-
Kumbukumbu la Torati 28:53-57Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
53 Ndipo mtakapolazimika kuwala watoto wenu* wenyewe, nyama ya wana wenu na mabinti wenu+ ambao Yehova Mungu wenu amewapa, kwa sababu ya kuzingirwa kabisa na kwa sababu ya mateso yatakayosababishwa na adui yenu.
54 “Hata mwanamume mpole sana na aliyedekezwa miongoni mwenu hatamhurumia ndugu yake au mke wake mpendwa au wanawe wanaobaki, 55 naye hatawagawia hata kidogo nyama ya wanawe ambayo atakula, kwa sababu hana kitu kingine chochote cha kula kwa sababu ya kuzingirwa kabisa na kwa sababu ya mateso yatakayosababishwa na adui yenu katika majiji yenu.+ 56 Na mwanamke mpole sana na aliyedekezwa miongoni mwenu ambaye hata hawezi kuthubutu kukanyaga chini kwa wayo wa mguu wake kwa sababu ya kudekezwa sana+ hatamhurumia mume wake mpendwa wala mwanawe wala binti yake, 57 wala hata kondo la nyuma linalotoka katikati ya miguu yake wala wana anaozaa, kwa sababu atawala kwa siri kwa sababu ya kuzingirwa kabisa na kwa sababu ya mateso yatakayosababishwa na adui yenu katika majiji yenu.
-
-
2 Wafalme 25:3-7Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
3 Katika siku ya tisa ya mwezi wa nne njaa ilikuwa kali sana+ jijini, na watu waliokuwemo hawakuwa na chakula.+ 4 Sehemu ya ukuta wa jiji ilibomolewa,+ na wanajeshi wote wakakimbia wakati wa usiku kupitia lango lililokuwa kati ya kuta mbili karibu na bustani ya mfalme, wakati Wakaldayo walipokuwa wakilizingira jiji; naye mfalme akafuata njia inayoelekea Araba.+ 5 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia mfalme, nalo likamfikia katika jangwa tambarare la Yeriko, na wanajeshi wake wote wakatawanyika na kumwacha. 6 Kisha wakamkamata mfalme+ na kumpeleka mpaka kwa mfalme wa Babiloni kule Ribla, nao wakamhukumu. 7 Wakawachinja wana wa Sedekia huku akitazama; kisha Nebukadneza akampofusha macho Sedekia, akamfunga kwa pingu za shaba, na kumpeleka Babiloni.+
-