Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 8/98 uku. 1
  • Vijana—Tumieni kwa Manufaa Masomo Yenu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Vijana—Tumieni kwa Manufaa Masomo Yenu
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Watoto Wako Ni Tayari Kurudi Shuleni?
    Huduma Yetu ya Ufalme—1990
  • Je, Uko Tayari Kurudi Shuleni?
    Huduma ya Ufalme—2009
  • Pata Manufaa Zote za Shule
    Huduma Yetu ya Ufalme—1997
  • Shule Yenye Mafanikio Ambayo Ni ya Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—1998
km 8/98 uku. 1

Vijana—Tumieni kwa Manufaa Masomo Yenu

1 Mwahisije kurudi shuleni baada ya likizo ya shule? Je, mwatamani kunufaika na muhula mwingine wa masomo? Je, mtatumia kwa manufaa fursa ambazo shule huwa nazo ili mshiriki kweli pamoja na wanadarasa wenzenu na walimu? Tuna uhakika kwamba mwataka kufanya vema mwezavyo shuleni.

2 Uwe Mwanafunzi Mzuri: Ukijitayarisha vizuri unapofanya masomo yako na kukaza fikira kwa makini utapata manufaa zenye kudumu. Uwe mwenye bidii kuhusu kufanya masomo yako ya nyumbani, lakini usiruhusu kazi ya shule iingilie utendaji mbalimbali wa kitheokrasi.—Flp. 1:10.

3 Anza muhula mpya wa shule kwa kusoma broshua Mashahidi wa Yehova na Elimu. Kisha, wewe au wazazi wako mwapaswa kumpa nakala moja kila mmoja wa walimu wako. Wajulishe kwamba swali lolote ambalo huenda wakawa nalo litajibiwa. Hilo litawasaidia kuelewa kanuni zako na itikadi zako vizuri zaidi na kushirikiana nawe unapotumia yale uliyofunzwa. Pia itawahakikishia walimu wako kwamba wewe na wazazi wako mwataka kushirikiana nao wanapokusaidia kujipatia elimu yenye thamani.

4 Uwe Shahidi Mzuri: Kwa nini usifanye shule iwe eneo lako la kibinafsi la kutoa ushahidi wa vivi hivi? Wakati wa muhula ujao wa shule, utakuwa na fursa za pekee za kutoa ushahidi. Una ujuzi wa kiroho mzuri ajabu ambao unapoushiriki, waweza “[kujiokoa] wewe mwenyewe na wale wakusikilizao pia.” (1 Tim. 4:16) Kwa kudumisha mwenendo ufaao wa Kikristo na kwa kutoa ushahidi inapofaa kufanya hivyo, utajinufaisha mwenyewe na wengine.

5 Ndugu mmoja mchanga alitoa ushahidi wa vivi hivi kwa wanafunzi wenzake shuleni mwake. Miongoni mwa wale walioitikia vizuri alikuwa Mkatoliki, mtu asiyeamini kuwapo kwa Mungu aliyezoea kudhihaki wale ambao humwamini Mungu, na kijana ambaye alikuwa mvutaji wa sigareti kwa mfululizo na mnywaji wa kupindukia. Kwa ujumla, ndugu huyu mchanga alisaidia watu 15 wa rika lake wafikie wakfu na ubatizo!

6 Kwa hiyo vijana, endeleeni kujifunza na kuhubiri katika eneo lenu la pekee. Ndipo mtakapofurahia manufaa kubwa zaidi ya kwenda shuleni.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki