Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 8/15 kur. 3-4
  • Kwa Nini Uhalifu Ni Mwingi Sana?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Nini Uhalifu Ni Mwingi Sana?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Habari Zinazolingana
  • Wakati Ambapo Hakukuwa na Uhalifu
    Amkeni!—1998
  • Wewe Unataka Uhalifu Umalizwe?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Sasa Mwisho wa Uhalifu Uko Karibu!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Kujitahidi Kumaliza Uhalifu
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 8/15 kur. 3-4

Kwa Nini Uhalifu Ni Mwingi Sana?

“UHALIFU ulio mwingi hufanywa I dhidi ya mali,” kauli hiyo yashikiliwa na broshua moja ya serikali ya Uingereza. Hata hivyo, katika nchi hiyo uhalifu wa kijeuri unaofanywa dhidi ya watu waripotiwa kuwa “uhalifu wa namna yenye kuongezeka kwa haraka zaidi,” ingawa huo ni asilimia 5 tu ya makosa yote.

Hali hii ni mfano wa ongezeko la uhalifu ulimwenguni pote. Visa vya utekwaji nyara, unyang’anyi wa kutumia silaha, kunajisiwa, na vitendo vingine vya jeuri huonyeshwa kwa ukawaida katika safu za magazeti ya ulimwengu, mara nyingi hiyo ikivuta zaidi fikira za watu kuliko ripoti za uhalifu usio na jeuri. Basi, kuna ushuhuda wa wazi kwamba wewe na mali zako huenda mkawa shabaha ya kutendwa uhalifu. Lakini kwa nini? Ni nini husukuma watu kuwa wahalifu?

Wahalifu wengi ni watu wenye utayari wa kujifaidi wenyewe kwa kurukia fursa yoyote ijitokezayo. Tokeo ni kwamba, wenye mamlaka hujitahidi kuzuia vuvumko kubwa la uhalifu kwa kuwatia watu moyo wawe na habari zaidi juu ya mambo yenye kuendelea katika ujirani wao. Ingawa mbinu hizo hutumiwa kujaribu kuzuia vitendo vya uhalifu, je! hivyo huachisha watu kuwa wahalifu? Sivyo.

Uchunguzi mwingi umefanywa kuhusu utu ule wenye kusababisha uhalifu. Kwa kupendeza, Neno la Mungu, Biblia, lafanya uandalizi wa kuchungulia jinsi mhalifu huwa akifikiri, wakati linapowaonya wanaume vijana juu ya wenye kusema hivi kwa ushawishi: “Haya njoni; acheni tutafute mtu fulani wa kuua! Acheni tushambulie watu fulani wasio na hatia ili tu tuone raha ya kufanya hivyo! Huenda wakawa hai na wazima tuwapatapo, lakini watakuwa wamekufa tumalizapo mambo yetu nao! Tutapata mali za aina zote na kujaza nyumba zetu kwa viporwa! Njoni mjiunge na sisi, nasi sote tutashiriki kile tuibacho.” (Mithali 1:11-14, Today’s English Version) Ndiyo, pupa, choyo, na maoni ya kutazamia vitu vya kimwili hukuza uhalifu.

Utumizi mbaya wa dawa za kulevya na kula-raha hutawala pia fikira ya watu wengi katika karne hii ya 20. Pesa zahitajiwa ili kulipia yale mazidio yanayotamaniwa, hata ikiwa kufanya hivyo kwataka kuumiza mtu mwingine au kumuua ili kupata pesa hizo. Katika hizi ‘nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo,’ ni kweli kwamba hesabu kubwa zaidi ya watu “hufanya haraka-haraka kuingia katika uhalifu, wakikosa saburi ili wamwage damu.” —2 Timotheo 3:1, 3, 4, NW; Mithali 1:16, The New English Bible.

Uhalifu ni “kosa zito [hasa] dhidi ya maadili,” yasema Webster’s Ninth New Collegiate Dictionary. Twaishi katika kipindi cha mvunjiko wa maadili. Mtume Paulo alionya Wakristo Waefeso juu ya watu ambao ‘hutembea katika kutofaidika kwa akili zao, huku wao wakiwa katika giza kiakili, na wakiwa wametengwa mbali kutoka kwenye uhai ulio wa Mungu, kwa sababu ya kukosa maarifa kuliko ndani yao, kwa sababu ya kukosa hisia kwa mioyo yao. [Hawa wamekuja] kupita hisia yote ya kiadili.” Vivyo hivyo, sisi twahitaji kuyasikiliza hayo leo.—Waefeso 4:17-19, NW.

Lile ongezeko kubwa la mapotosho ya ngono za ukatili ambayo hurekodiwa katika kanda za vidio, kule kutukuzwa kwa vita, na kule kufuatia raha haramu kwa njia ya ubinafsi, je! yote hayo hayachangii kufanya watu fulani wawe wahalifu huku wakifanya watu wasio na hatia wawe shabaha ya kutendwa uhalifu? Lakini bado kuna kisababishi kingine katika tandabui hili lenye kutatanisha kuhusu uhalifu. Hicho ni nini?

Ni Shetani Ibilisi. Hasira yake huwasha moto wa jeuri isiyotumia akili na uhalifu uliopo sana katika ulimwengu huu wa sasa. (1 Yohana 5:19; Ufunuo 12:12) Lengo lake ni kugeuza watu wote watoke kwa Mungu wa kweli, Yehova. Ingawa huenda yeye akafaulu kugeuza wengi, Biblia yafunua kiunabii kwamba yeye atashindwa kuvunja ukamilifu wa watumishi wa kweli wa Mungu. Mwishowe, Shetani ataondolewa. Lakini je!, hata Shetani akiisha kuondoshwa, huo utakuwa ndio mwisho wa uhalifu? Na je! sasa mwisho wa uhalifu uko karibu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki