Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 8/8 uku. 31
  • “Usikate Tamaa Kamwe”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Usikate Tamaa Kamwe”
  • Amkeni!—1992
  • Habari Zinazolingana
  • ‘Twahitaji Watu Wenye Kufuatia Haki’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Kutatua Matatizo ya Vijana
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Aliazimia Aishi Kulingana na Viwango vya Adili za Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Kutoka Mshuko wa Moyo Hadi Furaha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 8/8 uku. 31

“Usikate Tamaa Kamwe”

ALIPOZALIWA, Wilma Rudolph alikuwa mdogo sana na mdhaifu. Alianza kutembea alipokuwa mwenye umri wa miaka minne. Ndipo akawa mgonjwa sana kwa homa inayosababisha vipele vyekundu na homa ya mapafu. Ingawa hakufa, mguu wake wa kushoto ulipooza. Akiazimia kuwa Wilma angetembea, mama yake alikanda mguu wake uliodhoofika na akafunza watoto wake wakubwa watatu kufanya hivyo pia. Kwa hiyo kulikuwa na mabadilishano manne ya kazi ya “kusugua Wilma.”

Alipokuwa mwenye umri wa miaka minane, Wilma aliweza kutembea akiwa na kigango cha mguu. Upesi alikuwa anakimbia na kucheza. Aliazimia kushinda ulemavu wake. Mazoezi yalimsaidia, na ndivyo na shauri la mama yake: “Usikate tamaa kamwe.”

Wilma hakukata tamaa. Na katika 1960, kwenye Olimpiki katika Roma, Italia, alipata medali tatu za dhahabu. Yeye alishinda mbio za meta 100 na meta 200 na akaongoza katika mkondo wa mwisho wa mbio za kupokezana vijiti za meta 400.

Wakati wa vita ya ulimwengu ya kwanza, Glenn Cunningham alipokuwa mvulana wa miaka saba, alichomeka vibaya sana miguuni likiwa tisho kwa uhai wake. Alikaa miezi kadhaa kitandani na aliambiwa kuwa huenda asiweze kutembea tena kamwe. Mama yake alikanda kila siku misuli yake iliyoharibika na akamhimiza atembee na halafu akimbie. Glenn hakukata tamaa. Kwa kweli, hatimaye alishinda mbio 21 kati ya 31 za meta 1,600 katika kiwanja cha ndani ya jengo katika Madison Square Garden. Na, katika 1934, aliweka rekodi mpya ya dunia katika mbio za meta 1,600.

Wakati fulani katika maisha zetu sisi sote hukabiliana na vikwazo vya aina moja au nyingine. Mara nyingi ni tatizo fulani la kiafya. Badala ya kukubali kushindwa, ni vema kama nini kuazimia kutokata tamaa! “Hatufi moyo,” akaandika mtume Paulo kuhusiana na jitihada za kiroho. “Hata kama maumbile yetu ya nje [mwili wetu] yataoza, lakini, kwa ndani tunafanywa wapya [au kupewa nguvu mpya] siku kwa siku.”—2 Wakorintho 4:16, HNWW.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

UPI/Bettmann Newsphotos

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki