Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 8/09 uku. 2
  • Je, Uko Tayari Kurudi Shuleni?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Uko Tayari Kurudi Shuleni?
  • Huduma ya Ufalme—2009
  • Habari Zinazolingana
  • Umewatayarisha Watoto Wako?
    Huduma Yetu ya Ufalme—2011
  • Vijana—Tumieni kwa Manufaa Masomo Yenu
    Huduma Yetu ya Ufalme—1998
  • Je! Watoto Wako Ni Tayari Kurudi Shuleni?
    Huduma Yetu ya Ufalme—1990
  • Tunawafurahia Vijana Wanaotembea Katika Njia ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
Pata Habari Zaidi
Huduma ya Ufalme—2009
km 8/09 uku. 2

Je, Uko Tayari Kurudi Shuleni?

1. Utapata fursa gani utakaporudi shuleni?

1 Ninyi vijana wote Wakristo mnaorudi shuleni, mtakabili changamoto na matatizo mbalimbali. Lakini pia mtapata fursa za ‘kutoa ushahidi juu ya ile kweli.’ (Yoh. 18:37) Je, umejitayarisha vizuri kutoa ushahidi shuleni?

2. Umetayarishwa kurudi shuleni jinsi gani?

2 Ili ufanikiwe katika sehemu zote za maisha yako, umefundishwa vizuri na Yehova, wazazi wako, na mtumwa mwaminifu na mwenye busara. (Met. 1:8; 6:20; 23:23-25; Efe. 6:1-4; 2 Tim. 3:16, 17) Bila shaka, unajua ni changamoto gani ambazo utakabili shuleni. Umefundishwa mapenzi ya Mungu na unajua vizuri hali utakazokabili shuleni, basi, jitayarishe kutoa ushahidi. (Met. 22:3) Fikiria kwa uzito mwongozo na mapendekezo mazuri yanayopatana na Maandiko ambayo yanapatikana katika vitabu viwili vya Vijana Huuliza na vilevile katika makala za “Vijana Huuliza” katika Amkeni!

3. Unaweza kutoa ushahidi kwa njia gani?

3 Unaweza kutoa ushahidi kwa njia nyingi katika eneo lako shuleni. Watu wanapoona mavazi na mapambo yako mazuri, maksi zako, mwenendo na maongezi yako, heshima yako kwa wanadarasa wenzako na walimu wako, na wanapotambua kwamba una kusudi maishani, huenda baadhi yao wakakuuliza, “Kwa nini wewe ni tofauti sana?” (Mal. 3:18; Yoh. 15:19; 1 Tim. 2:9, 10) Huenda ukapata fursa ya kutoa ushahidi na kueleza imani yako. Yamkini utashinikizwa kushiriki katika sherehe za kizalendo au sikukuu mbalimbali. Iwapo utaulizwa kinachofanya usishiriki, je, utajibu tu, “Dini yangu inanikataza; mimi ni Shahidi wa Yehova,” au utachukua nafasi hiyo kutoa ushahidi juu ya Baba yako mwenye upendo, Yehova? Ukijitayarisha vizuri kwa kufuata mwongozo wa Yehova utaweza kuwahubiria walimu, wanafunzi wenzako, na wengineo.—1 Pet. 3:15.

4. Kwa nini una hakika kwamba unaweza kufanikiwa shuleni?

4 Huenda una wasiwasi kidogo kuhusu kurudi shuleni, lakini kumbuka kwamba kuna wengi walio tayari kukusaidia ili ufanikiwe. Isitoshe, tunashangilia pamoja nawe kwamba una fursa ya kuwahubiria wengine katika eneo lako shuleni. Kwa hiyo, uwe na moyo mkuu unaporudi shuleni!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki