Ayubu
39 “Je, unajua mbuzi wa milimani huzaa wakati gani?+
Je, umewahi kuwatazama paa wakizaa watoto wao?+
2 Je, wewe huhesabu miezi ambayo wanabeba mimba?
Je, unajua wakati wanapozaa?
3 Wao huchuchumaa wanapozaa watoto wao,
Na uchungu wao wa kuzaa huisha.
4 Watoto wao hupata nguvu na kukua mbugani;
Huenda zao na hawarudi.
6 Nimelifanya jangwa tambarare kuwa makao yake
Na nchi yenye chumvi kuwa makazi yake.
7 Yeye hudharau vurugu za mji;
Hasikii kelele za mtu anayemwongoza.
8 Hutangatanga milimani, akitafuta malisho,
Akitafuta mmea wowote wa kijani.
9 Je, fahali mwitu yuko tayari kukutumikia?+
Je, atalala zizini mwako* usiku?
11 Je, utazitumaini nguvu zake nyingi
Na kumwacha afanye kazi zako ngumu?
13 Mabawa ya mbuni hupigapiga kwa shangwe,
Lakini, je, mabawa na manyoya yake yanaweza kulinganishwa na ya korongo?+
14 Kwa maana yeye huacha mayai yake ardhini,
Na kuyapasha joto mavumbini.
15 Yeye husahau kwamba mguu fulani unaweza kuyavunja
Au kwamba mnyama wa mwituni anaweza kuyakanyaga.
16 Huwatendea wanawe kwa ukatili, kana kwamba si wake;+
Haogopi kwamba huenda kazi yake ngumu ikawa ya bure.
18 Lakini anapoinuka na kupigapiga mabawa yake,
Humcheka farasi na yule aliyempanda.
19 Je, ni wewe unayempa farasi nguvu zake?+
Je, unamvika shingoni manyoya marefu yanayotikisika?
20 Je, unaweza kumfanya aruke kama nzige?
Mkoromo wake wa maringo unatisha.+
22 Huicheka hofu na haogopi chochote.+
Harudi nyuma kwa sababu ya upanga.
23 Podo la mishale hutoa sauti kando yake,
Mkuki na fumo humetameta.
25 Pembe inapolia, husema, ‘Aha!’
Hunusa vita kutoka mbali sana
Na kusikia kelele za makamanda na kelele za vita.+
26 Je, ni kwa uelewaji wako kwamba kipanga huruka,
Akiyatandaza mabawa yake kuelekea kusini?