Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Samweli 11
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

1 Samweli—Yaliyomo

      • Sauli awashinda Waamoni (1-11)

      • Sauli atangazwa tena kuwa mfalme (12-15)

1 Samweli 11:1

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “makubaliano.”

Marejeo

  • +Kum 2:19
  • +Amu 21:8; 1Sa 31:11, 12

1 Samweli 11:2

Fahirisi Mbalimbali

  • Mwongozo wa Utafiti

    Mnara wa Mlinzi,

    12/15/1995, kur. 9-10

1 Samweli 11:4

Marejeo

  • +1Sa 10:26; 14:2

1 Samweli 11:6

Marejeo

  • +Amu 3:9, 10; 6:34; 11:29; 14:5, 6; 1Sa 10:10, 11; 16:13

1 Samweli 11:7

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “kama mtu mmoja.”

1 Samweli 11:10

Marejeo

  • +1Sa 11:3

1 Samweli 11:11

Maelezo ya Chini

  • *

    Yaani, kuanzia saa 8 hivi usiku hadi saa 12 asubuhi.

Marejeo

  • +1Sa 11:1

1 Samweli 11:12

Marejeo

  • +1Sa 10:26, 27

1 Samweli 11:13

Marejeo

  • +2Sa 19:22

1 Samweli 11:14

Marejeo

  • +1Sa 7:15, 16
  • +1Sa 10:17, 24

1 Samweli 11:15

Marejeo

  • +Law 7:11
  • +1Fa 1:39, 40; 2Fa 11:12, 14; 1Nya 12:39, 40

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

1 Sam. 11:1Kum 2:19
1 Sam. 11:1Amu 21:8; 1Sa 31:11, 12
1 Sam. 11:41Sa 10:26; 14:2
1 Sam. 11:6Amu 3:9, 10; 6:34; 11:29; 14:5, 6; 1Sa 10:10, 11; 16:13
1 Sam. 11:101Sa 11:3
1 Sam. 11:111Sa 11:1
1 Sam. 11:121Sa 10:26, 27
1 Sam. 11:132Sa 19:22
1 Sam. 11:141Sa 7:15, 16
1 Sam. 11:141Sa 10:17, 24
1 Sam. 11:15Law 7:11
1 Sam. 11:151Fa 1:39, 40; 2Fa 11:12, 14; 1Nya 12:39, 40
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
1 Samweli 11:1-15

Kitabu cha Kwanza cha Samweli

11 Nahashi Mwamoni+ akapanda na kupiga kambi ili kushambulia Yabeshi+ kule Gileadi. Watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi: “Fanya agano* pamoja nasi, nasi tutakutumikia.” 2 Nahashi Mwamoni akawaambia: “Nitafanya agano pamoja nanyi kwa sharti hili: macho yenu yote ya kulia yang’olewe. Nitafanya hivyo ili kuwaaibisha Waisraeli wote.” 3 Wazee wa Yabeshi wakamwambia: “Tupe muda wa siku saba ili tuwatume wajumbe katika eneo lote la Israeli. Na ikiwa hakuna yeyote wa kutuokoa, tutajisalimisha kwako.” 4 Baada ya muda, wajumbe hao wakafika katika jiji la Gibea+ la Sauli na kuwaambia watu wote maneno hayo, na watu wote wakalia kwa sauti kubwa sana.

5 Lakini Sauli alikuwa akitoka shambani akiwa nyuma ya mifugo yake, naye akauliza: “Watu wana shida gani? Kwa nini wanalia?” Basi wakamwambia maneno yaliyosemwa na watu wa Yabeshi. 6 Roho ya Mungu ikamtia nguvu Sauli+ alipoyasikia maneno hayo, akawaka hasira. 7 Kwa hiyo akachukua ng’ombe dume wawili, akawakata vipandevipande, akawatuma wajumbe wavipeleke katika eneo lote la Israeli wakisema: “Mtu yeyote ambaye hamfuati Sauli na Samweli ajue kwamba ng’ombe wake watafanyiwa hivi!” Na watu wakashikwa na hofu ya Yehova hivi kwamba wakatoka wote pamoja.* 8 Kisha akawahesabu kule Bezeki, Waisraeli walikuwa 300,000 na watu wa Yuda walikuwa 30,000. 9 Kwa hiyo wakawaambia wajumbe waliokuwa wamekuja: “Hivi ndivyo mnavyopaswa kuwaambia watu wa Yabeshi kule Gileadi, ‘Kesho wakati wa jua kali mtaokolewa.’” Basi wale wajumbe wakaja na kuwaambia watu wa Yabeshi, nao wakashangilia sana. 10 Ndipo watu wa Yabeshi wakasema: “Kesho tutajisalimisha kwenu, nanyi mtatutendea mpendavyo.”+

11 Siku iliyofuata, Sauli aliwagawa watu katika vikosi vitatu, nao wakaingia katikati ya kambi wakati wa kesha la alfajiri* na kuwaua Waamoni+ mpaka jua lilipokuwa kali. Watu waliookoka walitawanywa hivi kwamba hakuna watu wawili waliobaki pamoja. 12 Kisha watu wakamwambia Samweli: “Ni nani waliokuwa wakiuliza, ‘Je, Sauli atakuwa mfalme wetu?’+ Waleteni watu hao ili tuwaue.” 13 Hata hivyo, Sauli akasema: “Hakuna mtu yeyote anayepaswa kuuawa leo,+ kwa maana leo Yehova amewaokoa Waisraeli.”

14 Baadaye Samweli akawaambia watu: “Njooni twende Gilgali+ tukamtangaze tena mfalme.”+ 15 Basi watu wote wakaenda Gilgali, na huko Gilgali wakamweka Sauli kuwa mfalme mbele za Yehova. Kisha wakatoa huko dhabihu za ushirika mbele za Yehova,+ na Sauli na watu wote wa Israeli wakasherehekea kwa shangwe kubwa.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki