10 “‘Na mtu yeyote wa nyumba ya Israeli au mkaaji mgeni yeyote anayekaa akiwa mgeni katikati yenu atakayekula namna yoyote ya damu,+ nitauweka uso wangu dhidi ya nafsi+ hiyo inayokula damu, nami hakika nitamkatilia mbali kutoka katikati ya watu wake.