo ni Wacherokee, Wacreek, Wachoctaw, Wachickasaw, na Waseminole. “Kwa kutishwa, kudanganywa, na kulazimishwa kinguvu, watu wa mataifa hayo makubwa ya kikabila walishurutishwa kutembea kilometa 1,600 huku wakiwazika maelfu ya wazee wao, vijana wao na wadhaifu katika makaburi yaliyochimbwa haraka kwenye ile Njia ya Machozi.”

Aliendelea kusema hivi: “Hata hivyo, katika nyakati hizi za watu walioelimika, ni lazima watu wakubali kwamba kueneza magonjwa kimakusudi, kuangamizwa kwa makundi ya nyati, kutumia vileo vinavyodhuru ili kuharibu akili na mwili, na mauaji ya ovyoovyo ya wanawake na watoto yametokeza msiba wenye kutisha sana hivi kwamba hatuwezi kusema msiba huo umetokea tu kwa sababu ya mgongano usioepukika wa tamaduni zinazoshindana.”a Alikubali hivi: “Shirika hili lilinuia kuharibu vitu vyote vya Wahindi. Shirika hili lilipiga marufuku lugha zote za Wahindi . . . na kuwafanya Wahindi wajidharau. Zaidi ya yote, Ofisi ya Mambo ya Ndani ya Wahindi Wamarekani iliwatendea mambo hayo watoto waliokuwa kwenye shule zake za bweni, na kuwaumiza kihisia, kiakili, kimwili, na kiroho.”

Alimalizia kwa kusema hivi: “Acheni tuanze kwa kuomba msamaha kabisa kwa ajili ya mambo ambayo shirika hili lilifanya wakati uliopita. . . . Katu hatutaiba tena mali ya Wahindi. . . . Katu hatutashambulia tena dini zenu, lugha zenu, sherehe zenu za kitamaduni, au mambo mengine ya kabila lenu.” Zaidi ya yote, alisema hivi: “Ni lazima tufute machozi ya vizazi saba tukiwa pamoja. Ni lazima tuondoe majonzi yetu tukiwa pamoja.”—Vital Speeches of the Day, Oktoba 1, 2000.

Ufalme wa Mungu ndio utatuzi tu wa kweli na wa kudumu kwa ukatili ambao mwanadamu anamtendea mwenziwe. Ufalme huo utawawezesha wote kupata haki tena na ‘kufuta kabisa kila chozi kutoka katika macho yao, na kifo hakitakuwapo tena, wala ombolezo wala kupaaza kilio wala umivu halitakuwapo tena kamwe. Mambo ya zamani yamepitilia mbali.’—Ufunuo 21:3, 4.

[Maelezo ya Chini]

a Historia ya Wahindi Wamarekani yathibitisha kwamba mara nyingi makabila hayo yalipigana yenyewe kwa yenyewe, hivyo yaliendelea kupigania “mashamba, farasi, na nyati.”—The People Called Apache.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

Mhindi: Artwork based on photograph by Edward S. Curtis; Ramani: Mountain High Maps® Copyright © 1997 Digital Wisdom, Inc.; Makao ya Wahindi: Leslie’s

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki