2 Wathesalonike
2 Hata hivyo, akina ndugu, kwa habari ya kuwapo kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanywa kwetu pamoja kwake, twawaomba nyinyi 2 msiwe wenye kutikiswa upesi kutoka kwenye kufikiri kwenu wala kuwa wenye kusisimuliwa ama kupitia usemi uliopuliziwa au kupitia ujumbe wa maneno au kupitia barua kama kwamba ni kutoka kwetu, ya kuwa siku ya Yehova ipo hapa.
3 Msiache mtu yeyote awashawishi nyinyi katika namna yoyote, kwa sababu haitakuja isipokuwa uasi-imani uje kwanza na mtu wa uasi-sheria apate kufunuliwa, mwana wa uangamizo. 4 Yeye amewekwa katika upinzani na hujiinua mwenyewe juu ya kila aitwaye “mungu” au kitu cha kupewa ustahifu, hivi kwamba yeye huketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha mwenyewe hadharani kuwa mungu. 5 Je, hamkumbuki kwamba, nilipokuwa ningali pamoja nanyi, ilikuwa kawaida yangu kuwaambia nyinyi mambo haya?
6 Na kwa hiyo sasa mwajua kitu kitendacho kikiwa kizuizi, ili afunuliwe katika wakati wake mwenyewe upasao. 7 Kweli, fumbo la uasi-sheria huu tayari lafanya kazi; lakini hadi tu yeye anayetenda sasa hivi akiwa kizuizi apatapo kuondolewa njiani. 8 Ndipo, kwa kweli, mwasi-sheria atafunuliwa, ambaye Bwana Yesu atamwondolea mbali kwa roho ya kinywa chake na kufanya awe si kitu kwa udhihirisho wa kuwapo kwake. 9 Lakini kuwapo kwa huyo mwasi-sheria ni kulingana na utendaji wa Shetani pamoja na kila kazi yenye nguvu na ishara za uwongo na mambo ya ajabu 10 na pamoja na kila udanganyo usio wa uadilifu kwa wale wanaoangamia, yakiwa malipo kwa sababu hawakukubali upendo wa ile kweli ili wapate kuokolewa. 11 Kwa hiyo ndiyo sababu Mungu huacha utendaji wa kosa uwaendee wao, ili wapate kuuamini uwongo, 12 ili wote wapate kuhukumiwa kwa sababu hawakuamini kweli bali walipendezwa na ukosefu wa uadilifu.
13 Hata hivyo, sisi twawajibika kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, akina ndugu mliopendwa na Yehova, kwa sababu Mungu aliwateua nyinyi tangu mwanzo kwa ajili ya wokovu kwa kuwatakasa nyinyi kwa roho na kwa imani yenu katika kweli. 14 Kwa kusudio hilihili aliwaita nyinyi kupitia habari njema tuitangazayo, kwa kusudi la kujipatia utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. 15 Basi, kwa hiyo, akina ndugu, simameni imara na kudumisha mshiko wenu juu ya mapokeo mliyofundishwa, kwamba ilikuwa kupitia ujumbe wa maneno au kupitia barua yetu. 16 Zaidi ya hayo, Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu, aliyetupenda sisi na aliyetupa faraja idumuyo milele na tumaini jema kwa njia ya fadhili isiyostahiliwa na, 17 afariji mioyo yenu na kuwafanya nyinyi kuwa imara katika kila kitendo chema na neno jema.