Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Samweli 10
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

2 Samweli—Yaliyomo

      • Awashinda Waamoni na Wasiria (1-19)

2 Samweli 10:1

Marejeo

  • +Mwa 19:36, 38; Amu 10:7; 11:12, 33; 1Sa 11:1
  • +1Nya 19:1-5

2 Samweli 10:4

Marejeo

  • +Law 19:27

2 Samweli 10:5

Marejeo

  • +Yos 18:21

2 Samweli 10:6

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “wanaume wa Tobu.”

Marejeo

  • +Hes 13:21
  • +2Sa 8:5
  • +Yos 13:13
  • +1Nya 19:6, 7

2 Samweli 10:7

Marejeo

  • +2Sa 23:8; 1Nya 19:8, 9

2 Samweli 10:8

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “wanaume wa Tobu.”

2 Samweli 10:9

Marejeo

  • +1Nya 19:10-13

2 Samweli 10:10

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “mikononi mwa.”

Marejeo

  • +1Sa 26:6; 2Sa 2:18; 23:18; 1Nya 2:15, 16
  • +Hes 21:24

2 Samweli 10:12

Marejeo

  • +Kum 31:6
  • +Zb 37:5; 44:5; Met 29:25

2 Samweli 10:13

Marejeo

  • +1Nya 19:14, 15

2 Samweli 10:15

Marejeo

  • +1Nya 19:16

2 Samweli 10:16

Marejeo

  • +2Sa 8:3-5
  • +Mwa 15:18; Kut 23:31

2 Samweli 10:17

Marejeo

  • +1Nya 19:17-19

2 Samweli 10:18

Marejeo

  • +Kum 20:1; Zb 18:37, 38

2 Samweli 10:19

Marejeo

  • +Mwa 15:18; Kum 20:10, 11

Tafsiri Mbalimbali

Bofya nambari ya mstari ili kuona mstari huo katika tafsiri mbalimbali za Biblia.

Jumla

2 Sam. 10:1Mwa 19:36, 38; Amu 10:7; 11:12, 33; 1Sa 11:1
2 Sam. 10:11Nya 19:1-5
2 Sam. 10:4Law 19:27
2 Sam. 10:5Yos 18:21
2 Sam. 10:6Hes 13:21
2 Sam. 10:62Sa 8:5
2 Sam. 10:6Yos 13:13
2 Sam. 10:61Nya 19:6, 7
2 Sam. 10:72Sa 23:8; 1Nya 19:8, 9
2 Sam. 10:91Nya 19:10-13
2 Sam. 10:101Sa 26:6; 2Sa 2:18; 23:18; 1Nya 2:15, 16
2 Sam. 10:10Hes 21:24
2 Sam. 10:12Kum 31:6
2 Sam. 10:12Zb 37:5; 44:5; Met 29:25
2 Sam. 10:131Nya 19:14, 15
2 Sam. 10:151Nya 19:16
2 Sam. 10:162Sa 8:3-5
2 Sam. 10:16Mwa 15:18; Kut 23:31
2 Sam. 10:171Nya 19:17-19
2 Sam. 10:18Kum 20:1; Zb 18:37, 38
2 Sam. 10:19Mwa 15:18; Kum 20:10, 11
  • Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • Soma katika Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
2 Samweli 10:1-19

Kitabu cha Pili cha Samweli

10 Baadaye mfalme wa Waamoni+ akafa, na Hanuni mwanawe akawa mfalme baada yake.+ 2 Ndipo Daudi akasema: “Nitamtendea kwa upendo mshikamanifu Hanuni mwana wa Nahashi kama baba yake alivyonitendea kwa upendo mshikamanifu.” Basi Daudi akawatuma watumishi wake ili wamfariji baada ya kufiwa na baba yake. Lakini watumishi wa Daudi walipofika katika nchi ya Waamoni, 3 wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni bwana wao: “Je, unafikiri kwamba Daudi anawatuma wafariji kwako ili kumheshimu baba yako? Je, Daudi hajawatuma watumishi wake ili kulichunguza jiji lote na kulipeleleza na kuliteka?” 4 Kwa hiyo Hanuni akawachukua watumishi wa Daudi, akawanyoa nusu ya ndevu zao,+ akakata nguo zao katikati kwenye matako na kuwafukuza. 5 Daudi alipoambiwa habari hiyo, mara moja akawatuma wanaume fulani waende kukutana nao, kwa sababu watumishi hao walikuwa wameaibishwa sana; mfalme akawaambia: “Kaeni Yeriko+ mpaka ndevu zenu zitakapoota, kisha mrudi.”

6 Baada ya muda Waamoni wakaona kuwa wananuka mbele ya Daudi, kwa hiyo wakawatuma wajumbe waende kuwakodi Wasiria wa Beth-rehobu + na Wasiria wa Soba,+ wanajeshi 20,000 wanaotembea kwa miguu; na mfalme wa Maaka+ akiwa na wanaume 1,000; na kutoka Ishtobu,* wanaume 12,000.+ 7 Daudi aliposikia habari hizo, akamtuma Yoabu na jeshi lote, kutia ndani mashujaa wake hodari zaidi.+ 8 Nao Waamoni wakatoka na kujipanga kivita kwenye lango la jiji huku Wasiria wa Soba na wa Rehobu, pamoja na Ishtobu* na Maaka, wakiwa peke yao uwanjani.

9 Yoabu alipoona kwamba anashambuliwa upande wa mbele na wa nyuma, akachagua baadhi ya wanajeshi bora katika Israeli na kuwapanga kivita ili wapigane na Wasiria.+ 10 Wanaume waliobaki aliwaweka chini ya usimamizi wa* Abishai ndugu yake,+ ili awapange kivita kupigana na Waamoni.+ 11 Kisha akasema: “Ikiwa Wasiria watanizidi nguvu, basi mtaniokoa; lakini Waamoni wakiwazidi ninyi nguvu, nitawaokoa. 12 Ni lazima tuwe imara na jasiri+ kwa ajili ya watu wetu na kwa ajili ya majiji ya Mungu wetu, naye Yehova atafanya yaliyo mema machoni pake.”+

13 Kisha Yoabu na wanaume wake wakasonga mbele kwenda kupigana vita na Wasiria, nao wakamkimbia.+ 14 Waamoni walipoona kwamba Wasiria wamekimbia, wakamkimbia Abishai na kuingia jijini. Baada ya Yoabu kupigana na Waamoni akarudi Yerusalemu.

15 Wasiria walipoona kwamba wameshindwa na Waisraeli, wakajikusanya tena.+ 16 Basi Hadadezeri+ akaagiza Wasiria kutoka katika eneo la Mto Efrati+ waletwe, nao wakaja Helamu, wakiongozwa na Shobaki mkuu wa jeshi la Hadadezeri.

17 Daudi alipoambiwa habari hiyo, akawakusanya mara moja Waisraeli wote, wakavuka Yordani na kufika Helamu. Kisha Wasiria wakajipanga kivita ili kwenda kupigana na Daudi.+ 18 Lakini Wasiria wakawakimbia Waisraeli; na Daudi akawaua Wasiria 700 wanaoendesha magari ya vita na wapanda farasi 40,000, naye akampiga Shobaki mkuu wa jeshi, akafa huko.+ 19 Wafalme wote waliokuwa watumishi wa Hadadezeri walipoona kwamba wameshindwa na Waisraeli, mara moja wakafanya amani na Waisraeli, wakawa watumishi wao;+ na Wasiria wakaogopa kuwasaidia tena Waamoni.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki