Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w74 8/1 uku. 356
  • Ufahamu Katika Habari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ufahamu Katika Habari
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Uhuru kutokana na Tumbako
  • Wakatoliki na Wakomunisti
  • Maadili ya Tumbaku?
    Amkeni!—1992
  • Tumbako na Uchunguzi wa Kama Yafaa Kutumiwa
    Amkeni!—1990
  • Kuongozwa na Dhamiri Katika Kufanya Mema kwa Wote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Sigareti—Je, Wewe Huzikataa?
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
w74 8/1 uku. 356

Ufahamu Katika Habari

Uhuru kutokana na Tumbako

● Mazao ya ulimwengu ya tumbako yamepanda kwa karibu kiasi cha 12 kwa mia miaka kumi iliyopita. Hili limetukia ujapokuwa uhakika wa kwamba utabibu unakamatanisha kuvuta sigara na maradhi mengi. Ushuhuda unazidi kuongezeka kwamba hata watoto wa wavutaji wanapatwa na madhara. Kwa sababu gani watu wengi zaidi hawaachi?

Daktari F. R. Wake, wa Canada’s Carleton University, anasema hivi: “Ugumu mkubwa siyo kuwafanya watu waache kuvuta sigara, bali kuwazuia wasiirudie wanapokwisha kuiacha.” Ajabu ni kwamba, kujua tu kuvuta sigara kunasababisha donda baya sana mara nyingi hakutoshi.

Kuvuta sigara hakujapata kuwa ugumu mkubwa kati ya mashahidi wa Yehova. Tangu miaka ya kuanzia wa 1890 wao wameandika maonyo juu yake. Sasa, tangu kipindi cha mwisho cha mwaka wa 1973, ye yote anayekuja kuwa mmojawapo wa mashahidi wa Yehova au anayetaka aendelee kuwa mshiriki anayekubalika wa makundi yao amehitajiwa aache mazoea ya kutumia tumbako. Kizuizi kinacholingana na hiki ki juu ya wale wanaopata riziki yao kwa kufanya biashara ya tumbako.

Kwa sababu gani wanahangaikia kuachisha makundi yao kabisa na ukamatano wo wote na tumbako? Mashahidi wa Yehova wanazijua hatari za afya zinazoletwa na mazoea haya. Mbali na hayo, ulizo lililo la muhimu la adili kwao ni, Je! tunatumia miili yetu kwa njia inayoonyesha shukrani kwa Muumba wetu kwa ‘kujitakasa na kila uchafu wa mwili na roho’? (2 Kor. 7.1) Vile vile wao wanakuona kuendelezwa kwa tumbako kama kwenye kupingana na upendo wa mtu kwa jirani. Tamaa ya kibali cha Mungu inawavuta wapate uhuru kutokana na tumbako.

Wakatoliki na Wakomunisti

● Viongozi wa kidini wa Italia wa Kanisa Katoliki wameomba kwamba papa afute amri ya mwaka wa 1949 inayoamuru kwamba mtu ye yote ‘anayekubaliana na chama cha Kikomunisti atengwe na ushirika. Ni mambo gani zaidi yaliyotukia, nayo yaonyesha nini?

Nyakati za karibuni Vatican imepokea wakuu kutoka mataifa kadha ya Kikomunisti na hata imekiri tamaa ya kuanzisha uhusiano na Uchina. Watazamaji walio macho wanaona mabadiliko makubwa sana kutoka hali za kwanza za kanisa katika matendo haya. Kweli, sikuzote Kanisa Katoliki limekuwa ‘rafiki wa dunia,’ na, likiwa na maoni ya kilimwengu, kwa kawaida limepanga kuwa na mapadre na maaskofu na wafuasi wengi katika pande zote za mashindano ya kisiasa, hata vita. Kwa njia hiyo limedumisha cheo cha maongozi na mshindi bila ya kujali namna ambavyo mambo yanasuluhishwa.

Lakini leo matukio ya ulimwengu yanalilazimisha kukubali mambo yanayofunua hali yenye kudhoofika kidogo kidogo. Amani yaelekea kusitawi kati ya mataifa ya Ulaya ya Amerika na Mashariki ya Kikomunisti. Ili lidumishe nguvu kiasi fulani za kisiasa, kanisa linalazimishwa kujipatanisha na adui wake wa muda mrefu asiyeamini kuwako kwa Mungu.

Hivyo kanisa la uwezo mwingi wa kilimwengu linapoteza nguvu zake juu ya maongozi ya kisiasa ya kilimwengu. Mambo ambayo linayasema sasa ni ya kupatanisha. Haya yote yanakumbusha mfano wa unabii unaoonyeshwa katika kitabu cha Biblia cha Ufunuo sura ya 17. Humo dini yote ya uongo inaonyeshwa kama kahaba ambaye anaharibiwa mwishowe na mataifa, akiisha kupoteza amri juu ya mataifa ya kinyama.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki