Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 7/15 uku. 30
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Habari Zinazolingana
  • Michezo ya Bahati Nasibu kwa Nini Inapendwa na Wengi?
    Amkeni!—1991
  • Michezo ya Bahati Nasibu— Nani Hushinda? Nani Hupoteza?
    Amkeni!—1991
  • Harara ya Michezo ya Bahati Nasibu Kamari ya Ulimwengu
    Amkeni!—1991
  • Kamari Hupendwa Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 7/15 uku. 30

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

◼ Je! yafaa Mkristo anunue tiketi za mchezo wa bahati-nasibu ili kujitumbuiza tu ikiwa mapato yenye kutokana na mchezo huo yatumiwa kufadhili watu?

Kwa uhakika Biblia haivunji moyo kuwa na utumbuizo unaofaa, kwa maana Yehova ndiye “Mungu mwenye furaha.” (1 Timotheo 1:11, NW) Watu wake waweza kuona shangwe ya muziki, dansi yenye kiasi, ulaji au unywaji wenye kiasi, na michezo yenye usawaziko. (Zaburi 150:4; Mhubiri 2:24) Hata hivyo, ni wazi kwamba kucheza kamari hupingana na shauri la Mungu lenye hekima, na ndivyo ilivyo kuhusu kushiriki katika michezo ya bahati-nasibu.

Mchezo wa bahati-nasibu ni nini hasa? Wahusisha ndani kununua tiketi za kupata nasibu ya kushinda zawadi fulani-fulani. Washindi huamuliwa kwa kuchota namba fulani au kwa uchaguzi wa kuokota namba yoyote ile.a Mara nyingi huwa kuna zawadi moja kubwa sana, labda ikiwa ya mamilioni ya dola, mafaranga, au mashilingi. Zawadi kubwa hivyo huvutia sana hivi kwamba michezo ya bahati-nasibu imekuwa “kamari ya namna iliyoenea zaidi ya nyinginezo.” (The World Book Encyclopedia) Mamia ya mamilioni ya watu hucheza kamari kwa njia ya michezo ya bahati-nasibu.

Watu fulani wamesababu kwamba si vibaya kuhusika katika mchezo wa bahati-nasibu kwa sababu huenda gharama ya kununua tiketi (nasibu) ikawa kidogo, kwa sababu wale wanaoshiriki hufanya hivyo kwa nia yao wenyewe, na kwa sababu baadhi ya mapato ya mchezo huo huenda yakatumiwa kwa kusudi fulani la kufadhili watu, kama vile kusaidia maskini. Kusababu mambo jinsi hiyo kuna uhalali gani?

Ingawa watu fulani hudai kwamba kununua tiketi ya mchezo wa bahati-nasibu ni utumbuizo rahisi, wa gharama ndogo, haiwezi kukanwa kwamba pupa yahusika. Watu hununua tiketi za michezo ya bahati-nasibu wakitumaini kushinda pesa nyingi. Kwa uhakika jambo hili ni kinyume cha shauri la Kimungu lililo dhidi ya pupa, ambayo yaweza kuwa uovu mzito uwezao kuzuia mtu ‘asirithi ufalme wa Mungu.’ Kwa sababu hiyo, Mkristo akidhihirisha pupa yenye uendelevu kwa kucheza kamari, angeweza kuondoshwa katika kundi. (1 Wakorintho 5:11; 6:10) Biblia husema hivi; “Urithi hupatwa kwa pupa hapo kwanza, lakini wakati ujao wa urithi huo wenyewe hautakuwa wenye baraka.” (Mithali 20:21, NW) Mkristo akihisi msisimuko wowote wa ‘kujitafutia bahati yake’ katika mchezo wa bahati-nasibu, apaswa kufikiria kwa uzito juu ya pupa iliyo msingi wa mchezo huo wa bahati-nasibu. Waefeso 5:3, NW, yasema kwamba ‘pupa haipasi hata kutajwa miongoni mwetu,’ sembuse kujiachilia kwa Mkristo ili imshinde nguvu.

Kwa kawaida sehemu iliyo kubwa zaidi ya wachezaji wa bahati-nasibu hupatikana katika mitaa iliyo maskini. Kwa hiyo hata ikiwa gharama ya kununua tiketi ni kidogo, pesa zinatumiwa vibaya ambazo zimepasa kuelekezwa kwenye mahitaji halisi ya jamaa—chakula kingi zaidi, nguo za kutosha, matibabu bora zaidi. Mtu mwenye kudai kuwa Mkristo lakini mwenye kuachilia mahitaji hayo ya jamaa “ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.”— 1 Timotheo 5:8.

Hata kama gharama ya kununua tiketi ya mchezo wa bahati-nasibu haingedhuru sana pesa za mtu binafsi au za jamaa, hiyo haimaanishi kwamba wengine hawapatwi na madhara. Kwa nini? Kwa sababu karibu kila mtu mwenye kununua tiketi ya mchezo wa bahati-nasibu angependa kushinda. Zawadi ya pesa zake ingetoka wapi? Ikiwa tiketi yake iligharimu mafaranga kumi na zawadi yenyewe ni mafaranga milioni moja, hiyo yamaanisha kwamba yeye achukua pesa za tiketi hiyo kutoka kwa watu wengine mia moja elfu. Je! hiyo yapatana na shauri la Mungu lililo dhidi ya kutamani mali za watu wengine? (Kumbukumbu 5:21) Kwa uhakika, zawadi yake itahusisha pesa zilizochukuliwa kutoka kwa watu wengine wengi zaidi, kwa maana tiketi zitakazouzwa zinazidi mia moja elfu kwa mbali. Itakuwa lazima kiasi kikubwa cha pesa za tiketi kitumiwe kwa gharama za usimamizi wa kazi, na pia kiasi fulani kitumiwe kwa kusudi la kufadhili watu, kusudi ambalo hutangazwa kuwa ndiyo sababu kuu ya mchezo wa bahati-nasibu. Kwa hiyo hata ikiwa mtu ajiweza kutumia mafaranga kumi hayo ili kununua tiketi yake mwenyewe, namna gani zile hesabu kubwa za watu wenginewo? Zaidi ya hilo, labda ushindi wake utatangazwa peupe, hiyo ikisukuma wengi waanze kucheza bahati-nasibu au kununua tiketi nyingi zaidi, hata kama hawajiwezi.

Pia haiwezi kukanwa kwamba mchezo wa bahati-nasibu hufungamana na ile ndoto ya kushinda pesa bila kuzifanyia kazi. Ndiyo, mchezo wa bahati-nasibu huwatia watu moyo wawe na uvivu au huonyesha kwamba uvivu ni jambo la kuvutia. Ingawa hivyo, Biblia huhimiza watu wa Mungu watumie mapato yao kwa busara, wawe wenye bidii, na wafanye kazi kwa bidii. Badala ya kuendeleza roho ya ‘jipatie cha bure,’ hiyo hushauri hivi: “Ikiwa mtu hataki ku’anya kazi, basi, asile chakula.” —2 Wathesalonike 3:10; Mithali 13:4; 20:4; 21:25; 1 Wathesalonike 4:9-12.

Jambo la kwamba huenda wengine wakashiriki katika mchezo wa bahati-nasibu kwa hiari yao wenyewe na kwamba ni jambo halali kisheria, hiyo haitetei kwamba ni haki Wakristo kujihusisha humo. Serikali fulani-fulani huhalalisha namna nyingine za kucheza kamari, na pia umalaya na ndoa ya wenzi wengi. Ingawa huenda mambo hayo yakawa halali kisheria na watu wengi wakawa na nia ya kujihusisha humo, hii haimaanishi kwamba utendaji huo wafaa machoni pa Mungu. Badala ya hivyo, Wakristo hujitahidi kuiga maoni ya Daudi: “Ee Bwana [Yehova, NW], unijulishe njia zako, unifundishe mapito yako, uniongoze katika kweli yako, na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu.”—Zaburi 25:4, 5.

Ikiwa Mkristo ataka kikweli kuwasaidia maskini, wenye vizuizi vya kimwili, au walio wazee-wazee, kwa uhakika yeye aweza kufanya hivyo moja kwa moja au kwa njia isiyohusisha kucheza kamari.

[Maelezo ya Chini]

a Ingawa namna hii ya kucheza kamari yajulikana mahali pengi kuwa mchezo wa bahati-nasibu, huenda pia ikaitwa karata, pata-potea, changanya-changanya, farasi, au jina jingine la kienyeji.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki