Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 6/15 kur. 30-31
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Jina la Mungu Laondolewa Lawama
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Malipo
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Wazia Ulimwengu Usio na Pupa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kwa Nini Nisiibe?
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 6/15 kur. 30-31

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Mashahidi wa Yehova huonaje ununuzi wa vitu vilivyoibwa?

Wakristo huepuka kuwa na sehemu yoyote katika kununua bidhaa au vifaa ambavyo wanajua vimeibwa.

Kuiba kwa kweli hakufai. Sheria ya Mungu kwa Israeli ilisema waziwazi: “Usiibe.” (Kutoka 20:15; Mambo ya Walawi 19:11) Ikiwa mwizi angekamatwa, angelazimika kulipia mara mbili, mara nne, au mara tano, ikitegemea hali.

Kuanzia nyakati za kale, wevi wamejaribu kuuza vitu vilivyoibwa ili wapate faida ya haraka na ili wasishikwe wakiwa na ushuhuda wa hatia yao. Ili wafanye hivyo, mara nyingi wao huuza vitu vilivyoibwa kwa bei ya chini ambayo wanunuzi wengi huona vigumu kukataa. Jambo kama hilo huenda likahusika kwa yale tunayosoma kwenye Kutoka 22:1: “Mtu akiiba ng’ombe au kondoo, na kumchinja, au kumwuza; atalipa ng’ombe watano badala ya ng’ombe mmoja, na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja.”

Akitambua kuwa mtu angekuwa na hatia kwa kukiuka sheria hizo, Rabi Abraham Chill aandika: “Kununua au kukubali mali iliyoibwa kunakatazwa, hata ikiwa mali hiyo haionwi kuwa imeibwa. Hivyo, mtu hapaswi kununua mbuzi kutoka kwa mchungaji, kwa sababu huenda mchungaji huyo anamwuza bila kumfahamisha mwajiri wake na anakusudia pesa hizo ziwe zake.”—The Mitzvot—The Commandments and Their Rationale.

Lakini kwa kweli, sheria ya Mungu haikatazi ‘kununua mbuzi kutoka kwa mchungaji’ eti tu kwa sababu ya kushuku kwamba huenda akajitwalia pesa za mwajiri wake, baada ya kuuza mbuzi aliyeibwa. Lakini kwa upande ule mwingine, watumishi wa Yehova hawapaswi kushiriki ununuzi (wa mbuzi au kitu kingine chochote) inapokuwa wazi kwamba kitu hicho si cha mwuzaji au kwamba huenda ikawa kimeibwa. Sheria ya Mungu huonyesha kwamba Yeye hutambua mali ya kibinafsi, lakini mwivi hutwaa mali ya wenyewe. Mtu anayenunua kile kinachojulikana kuwa kimeibwa huenda asiwe mwivi, lakini ununuzi wake unapunguza uwezekano wa mwenye kitu hicho kuweza kukipata tena kamwe.—Mithali 16:19; linganisha 1 Wathesalonike 4:6.

Sisi sote tunaelewa kwamba wanunuzi—wawe ni wake wa nyumbani au wajumbe wa makampuni—hutafuta kununua vitu kwa bei iliyo nafuu zaidi. Wanawake ulimwenguni pote hutafuta bei nzuri za ununuzi, hujaribu kuchelewesha ununuzi wao hadi kipindi ambacho bei ziko chini, au wananunua katika masoko au maduka makubwa yanayoendeshwa kwa gharama ndogo zaidi na hivyo bidhaa zayo huwa kwa bei nafuu zaidi. (Mithali 31:14) Na bado, kupendezwa huko kupata bei bora zaidi kwapaswa kuwa na mipaka ya kimaadili. Waaminifu-washikamanifu wa siku za Nehemia walikataa kufanya ununuzi siku ya Sabato, hata ingawa wangepata bei nafuu katika siku hizo. (Nehemia 10:31; linganisha Amosi 8:4-6.) Ni hali moja na Wakristo. Kukataa kwao kuiba huwasaidia kudhibiti shawishi lolote la kununua bidhaa zenye bei ya chini ambazo kwa wazi zimeibwa.

Huenda ikawa inafahamika kuwa wauzaji fulani huuza bidhaa zilizoibwa. Au bei inayotajwa kwa usirisiri huenda ikawa ya chini isivyo kawaida hivi kwamba mtu yeyote mwenye akili timamu angeweza kufanya mkataa kwamba vitu hivyo vinaelekea vilipatikana kwa njia isiyo halali. Hata sheria ya nchi huenda ikapendekeza uhitaji huo wa kutumia akili. Buku moja kuhusu maarifa ya sheria lasema:

“Si jambo la lazima kwa mshtakiwa kupata ufahamu wa hatia ya kwamba mali hiyo iliibwa nani au ni nani aliyeiiba, au ni lini au wapi ilipoibwa, au hali ambazo kwazo iliibwa, lakini inatosha kwamba ajua iliibwa. . . . Mahakama fulani huwa na maoni kwamba kuwapo kwa ufahamu wa hatia kwaweza kujulikana kwa jambo la kwamba mshtakiwa alipokea mali chini ya hali hizo ambazo zaweza kumridhisha mtu wa akili ya kawaida na mwenye kufikiri kwamba mali hiyo iliibwa.”

Hilo laongezea sababu ya akili kwa Mkristo kuepuka kununua vitu vilivyoibwa. Inaelekea kwamba kununua vitu kama hivyo kungeweza kumfanya awe mvunja-sheria. Watu wengi hawajali kuvunja sheria wanapofikiri kuwa wanaweza kuponyoka. Hilo si kweli kwa Wakristo, ambao wanataka ‘kutii mamlaka iliyo kuu.’ Kuwa kwao washika-sheria huwalinda wasishtakiwe kuwa wahalifu, na huchangia kuwa na dhamiri safi mbele za Yehova.—Warumi 13:1, 4, 5.

Rafiki ya Mungu Abrahamu aliweka mfano mzuri kuhusiana na dhamiri. Katika siku yake, watawala wanne wa mashariki waliwashinda wafalme wa mahali ambapo Loti aliishi, wakibeba mali nyingi zikiwa mali zilizoibwa kijeshi. Abrahamu, aliwafuatilia, akashinda adui, na kurudisha vitu vilivyoibwa. Mfalme wa Sodoma alimwambia Abrahamu: “Hizo mali uchukue wewe” kuwa zawadi. Badala yake, Abrahamu alipeleka mali hizo kwa mwenyeji wazo wa haki, akisema: “Sitatwaa . . . cho chote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu.”—Mwanzo 14:1-24.

Wakristo hawapendezwi na faida yoyote ya kifedha ambayo yaweza kupatikana kutokana na mali iliyoibwa. Yeremia aliandika: “Kama kware akusanyaye makinda asiyoyazaa, ndivyo alivyo mtu ajipatiaye mali, wala si kwa haki.” (Yeremia 17:11) Kwa hiyo, zaidi ya kuonyesha hekima kwa kutovunja sheria za Kaisari kuhusu mali iliyoibwa, Wakristo hutaka kuonyesha haki ya Mungu kwa kukataa kuhusika kwa vyovyote na ukosefu wa haki kwa kuiba. Daudi aliandika vema hivi: “Kidogo alicho nacho mwenye haki ni bora kuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi.”—Zaburi 37:16.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki