Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kumbukumbu la Torati 11
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Kumbukumbu la Torati—Yaliyomo

      • Mmeuona ukuu wa Yehova (1-7)

      • Nchi Iliyoahidiwa (8-12)

      • Thawabu za kutii (13-17)

      • Maneno ya Mungu yakaziwe katika mioyo (18-25)

      • “Baraka na laana” (26-32)

Kumbukumbu la Torati 11:1

Marejeo

  • +Kum 6:5; 10:12; Mk 12:30

Kumbukumbu la Torati 11:2

Marejeo

  • +Kum 8:5; Ebr 12:6
  • +Kum 5:24; 9:26
  • +Kut 13:3

Kumbukumbu la Torati 11:3

Marejeo

  • +Kum 4:34

Kumbukumbu la Torati 11:4

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “mpaka leo.”

Marejeo

  • +Kut 14:23, 28; Ebr 11:29

Kumbukumbu la Torati 11:6

Marejeo

  • +Hes 16:1, 32

Kumbukumbu la Torati 11:9

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “mbegu yao.”

Marejeo

  • +Kum 4:40; Met 3:1, 2
  • +Mwa 13:14, 15; 26:3; 28:13
  • +Kut 3:8; Eze 20:6

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    8/1/2007, uku. 29

  • Fahirishi ya Machapisho

    w07 8/1 29

Kumbukumbu la Torati 11:10

Maelezo ya Chini

  • *

    Yaani, kwa kutumia mfumo fulani uliokanyagwa kwa mguu, labda mfumo unaotumia gurudumu la maji au kwa kuchimba na kufungua mitaro ya maji kwa miguu.

Kumbukumbu la Torati 11:11

Marejeo

  • +Kum 1:7
  • +Kum 8:7

Kumbukumbu la Torati 11:12

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    8/1/2007, uku. 29

  • Fahirishi ya Machapisho

    w07 8/1 29

Kumbukumbu la Torati 11:13

Maelezo ya Chini

  • *

    Angalia Kamusi.

Marejeo

  • +Kum 4:29; 6:5; 10:12; Mt 22:37

Kumbukumbu la Torati 11:14

Maelezo ya Chini

  • *

    Yaani, Mungu.

Marejeo

  • +Law 26:4; Kum 8:7-9; 28:12; Yer 14:22

Kumbukumbu la Torati 11:15

Marejeo

  • +Kum 8:10

Kumbukumbu la Torati 11:16

Marejeo

  • +Kum 8:19; 29:18; Ebr 3:12

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    6/2019, kur. 3-4

Kumbukumbu la Torati 11:17

Marejeo

  • +Kum 28:15, 23; 1Fa 8:35, 36; 2Nya 7:13, 14
  • +Kum 8:19

Kumbukumbu la Torati 11:18

Maelezo ya Chini

  • *

    Angalia Kamusi.

  • *

    Tnn., “katikati ya macho yako.”

Marejeo

  • +Met 7:1-3

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Upeo wa Ufunuo, uku. 197

    Mnara wa Mlinzi,

    6/1/1998, uku. 20

    Furaha ya Familia, kur. 70-71

  • Fahirishi ya Machapisho

    re 197; w98 6/1 20; fy 70-71

Kumbukumbu la Torati 11:19

Marejeo

  • +Kum 6:6-9; Met 22:6; Efe 6:4

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi (Funzo),

    3/2023, kur. 21-23

    Furaha ya Familia, kur. 70-71

    Mnara wa Mlinzi,

    5/1/1995, uku. 10

    Kuishi Milele, uku. 245

  • Fahirishi ya Machapisho

    fy 70-71

Kumbukumbu la Torati 11:21

Marejeo

  • +Kum 4:40; Met 4:10
  • +Mwa 13:14, 15

Kumbukumbu la Torati 11:22

Marejeo

  • +Kum 6:5; Lu 10:27
  • +Kum 10:20; 13:4; Yos 22:5

Kumbukumbu la Torati 11:23

Marejeo

  • +Kut 23:28; Yos 3:10
  • +Kum 7:1; 9:1, 5

Kumbukumbu la Torati 11:24

Maelezo ya Chini

  • *

    Yaani, ile Bahari Kuu, Mediterania.

Marejeo

  • +Yos 14:9
  • +Mwa 15:18; Kut 23:31

Kumbukumbu la Torati 11:25

Marejeo

  • +Kum 7:24; Yos 1:5
  • +Kut 23:27; Yos 2:9, 10; 5:1

Kumbukumbu la Torati 11:26

Marejeo

  • +Kum 30:15

Kumbukumbu la Torati 11:27

Marejeo

  • +Kum 28:1, 2; Zb 19:8, 11

Kumbukumbu la Torati 11:28

Marejeo

  • +Law 26:15, 16; Isa 1:20

Kumbukumbu la Torati 11:29

Marejeo

  • +Kum 27:12, 13; Yos 8:33, 34

Kumbukumbu la Torati 11:30

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “machweo ya jua.”

Marejeo

  • +Mwa 12:6

Kumbukumbu la Torati 11:31

Marejeo

  • +Yos 1:11

Kumbukumbu la Torati 11:32

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “maamuzi yote ya hukumu ninayoweka.”

Marejeo

  • +Kum 5:32; 12:32

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

Kum. 11:1Kum 6:5; 10:12; Mk 12:30
Kum. 11:2Kum 8:5; Ebr 12:6
Kum. 11:2Kum 5:24; 9:26
Kum. 11:2Kut 13:3
Kum. 11:3Kum 4:34
Kum. 11:4Kut 14:23, 28; Ebr 11:29
Kum. 11:6Hes 16:1, 32
Kum. 11:9Kum 4:40; Met 3:1, 2
Kum. 11:9Mwa 13:14, 15; 26:3; 28:13
Kum. 11:9Kut 3:8; Eze 20:6
Kum. 11:11Kum 1:7
Kum. 11:11Kum 8:7
Kum. 11:13Kum 4:29; 6:5; 10:12; Mt 22:37
Kum. 11:14Law 26:4; Kum 8:7-9; 28:12; Yer 14:22
Kum. 11:15Kum 8:10
Kum. 11:16Kum 8:19; 29:18; Ebr 3:12
Kum. 11:17Kum 28:15, 23; 1Fa 8:35, 36; 2Nya 7:13, 14
Kum. 11:17Kum 8:19
Kum. 11:18Met 7:1-3
Kum. 11:19Kum 6:6-9; Met 22:6; Efe 6:4
Kum. 11:21Kum 4:40; Met 4:10
Kum. 11:21Mwa 13:14, 15
Kum. 11:22Kum 6:5; Lu 10:27
Kum. 11:22Kum 10:20; 13:4; Yos 22:5
Kum. 11:23Kut 23:28; Yos 3:10
Kum. 11:23Kum 7:1; 9:1, 5
Kum. 11:24Yos 14:9
Kum. 11:24Mwa 15:18; Kut 23:31
Kum. 11:25Kum 7:24; Yos 1:5
Kum. 11:25Kut 23:27; Yos 2:9, 10; 5:1
Kum. 11:26Kum 30:15
Kum. 11:27Kum 28:1, 2; Zb 19:8, 11
Kum. 11:28Law 26:15, 16; Isa 1:20
Kum. 11:29Kum 27:12, 13; Yos 8:33, 34
Kum. 11:30Mwa 12:6
Kum. 11:31Yos 1:11
Kum. 11:32Kum 5:32; 12:32
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
  • 27
  • 28
  • 29
  • 30
  • 31
  • 32
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
Kumbukumbu la Torati 11:1-32

Kumbukumbu la Torati

11 “Ni lazima mumpende Yehova Mungu wenu+ na kutimiza sikuzote wajibu wenu kwake, sheria zake, maagizo yake, na amri zake. 2 Mnajua kwamba leo ninazungumza nanyi, si na wana wenu ambao hawajajua wala kuona nidhamu ya Yehova Mungu wenu,+ ukuu wake,+ mkono wake wenye nguvu+ na mkono wake ulionyooshwa. 3 Hawakuona ishara zake na matendo yake aliyotenda Misri kwa Farao mfalme wa Misri na kwa nchi yake yote;+ 4 wala mambo aliyoyatendea majeshi ya Misri, farasi wa Farao na magari yake ya vita, ambayo yalifunikwa na maji ya Bahari Nyekundu walipokuwa wakiwafuatia ninyi, na Yehova akawaangamiza milele.*+ 5 Hawakuona mambo aliyowatendea nyikani mpaka mlipofika mahali hapa, 6 wala mambo aliyowatendea Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu mwana wa Rubeni, dunia ilipofunguka na kuwameza wao pamoja na familia zao na mahema yao na kila kiumbe aliye hai aliyewafuata, mbele ya macho ya Waisraeli wote.+ 7 Macho yenu wenyewe yameona matendo yote makuu ambayo Yehova alifanya.

8 “Ni lazima mshike amri yote ninayowapa leo, ili muwe imara na kuvuka ili kuimiliki nchi, 9 na ili mwishi muda mrefu+ katika nchi ambayo Yehova aliapa kwamba angewapa mababu zenu na uzao wao,*+ nchi inayotiririka maziwa na asali.+

10 “Nchi mnayoenda kumiliki si kama nchi ya Misri mlikotoka, ambako mlikuwa mkipanda mbegu zenu na kuzimwagilia maji kwa mguu wenu,* kama bustani ya mboga. 11 Lakini nchi mnayokaribia kuvuka kuingia humo ili kuimiliki ni nchi yenye milima na mabonde tambarare.+ Inanyweshwa na maji ya mvua kutoka mbinguni;+ 12 ni nchi inayotunzwa na Yehova Mungu wenu. Macho ya Yehova Mungu wenu yanaitazama daima, kuanzia mwanzo wa mwaka mpaka mwisho wa mwaka.

13 “Na ikiwa mtatii kwa bidii amri zangu ninazowaamuru leo na kumpenda Yehova Mungu wenu na kumtumikia kwa moyo wenu wote na kwa nafsi* yenu yote,+ 14 nitawapa* pia mvua kwa ajili ya nchi yenu katika majira yake, mvua ya vuli na mvua ya masika, nanyi mtakusanya nafaka yenu na divai yenu mpya na mafuta yenu.+ 15 Nami nitaotesha majani katika mashamba yenu kwa ajili ya mifugo yenu, nanyi mtakula na kushiba.+ 16 Jihadharini msiruhusu mioyo yenu ishawishiwe kukengeuka na kuabudu miungu mingine na kuiinamia.+ 17 Kama sivyo, hasira ya Yehova itawaka dhidi yenu, naye atafunga mbingu hivi kwamba mvua haitanyesha+ na ardhi haitazaa mazao yake nanyi mtaangamia upesi kutoka katika nchi nzuri ambayo Yehova anawapa ninyi.+

18 “Ni lazima uyakazie maneno haya yangu katika moyo wako na nafsi* yako na kuyafunga kama kumbukumbu kwenye mkono wako, nayo yanapaswa kuwa kama utepe kwenye paji la uso wako.*+ 19 Wafundishe watoto wako maneno haya, na kuongea kuyahusu unapoketi nyumbani mwako na unapotembea barabarani na unapolala na unapoamka.+ 20 Yaandike kwenye miimo ya milango ya nyumba yako na kwenye malango yako, 21 ili wewe na wana wako mwishi muda mrefu+ katika nchi ambayo Yehova aliapa kwamba angewapa mababu zenu,+ sikuzote ambazo mbingu zitakuwa juu ya dunia.

22 “Ikiwa mtaishika kabisa amri hii ninayowapa na kuitekeleza, mkimpenda Yehova Mungu wenu,+ mkitembea katika njia zake zote na kushikamana naye,+ 23 Yehova atayafukuza mataifa haya yote kutoka mbele yenu,+ nanyi mtamiliki nchi ya mataifa makubwa zaidi na yenye watu wengi kuliko ninyi.+ 24 Kila mahali mtakapokanyaga kwa mguu wenu patakuwa penu.+ Mpaka wenu utaanzia nyikani mpaka Lebanoni, kuanzia ule Mto, mto Efrati, mpaka bahari ya magharibi.*+ 25 Hakuna yeyote atakayewazuia.+ Yehova Mungu wenu atawafanya wakaaji wote wa nchi mtakayokanyaga wawahofu na kuwaogopa,+ kama alivyowaahidi ninyi.

26 “Tazameni, leo ninaweka mbele yenu baraka na laana:+ 27 baraka, ikiwa mtatii amri za Yehova Mungu wenu ninazowaamuru ninyi leo,+ 28 na laana, ikiwa hamtatii amri za Yehova Mungu wenu+ na mkigeuka kutoka katika njia ninayowaamuru mfuate leo na mkifuata miungu mingine ambayo hamjaijua.

29 “Yehova Mungu wenu atakapowaleta katika nchi ambayo mtaimiliki, ni lazima mtangaze baraka kwenye Mlima Gerizimu na laana kwenye Mlima Ebali.+ 30 Je, haiko ng’ambo ya Yordani upande wa magharibi,* katika nchi ya Wakanaani wanaoishi Araba, mbele ya Gilgali, kando ya ile miti mikubwa ya More?+ 31 Kwa maana mnavuka Yordani mwingie na kuimiliki nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa ninyi.+ Mtakapoimiliki na kuishi humo, 32 ni lazima muwe waangalifu kutekeleza masharti na sheria zote ninazoweka* mbele yenu leo.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki