Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 14:15-21
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 15 Lakini ilipofika jioni, wanafunzi wake wakaja na kumwambia: “Mahali hapa hapana watu na muda umesonga sana; uambie umati uondoke, waende vijijini wakajinunulie chakula.”+ 16 Hata hivyo, Yesu akawaambia: “Si lazima waondoke; ninyi wapeni chakula.” 17 Wakamwambia: “Hatuna kitu hapa isipokuwa mikate mitano na samaki wawili tu.” 18 Akasema: “Nileteeni hapa.” 19 Akauagiza umati uketi kwenye nyasi. Kisha akachukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akatoa baraka+ na baada ya kuimega mikate, akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakaugawia umati. 20 Basi wote wakala wakashiba, nao wakakusanya vipande vilivyobaki, wakajaza vikapu 12.+ 21 Sasa wale waliokula walikuwa wanaume karibu 5,000, na pia wanawake na watoto wadogo.+

  • Luka 9:12-17
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 12 Ilipokaribia jioni, wale 12 wakaja na kumwambia Yesu: “Uambie umati uondoke, waende vijijini na mashambani ili wakatafute chakula na mahali pa kulala, kwa sababu mahali hapa hapana watu.”+ 13 Lakini akawaambia: “Ninyi wapeni chakula.”+ Wakasema: “Tuna mikate mitano tu na samaki wawili, labda twende tukawanunulie watu hawa wote chakula.” 14 Kwa kweli, kulikuwa na karibu wanaume 5,000. Lakini akawaambia wanafunzi wake: “Waambieni waketi katika vikundi vya watu hamsini hamsini.” 15 Wakafanya hivyo, na kila mtu akaketi. 16 Akachukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni na kuvibariki. Kisha akavimega, akaanza kuwapa wanafunzi ili wawape watu. 17 Basi wote wakala wakashiba, nao wakakusanya chakula kilichobaki na kujaza vikapu 12.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki