Ratiba ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi ya 1989
MAAGIZO
Wakati wa 1989, ufuatao utakuwa ndio mpango wa kuongozea Shule ya Huduma ya Kitheokrasi.
VITABU VYA MAFUNDISHO: Biblia, “All Scripture Is Inspired of God and Beneficial” [si], Reasoning From the Scriptures [rs], na Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani [peSW] vitakuwa ndio msingi wa migawo.
Shule itaanza kwa wimbo, sala, na maneno ya kukaribisha, kisha itaendelea hivi: [Nyimbo katika parandesi ni kwa ajili ya nyimbo kutoka kitabu cha nyimbo cha Kiswahili cha 1983].
MGAWO NA. 1: Dakika 15. Huu wapasa uongozwe na mzee au na mtumishi wa huduma mwenye kustahili. Mgawo huu utategemea kitabu “All Scripture Is Inspired of God and Beneficial.” Mgawo huu umepasa utolewe kuwa hotuba ya maagizo ya dakika 10 kufika 12 pamoja na kurudiwa kwa mdomo kwa dakika 3 kufika 5, kwa kutumia maswali ya sehemu hiyo yaliyochapwa. Lengo la hotuba hii si kusimulia tu habari hiyo, bali ni kuvuta fikira juu ya faida inayoweza kutumika ya habari hiyo inayozungumzwa, kukazia yatakayokuwa yenye msaada zaidi kwa kundi. Mahali inapohitajiwa, kichwa kimepasa kichaguliwe. Wote wanatiwa moyo kutangulia kujitayarisha kwa uangalifu ili wanufaike kikamilifu na habari hiyo.
Akina ndugu wenye kupewa mgawo wa hotuba hii wamepaswa wafuate wakati wao kwa uangalifu. Shauri la faragha limepasa kutolewa iwapo lazima.
MAMBO MAKUU KUTOKANA NA KUSOMA BIBLIA: Dakika 6. Mgawo huu umepasa uongozwe na mwangalizi wa shule au mzee mwingine mwenye kustahili au mtumishi wa huduma aliyegawiwa na mwangalizi wa shule. Huku kusiwe kusimulia tu sehemu zilizogawiwa kusomwa. Baada ya kutoa utangulizi mfupi wa mambo yaliyomo katika sura zilizogawiwa, wasaidie wasikilizaji wafahamu kwa nini na jinsi gani habari hiyo ni yenye faida kwetu. Chunguza matoleo ya Mnara wa Mlinzi upate habari zaidi za kukaziwa. Ndipo wanafunzi wataruhusiwa na mwangalizi wa shule waende kwenye madarasa yao mbalimbali.
HOTUBA NA. 2: Dakika 5. Huku ni kusoma Biblia juu ya habari iliyogawiwa itakayotolewa na ndugu. Hii itakuwa hivyo katika shule kubwa na pia vikundi vidogo vya shule. Kwa kawaida migawo ya kusoma ni mifupi kutosha kuruhusu mwanafunzi atoe habari yenye maelezo katika utangulizi na maelezo yake ya kumalizia, na hata katika mambo makuu ya katikati. Mandhari ya nyuma ya kihistoria, maana ya kiunabii au ya kimafundisho na jinsi kanuni zinavyohusu, yanaweza kutiwa ndani. Mistari yote iliyogawiwa yapasa isomwe kabisa.
HOTUBA NA. 3: Dakika 5. Hotuba hii watagawiwa akina dada. Habari za hotuba hii zitatolewa kwa matumizi ya zamu kwa zamu ya vitabu viwili, Reasoning na Kuishi Milele, na habari za kutoka kitabu hicho cha pili watagawiwa hasa wanafunzi wachanga au wapya. Mwanafunzi aliyegawiwa amepaswa awe anaweza kusoma. Wakati wa kutoa hotuba hizo, mwanafunzi anaweza kuwa ama ameketi katika kiti ama amesimama. Msaidizi mmoja atapangwa na mwangalizi wa shule, lakini wasaidizi zaidi wanaweza kutumiwa. Ni afadhali vikao vitie ndani utumishi wa shambani au kutoa ushuhuda wa vivi hivi. Anayetoa hotuba anaweza yeye mwenyewe kuanzisha mazungumzo ili kuweka kikao ama aache msaidizi au wasaidizi wake wafanye hivyo. Jambo la kufikiriwa kwanza ni habari inayotolewa, si kikao. Mwanafunzi amepaswa atumie kichwa kilichoonyeshwa.
HOTUBA NA. 4: Dakika 5. Igawiwe ndugu au dada. Anapogawiwa ndugu, apaswa ahutubie wasikilizaji wote. Ili hotuba yake iwe yenye kuelimisha na yenye kunufaisha kweli kweli wale wanaoisikia, kwa kawaida itakuwa bora ndugu atayarishe kwa kufikiria wasikilizaji katika Jumba la Ufalme. Lakini, ikiwa habari inahusu sana hali nyingine au kikao kingine chenye kufaa, ndugu anaweza kuchagua kukuza hotuba yake kulingana na kikao cha hali hiyo. Mwanafunzi amepaswa atumie kichwa kilichoonyeshwa.
Dada anapogawiwa hotuba hii, apaswa kuitoa kama Hotuba Na. 3 inavyoelezwa itolewe.
SHAURI NA MAELEZO: Baada ya kila hotuba ya mwanafunzi, mwangalizi wa shule atatoa shauri linalohusu, si lazima afuate mpango wa shauri lenye kuendelea kama ilivyoandikwa katika kikaratasi cha Shauri la Usemi. Badala ya kufanya hivyo, anapaswa kukaza fikira juu ya sehemu zile ambazo mwanafunzi anahitaji kufanyia maendeleo. Kama mhutubu-mwanafunzi anastahili kuandikiwa “V” tu na hakuna sifa nyingine ya usemi iliyotiwa alama “M” au “T,” basi mshauri amepaswa atie duara kuzunguka sifa ya usemi ambayo mwanafunzi atatengeneza safari nyingine, afanye hivyo katika kisanduku ambamo kwa kawaida alama hizi “V” “M” au “T” zingewekwa. Atamwarifu mwanafunzi jambo hili jioni hiyo na pia aonyeshe sifa hiyo ya usemi penye kikaratasi cha Mgawo wa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi (S-89) kitakachofuata cha mwanafunzi huyo. Wale wanaotoa hotuba wamepaswa wakalie viti vya mbele karibu na jukwaa. Hiyo itaokoa wakati, na pia itamwezesha mwangalizi wa shule ampe kila mwanafunzi shauri lake moja kwa moja. Wakati unaporuhusu baada ya kutolewa kwa shauri la mdomo linalohitajiwa, maelezo yaweza kutolewa na mshauri juu ya mambo yenye kuelimisha na yanayofaa kutumiwa ambayo wanafunzi hawakuyazungumza. Imempasa mwangalizi wa shule aangalie asije akatumia zaidi ya jumla ya dakika mbili akitoa shauri na maelezo baada ya kila hotuba ya mwanafunzi. Ikiwa ule utoaji wa mambo makuu ya Biblia uliacha nje jambo fulani la maana, shauri la faragha laweza kutolewa.
KUTAYARISHA HOTUBA: Ndugu wenye kugawiwa hotuba Na. 1 wamepaswa wachague kichwa inapohitajiwa. Wanafunzi wenye kugawiwa hotuba ya pili wachague kichwa kitakachoruhusu mazungumzo ya sehemu kubwa zaidi ya mambo yaliyo katika habari. Wanafunzi wenye kugawiwa hotuba ya nne wamepaswa watumie kichwa kilichoonyeshwa. Kabla ya kutoa hotuba, wanafunzi watataka warudie kusoma habari ya Kiongozi cha Shule iliyo na sifa ya usemi inayoendelea kutengenezwa.
KUFUATA WAKATI: Kusiwe hotuba ya kuzidi wakati uliopewa. Wala maelezo ya mshauri yasizidi wakati. Hotuba Na. 2 mpaka 4 zimepasa zikatizwe kwa busara ikiwa wakati unakwisha. Aliyepewa mgawo wa kutoa “ishara ya kuacha” amepaswa kufanya hivyo mara hiyo. Ndugu wanaoshughulika na Mgawo 1 wanapozidi wakati wao wamepaswa washauriwe kwa faragha. Wote wamepaswa wafuate wakati wao kwa uangalifu. Jumla ya dakika za programu yote ya shule ni: Dakika 45 bila kuhesabu dakika za wimbo na sala.
PITIO LA KUANDIKA: Pindi kwa pindi pitio la kuandika linatolewa. Katika kujitayarisha, pitia migawo ya habari na kumaliza mpango wa kusoma Biblia kibinafsi ulioratibiwa. Biblia pekee ndiyo inayoruhusiwa kutumiwa wakati wa pitio hili la dakika 25. Wakati unaobaki utatumiwa kwa mazungumzo ya maswali na majibu. Kila mwanafunzi atasahihisha karatasi yake mwenyewe. Mwangalizi wa shule atasoma majibu yote na kukaza fikira juu ya maswali ambayo ni magumu zaidi, akiwasaidia wote wayafahamu majibu vizuri. Ikiwa, kwa sababu fulani, hali za kwenu zinalazimisha pitio la kuandikwa lisifanywe juma lililopangwa laweza kufanywa juma la baadaye badala ya lile linaloonyeshwa katika ratiba.
MAKUNDI MAKUBWA NA MADOGO: Labda makundi yenye wanafunzi 50 au zaidi walioandikwa yatapenda kufanya mpango ili vikundi vya ziada vya wanafunzi vitoe mbele ya washauri wengine hotuba zilizoratibiwa. Bila shaka, watu wasio wakfu wanaoishi kupatana na kanuni za Kikristo wanaweza pia kujiandikisha katika shule hii na kupokea migawo.
WANAFUNZI WASIOKUWAPO: Wote katika kundi wanaweza kuonyesha uthamini kwa shule hii kwa kuhudhuria kila kipindi cha kila juma, kwa kutayarisha vizuri migawo yao, na kwa kushiriki vipindi vya maswali. Inatumainiwa kwamba wanafunzi wote watatimiza migawo yao kwa dhamiri. Mwanafunzi asipokuwapo wakati amepangwa kwenye ratiba, mtu mwingine anaweza kujitolea kuchukua mgawo huo, akionyesha matumizi yoyote ya habari kwa kadiri awezavyo katika huo muda mfupi wa kuarifiwa. Au, mwangalizi wa shule anaweza kuzungumza habari hiyo kwa ushirika unaofaa wa wasikilizaji.
RATIBA
Jan. 2 Kusoma Biblia: Ezekieli 38 na 39
Na. 1: Utangulizi kwa Maombolezo (si kur. 130-1, maf. 1-7)
Na. 2: Ezekieli 39:1-13
Na. 3: Wanabii wa Kweli Hawakuelewa Sikuzote Jinsi na Lini Vitu Vilivyotabiriwa Vingetukia (rs uku. 134)
Na. 4: Matamko ya Mnabii wa Kweli Huendeleza Ibada ya Kweli (rs uku. 135, kichwa kidogo cha kwanza)
Jan. 9 Kusoma Biblia: Ezekieli 40 hadi 44
Na. 1: Maombolezo 1:1 hadi 5:22 (si kur. 131-2, maf. 8-12)
Na. 2: Ezekieli 44:1-16
Na. 3: Sababu kwa Nini Yesu Hangeweza Kurudi Akiwa Binadamu (peSW sura 17, mafu. 1-5)
Na. 4: Wanabii wa Kweli Hutambulishwa kwa Matunda Yanayotokezwa (rs uku. 135, kichwa kidogo cha pili, hadi uku. 137, fu. 1)
Jan. 16 Kusoma Biblia: Ezekieli 45 hadi 48
Na. 1: Utangulizi kwa Ezekieli (si kur. 132-3, maf. 1-6)
Na. 2: Ezekieli 47:1-12
Na. 3: Sababu kwa Nini Makosa Yanayofanywa na Mashahidi wa Yehova Hayawaondolei Ustahili wa Kuwa Wanabii wa Kweli (rs uku. 137, maf. 2-4)
Na. 4: Mungu Haandikii Kimbele Kila Mtu Wakati wa Kufa (rs uku. 138)
Jan. 23 Kusoma Biblia: Danieli 1 na 2
Na. 1: Ezekieli 1:1 hadi 7:27 (si kur. 133-4, mafu.7-11)
Na. 2: Danieli 2:36-46
Na. 3: Mwili wa Yesu Haukuchukuliwa Mbinguni (peSW sura 17, mafu. 6-12)
Na. 4: Si Kila Kitu Kinachotukia Ambacho Ni Mapenzi ya Mungu (rs kur. 139 hadi 140, kichwa kidogo cha kwanza)
Jan. 30 Kusoma Biblia: Danieli 3 na 4
Na. 1: Ezekieli 8:1 hadi 11:25 (si uku. 134, maf. 12-14)
Na. 2: Danieli 3:19-30
Na. 3: Mungu Hatangulii Kujua na Kuandikia Kila Kitu (rs kur. 140, kichwa kidogo cha pili)
Na. 4: Uwezo wa Mungu wa Kutangulia Kujua na Kutangulia Kuandikia Matukio (rs uku. 141)
Feb. 6 Kusoma Biblia: Danieli 5 na 6
Na. 1: Ezekieli 12:1 hadi 23:49 (si 134-5, maf. 15-19)
Na. 2: Danieli 5:17-31
Na. 3: Jinsi Kristo Anavyorudi na Jinsi Kurudi Kwake Kunavyotambuliwa (peSW sura 17, mafu. 13-17)
Na. 4: Sababu kwa Nini Mungu Hakutumia Uwezo Wake wa Kutangulia Kujua Mambo Kwa Habari ya Adamu (rs uku. 142, kichwa kidogo cha kwanza)
Feb. 13 Kusoma Biblia: Danieli 7 na 8
Na. 1: Ezekieli 24:1 hadi 32:32 (si kur. 135-6, maf. 20-23)
Na. 2: Danieli 8:15-27
Na. 3: Mungu Hakuwaandikia Kimbele Yakobo, Esau, au Yuda (rs uku. 142, kichwa kidogo cha pili, hadi uku. 143, kichwa kidogo cha kwanza)
Na. 4: Kundi la Kikristo Liliandikiwa Kimbele Kwa Njia Gani? (rs uku. 143, kichwa kidogo cha pili)
Feb. 20 Kusoma Biblia: Danieli 9 na 10
Na. 1: Ezekieli 33:1 hadi 39:29 (si uku. 136, maf. 24-26)
Na. 2: Danieli 9:20-27
Na. 3: “Kuja” kwa Kristo na Mwisho wa Ulimwengu Kunarejezea Nini? (peSW sura 18, maf. 1-6)
Na. 4: Ni Nini Rai ya Kimaandiko juu ya Unajimu? (rs kur. 144-5)
Feb. 27: Kusoma Biblia: Danieli 11 na 12
Na. 1: Ezekieli 40:1 hadi 48:35 (si kur. 136-7, maf. 27, 28)
Na. 2: Danieli 12:1-13
Na. 3: Ni Nini Baadhi ya Sababu Timamu za Kuitikadi Katika Mungu? (rs uku. 145, kichwa kidogo cha mwisho)
Na. 4: Uovu na Mateso Havithibitishi Kutokuwako kwa Mungu (rs uku. 146 hadi uku. 147, kichwa kidogo cha kwanza)
Mac. 6 Kusoma Biblia: Hosea 1 hadi 5
Na. 1: Danieli, Utangulizi na Uthibitisho wa Ukweli Wacho (si kur. 138-9, maf. 1-7
Na. 2: Hosea 5:1-15
Na. 3: Vita na Njaa Ni Uthibitisho Uonekanao wa Kuwapo kwa Kristo Kusikoonekana (peSW uku. 150)
Na. 4: Mungu Ni Mtu Halisi Awezaye Kuwa na Hisia za Moyoni (rs uku. 147, kichwa kidogo cha kwanza)
Mac. 13 Kusoma Biblia: Hosea 6 hadi 10
Na. 1: Danieli 1:1 hadi 4:37 (si kur. 139-40, maf. 8-11)
Na. 2: Hosea 8:1-14
Na. 3: Mungu Hakuwa na Mwanzo (rs uku. 148, kichwa kidogo cha pili)
Na. 4: Utumizi wa Jina la Mungu Ni wa Maana Kabisa kwa Wokovu (rs uku. 149, kichwa kidogo cha kwanza)
Mac. 20 Kusoma Biblia: Hosea 11 hadi 14
Na. 1: Danieli 5:1 hadi 8:27 (si kur. 140-1, maf. 12-15)
Na. 2: Hosea 11:1-12
Na. 3: Tauni, Matetemeko ya Dunia, Woga, na Uasi-sheria Ni Uthibitisho wa Kuwapo kwa Kristo (peSW kur. 151-2)
Na. 4: Je! Dini Zote Ni Nzuri? (rs uku. 149, kichwa kidogo cha pili)
Mac. 27 Kusoma Biblia: Yoeli 1 hadi 3
Na. 1: Danieli 9:1 hadi 12:13 (si uku. 141, maf. 16-19)
Na. 2: Yoeli 2:21-32
Na. 3: Yesu ni “Mungu” wa Aina Gani? (rs kur. 150, kichwa kidogo cha kwanza)
Na. 4: Kushinda Vipingamizi vya Kutokuwa naItikadi Katika Mungu (rs uku. 150, fu. 3, hadi uku. 151, fu. 3)
Apr. 3 Kusoma Biblia: Amosi 1 hadi 5
Na. 1: Utangulizi kwa Hosea (si kur. 143-4, maf. 1-8)
Na. 2: Amosi 3:1-15
Na. 3: Utimizo wa 2 Timotheo 3:1-5 Ni Ishara ya Siku za Mwisho (peSW kur. 152-4)
Na. 4: Sababu kwa Nini Binadamu Hawajaweza Kusimamisha Serikali Yenye Haki (rs uku. 152 hadi uku. 153, fu. 1)
Apr. 10 Kusoma Biblia: Amosi 6 hadi 9
Na. 1: Hosea 1:1 hadi 14:9 (si kur. 144-5, maf. 9-13)
Na. 2: Amosi 8:1-14
Na. 3: Sababu kwa Nini Jitihada za Wanadamu za Kuleta Kitulizo Haziwezi Kufanikiwa (rs uku. 153, kichwa kidogo cha kwanza, hadi uku. 154, kichwa kidogo cha kwanza)
Na. 4: Ufalme wa Mungu Jawabu Pekee kwa Mahitaji Halisi ya Aina ya Binadamu (rs uku. 154, kichwa kidogo cha pili)
Apr. 17 Kusoma Biblia: Obadia 1 hadi Yona 4
Na. 1: Utangulizi kwa Yoeli (si uku. 146, maf. 1-5)
Na. 2: Yona 1:14–2:10
Na. 3: Sababu kwa Nini “Har–Magedoni” Si Neno La Kuogopesha (peSW sura 19, maf. 1-3)
Na. 4: Manabii ya Biblia Yamethibitika Kuwa Yenye Kutumainika Kabisa (rs uku. 155, kichwa kidogo cha kwanza)
Apr. 24 Ptio la Kuandika. Maliza Ezekieli 38 hadi Yona 4
Mei 1 Kusoma Biblia: Mika 1 hadi 4
Na. 1: Yoeli 1:1 hadi 3:21 (si kur. 146-7, maf. 6-11)
Na. 2: Mika 4:1-12
