Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 18:1-5
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 18 Katika saa hiyo wanafunzi wakamkaribia Yesu na kumuuliza: “Kwa kweli ni nani aliye mkuu zaidi katika Ufalme wa mbinguni?”+ 2 Basi akamwita mtoto mdogo, akamsimamisha katikati yao 3 na kusema: “Kwa kweli ninawaambia, msipogeuka* na kuwa kama watoto wadogo,+ hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.+ 4 Kwa hiyo, yeyote atakayejinyenyekeza kama mtoto huyu mdogo ndiye mkuu zaidi katika Ufalme wa mbinguni;+ 5 na yeyote anayempokea mtoto mdogo kama huyu kwa msingi wa jina langu ananipokea mimi pia.

  • Marko 9:33-37
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 33 Nao wakaingia Kapernaumu. Alipokuwa ndani ya nyumba akawauliza: “Mlikuwa mkibishania nini barabarani?”+ 34 Wakakaa kimya, kwa maana barabarani walikuwa wakibishana kuhusu aliye mkuu kati yao. 35 Basi akaketi na kuwaita wale 12 akawaambia: “Yeyote anayetaka kuwa wa kwanza, lazima awe wa mwisho kati ya wote na mhudumu wa wote.”+ 36 Kisha akamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha katikati yao; akamkumbatia na kuwaambia: 37 “Yeyote anayempokea mtoto mdogo+ kama huyu kwa msingi wa jina langu ananipokea mimi pia; na yeyote anayenipokea mimi hanipokei mimi tu, bali pia Yule aliyenituma.”+

  • Luka 22:24
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 24 Hata hivyo, pia kukatokea bishano kali kuhusu ni nani aliyekuwa mkuu zaidi kati yao.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki