Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 8/15 uku. 30
  • Kujua Yaliyo Katika Habari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kujua Yaliyo Katika Habari
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kuvumilia Dhambi Si Sifa Nzuri
  • Ushuhuda Usiokanika
  • Kusaidia Wale Walio na UKIMWI
    Amkeni!—1994
  • Jinsi Madaktari Hukabiliana na UKIMWI
    Amkeni!—1992
  • UKIMWI— Lile Wazazi na Watoto Wanapaswa Kujua
    Amkeni!—1992
  • UKIMWI— Shida kwa Matineja
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 8/15 uku. 30

Kujua Yaliyo Katika Habari

Kuvumilia Dhambi Si Sifa Nzuri

Katika hotuba yake ya hivi majuzi kwa viongozi wa kanisa, mchangiaji-habari za safu za magazeti ya kidini Michael J. McManus alisema kwamba makanisa yamechangia kuvunjika-vunjika kwa jamaa za Waamerika. Ndivyo linavyoripoti gazeti moja la Kalifornia, The Fresno Bee. McManus alisema kwamba kulikuwa na talaka milioni 1.2 na watoto 750,000 waliozaliwa kiharamu katika United States wakati wa 1985, na kwamba waandamini wawili-wawili wasiofunga ndoa milioni 2.2 walikuwa wakiishi pamoja. “Kanisa limefanya nini kuhusu yote hayo?” yeye akauliza, akiongezea hivi: “Kanisa limekimya; limekimya vibaya; limekimya katika njia yenye kuchukiza.”

McManus alionyesha kwamba, badala ya kushikilia kwa uthabiti viwango vya adili ya Biblia, vinavyohimiza uaminifu katika ndoa, kanisa limechukua hali ya kunyamaza kuhusu masuala haya ili kutegemeza idadi ya hudhurio. Kama mfano, yeye alitaja azimio la hivi karibuni “kwamba Kanisa la Episkopali limeacha kuwapinga wanaume na wanawake wanaoishi pamoja bila kufunga ndoa.”

Kwa wazi, maoni kama hayo ya kisasa kuhusu ngono na ndoa yanapingana sana na Biblia. Mtume Mkristo Paulo alisema hivi: “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi.” (Waebrania 13:4) Mafarisayo walipokabiliana na Yesu Kristo kwa habari ya talaka, yeye alisema kwamba “mtu atamwacha babaye na mamaye, atambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja.” Yeye aliongezea hivi: “Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.”—Mathayo 19:4, 5, 9.

Akiitikia azimio la ulegevu la kanisa kuhusu masuala hayo ya adili, McManus alisema hivi: “Kanisa la Episkopali limefikia mahali ambapo linasema kwamba sifa yalo nzuri zaidi ni kuvumilia. Hakuna mahali po pote ambapo Yesu amesema kwamba dhambi ivumiliwe. Yeye aliilaumu vikali dhambi.” Wanafunzi wa Biblia wenye kuarifiwa vizuri wanakubali.

Ushuhuda Usiokanika

“Baada ya miaka mingi ya kutia shaka yenye kiburi ya uagnosti, kwa kinyiminyimi wanasayansi wanaanza kumfikiria Mungu tena,” akasema mchangiaji-habari za safu za magazetini Pete McMartin wa The Vancouver Sun, gazeti la British Columbia. Ijapokuwa dini na sayansi zimehitilafiana kwa karne nyingi, “sivyo ilivyo tena,” anasema Wasley Krogdahl, aliyekuwa hapo zamani profesa wa elimu ya nyota na fizikia wa Chuo Kikuu cha Kentucky. Krogdahl ameifanya kazi yake ya maisha iwe kuchungulia katika darubini za kuona mbali na kujifunza kuhusu ulimwengu wote mzima. “Wote unaanza kuonekana kama mpango ulio mkubwa,” anaeleza, akiongezea hivi: “Kosmolojia (elimu ya ulimwengu wote mzima) inaonyesha wazi kwamba ulimwengu wote mzima ulikuwa na mwanzo, na hilo ladokeza muumba.”—The State Journal-Register, Springfield, lllinois.

Angalau wanasayansi fulani wanafikiria tena chanzo cha ulimwengu wote mzima. Sababu ni nini? Mtaalamu wa nyota Krogdahl anaeleza hivi: “Ulimwengu wote mzima unaanza kujaa maana zaidi ya ulivyofanya miaka 50 iliyopita.” Wakati wa miaka 25 iliyopita, ukuzi wa vifaa ambavyo ni vyepesi zaidi kama vile darubini zinazoweza kupiga picha mnururisho na zile zinazowekwa juu ya satelaiti zimetokeza uvumbuzi wa kwezar, nyota nyutroni, na pulsari. Krogdahl anakiri kwamba maarifa ya ulimwengu wote mzima yanavyozidi kuongezeka, ndivyo na ushuhuda wa kwamba kuna Mungu. Yeye anasema kwamba ushuhuda huo, “umebomoa nguzo kutoka kwa wasiosadiki kuwapo kwa Mungu.”

Hata hivyo, jambo ambalo akili za wanasayansi zimechukua miaka mingi kukubali baada ya utafiti na uchunguzi mwingi, wanafunzi wa Biblia wamelijua kwa karne nyingi. “Sifa zisizoonekana za [Muumba], yaani uwezo wake wa milele na uungu, zimekuwa zikionekana, kwa jicho la akili, tangu ulimwengu ulipoanza, katika vitu ambavyo yeye amefanya.”(Warumi 1:20, The New English Bible) Tukisema kwa njia rahisi, sikuzote ushuhuda huo umekuwa usiokanika.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki