Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 12:9-14
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 9 Baada ya kutoka hapo, akaingia ndani ya sinagogi lao, 10 na tazama! kulikuwa na mtu aliyepooza mkono!+ Basi, ili wapate sababu ya kumshtaki wakamuuliza, “Je, ni halali kumponya mtu siku ya Sabato?”+ 11 Akawaambia: “Ukiwa na kondoo mmoja, naye kondoo huyo atumbukie shimoni siku ya Sabato, je, kuna yeyote kati yenu ambaye hatamshika na kumtoa humo?+ 12 Kwa kweli, mwanadamu ni mwenye thamani sana kuliko kondoo! Basi ni halali kutenda mema siku ya Sabato.” 13 Kisha akamwambia mtu huyo: “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukawa mzima kama ule mkono mwingine. 14 Lakini Mafarisayo wakaenda nje na kupanga njama ili wamuue.

  • Luka 6:6-11
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 6 Siku nyingine ya Sabato+ aliingia katika sinagogi, akaanza kufundisha. Kulikuwa na mtu aliyepooza mkono wa kulia.+ 7 Waandishi na Mafarisayo walikuwa wakimwangalia Yesu kwa makini ili waone kama angeponya katika siku ya Sabato, ili wapate sababu ya kumshtaki. 8 Hata hivyo, alijua mawazo yao,+ basi akamwambia yule mtu aliyepooza mkono: “Inuka usimame hapa katikati.” Naye akainuka na kusimama hapo. 9 Kisha Yesu akawauliza: “Je, ni halali kufanya mema au kufanya mabaya siku ya Sabato, kuokoa uhai* au kuuangamiza?”+ 10 Baada ya kuwatazama wote waliokuwapo, Yesu akamwambia mtu huyo: “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukapona. 11 Lakini wakakasirika sana, wakaanza kushauriana kuhusu jambo ambalo wangemtendea Yesu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki