Waebrania
9 Basi, kwa upande walo, agano la kwanza lilikuwa na kawaida ya kuwa na maagizo rasmi ya utumishi mtakatifu na mahali patakatifu palo pa kidunia. 2 Kwa maana palijengwa behewa la hema la kwanza ambalo katika hilo mlikuwa kile kinara cha taa na pia meza na wonyesho wa mikate; napo paitwa “Mahali Patakatifu.” 3 Lakini nyuma ya pazia la pili kulikuwa na behewa la hema lililoitwa “Patakatifu Zaidi Sana.” 4 Hili lilikuwa na chetezo cha dhahabu na sanduku la agano likiwa limetandazwa kuzunguka mahali pote kwa dhahabu, ambalo ndani yalo ulikuwamo mtungi wa dhahabu wenye mana na fimbo iliyochipuka ya Aroni na mabamba ya agano; 5 lakini juu juu lilikuwa na makerubi wenye utukufu wenye kukitia kivuli kile kifuniko cha kufunikia. Lakini sasa sio wakati wa kusema kirefu kuhusu vitu hivi.
6 Baada ya vitu hivi kuwa vimejengwa hivyo, makuhani huliingia behewa la hema la kwanza nyakati zote kufanya utumishi mbalimbali mtakatifu; 7 lakini ndani ya behewa la pili kuhani wa cheo cha juu peke yake huingia mara moja kwa mwaka, si bila damu, ambayo yeye hutoa kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya dhambi za watu za kutokuwa na ujuzi. 8 Hivyo roho takatifu hufanya iwe wazi kwamba njia ya kuingia ndani ya mahali patakatifu haikuwa bado imefanywa dhahiri wakati hema la kwanza lilipokuwa limesimama. 9 Hema hilihili ni kielezi kwa wakati uliowekwa ulio hapa sasa, na kwa kupatana nalo zawadi na dhabihu pia zatolewa. Hata hivyo, hizo haziwezi kufanya mtu anayefanya utumishi mtakatifu awe mkamilifu kwa habari ya dhamiri yake, 10 bali zahusu vyakula na vinywaji na mabatizo tu ya namna mbalimbali. Hayo yalikuwa matakwa ya kisheria yenye kuhusiana na mwili na yaliamriwa hadi wakati uliowekwa ili kunyoosha mambo.
11 Hata hivyo, Kristo alipokuja akiwa kuhani wa cheo cha juu wa mambo mema ambayo yamekuwa, kupitia hema kubwa zaidi na kamilifu zaidi ambalo halikufanywa kwa mikono, yaani, si la uumbaji huu, 12 aliingia, si kwa damu ya mbuzi na ya mafahali wachanga, sivyo, bali kwa damu yake mwenyewe, mara moja kwa wakati wote ndani ya mahali patakatifu na kupata ukombozi udumuo milele kwa ajili yetu. 13 Kwa maana ikiwa damu ya mbuzi na ya mafahali na majivu ya mtamba wa ng’ombe yaliyonyunyizwa juu ya wale ambao wametiwa unajisi hutakasa kufikia kadiri ya usafi wa mwili, 14 je, si zaidi sana damu ya Kristo, ambaye kupitia roho idumuyo milele alijitoa mwenyewe bila waa kwa Mungu, itasafisha dhamiri zetu kutoka kazi zilizokufa ili tupate kutoa utumishi mtakatifu kwa Mungu aliye hai?
15 Basi hiyo ndiyo sababu yeye ni mpatanishi wa agano jipya, ili, kwa sababu kifo kimetukia kwa ajili ya kuachiliwa kwao kwa njia ya fidia kutoka kwenye mikiuko-sheria chini ya agano la kwanza, wale ambao wameitwa wapate kuipokea ahadi ya urithi udumuo milele. 16 Kwa maana palipo na agano, kifo cha mfanya-agano binadamu chahitaji kuandaliwa. 17 Kwa maana agano ni halali juu ya kafara wafu, kwa kuwa halina nguvu wakati wowote mfanya-agano binadamu akiwa hai. 18 Kwa sababu hiyo wala agano la kwanza halikuanzishwa kisherehe bila damu. 19 Kwa maana wakati kila amri kulingana na Sheria ilipokuwa imesemwa na Musa kwa watu wote, yeye alichukua damu ya mafahali wachanga na ya mbuzi pamoja na maji na sufu nyekundu-nyangavu na hisopo na kunyunyizia kitabu chenyewe na watu wote, 20 akisema: “Hii ndiyo damu ya agano ambalo Mungu ameweka kuwa agizo juu yenu.” 21 Naye alinyunyizia hema na vyombo vyote vya utumishi wa watu wote hivyohivyo kwa damu. 22 Ndiyo, karibu vitu vyote husafishwa kwa damu kulingana na Sheria, na isipokuwa damu yamwagwa hakuna msamaha utukiao.
23 Kwa hiyo ilikuwa lazima kwamba viwakilishi vya uhalisi wa vitu vilivyo katika mbingu visafishwe kwa njia hizo, lakini vitu vilivyo vya kimbingu vyenyewe visafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko dhabihu za namna hiyo. 24 Kwa maana Kristo aliingia, si mahali patakatifu palipofanywa kwa mikono, ambapo ni nakala ya uhalisi, bali mbinguni kwenyewe, ili sasa aonekane mbele ya uso wa Mungu kwa ajili yetu. 25 Wala si ili ajitoe mwenyewe mara nyingi, kwa kweli kama vile kuhani wa cheo cha juu huingia katika mahali patakatifu kutoka mwaka hadi mwaka kwa damu isiyo yake mwenyewe. 26 Kama sivyo, ingembidi yeye kuteseka mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu. Lakini sasa amejidhihirisha mwenyewe mara moja kwa wakati wote kwenye umalizio wa mifumo ya mambo ili kuweka mbali dhambi kupitia dhabihu yake mwenyewe. 27 Na kama vile watu wamewekewa akiba kufa mara moja kwa wakati wote, lakini baada ya hilo hukumu, 28 ndivyo pia Kristo alivyotolewa mara moja kwa wakati wote ili kuchukua dhambi za wengi; na mara ya pili aonekanapo itakuwa bila dhambi na kwa wale wanaomtazamia kwa bidii itakuwa kwa ajili ya wokovu wao.