Na. 3: Maponyo ya Kimwujiza Leo Hayafanywi na Roho ya Mungu (rs uku. 156 hadi uku. 157, fu. 3)
Na. 4: Tofauti Kati ya Maponyo ya Yesu na Mitume Wake na Yale ya Leo (rs uku. 157, kichwa kidogo, hadi uku. 158, kichwa kidogo cha kwanza)
Mei 8 Kusoma Biblia: Mika 5 hadi 7
Na. 1: Utangulizi kwa Amosi (si kur. 148-9, maf. 1-6)
Na. 2: Mika 6:3-16
Na. 3: Baraka Zinakuja kwa Aina ya Binadamu Baada ya Har–Magedoni (pe kur. 156-8)
Na. 4: Jinsi Wakristo wa Kweli Wanavyotambulishwa Leo (rs uku. 158, vichwa vidogo cha pili na cha tatu)
Mei 15 Kusoma Biblia: Nahumu 1 hadi 3
Na. 1: Amosi 1:1 hadi 9:15 (si kur. 149-50, maf. 7-12)
Na. 2: Nahumu 1:2-14
Na. 3: Sababu Vipawa vya Kuponya Vilipewa Katika Karne ya Kwanza (rs uku. 159)
Na. 4: Kuna Tumaini Gani kwa Kuponya kwa Kweli kwa Ajili ya Aina ya Binadamu Yote? (rs uku. 160, kichwa kidogo cha pili)
Mei 22 Kusoma Biblia: Habakuki 1 hadi 3
Na. 1: Utangulizi kwa Obadia (si kur. 151-2, maf. 1-5)
Na. 2: Habakuki 2:1-14
Na. 3: Ni Baraka na Kazi Gani Itakuwa Fungu la Waokokaji wa Har–Magedoni? (peSW sura 19, maf. 4-7)
Na. 4: Ni Nani Pekee Aliyekuwako Kabla ya Kuwa Binadamu? (rs uku. 161, kichwa kidogo cha mwisho)
Mei 29 Kusoma Biblia: Sefania 1 hadi 3
Na. 1: Obadia 1 hadi 21 (si uku. 152, maf. 6-9)
Na. 2: Sefania 2:1-11
Na. 3: Si Watu Wote Wema Huenda Mbinguni (rs uku. 162, kichwa kidogo cha kwanza)
Na. 4: Adamu Hakuahidiwa Uhai wa Kimbingu (rs uku. 162, kichwa kidogo cha pili)
Juni 5 Kusoma Biblia: Hagai 1 na 2
Na. 1: Utangulizi kwa Yona (si kur. 153-4, maf. 1-5)
Na. 2: Hagai 2:1-9, 20-23
Na. 3: Kutambulisha “Mbingu Mpya” na “Dunia Mpya” (peSW sura 19, maf. 8-10)
Na. 4: Haihitajiwi Kabisa Kwenda Mbinguni Ili Kuwa na Wakati Ujao Wenye Furaha (rs uku. 163, kichwa kidogo cha kwanza)
Juni 12 Kusoma Biblia: Zekaria 1 hadi 5
Na. 1: Yona 1:1 hadi 4:11 (si uku. 154, maf. 6-9
Na. 2: Zekaria 4:1-14
Na. 3: Yesu Hakufungua Njia ya Kwenda Mbinguni kwa Wale Waliokufa Kabla ya Yeye Kufa (rs uku. 163, kichwa kidogo cha pili)
Na. 4: Uhai wa Kimbingu Si Tumaini la Wakristo Wote (rs uku. 164)
Juni 19 Kusoma Biblia: Zekaria 6 hadi 9
Na. 1: Utangulizi kwa Mika (si kur. 155-6, maf. 1-8)
Na. 2: Zekaria 8:9-23
Na. 3: Baraka za Ufalme Zinakuja Kwa Aina ya Binadamu (peSW kur. 161-2)
Na. 4: Maandiko ya Kikristo Yana Tumaini la Baraka za Kidunia (rs uku. 165, kichwa kidogo)
Juni 26 Kusoma Biblia: Zekaria 10 hadi 14
Na. 1: Mika 1:1 hadi 7:20 (si kur. 156-7, maf. 9-15)
Na. 2: Zekaria 13:1-9
Na. 3: Ni Wangapi Watapata Thawabu ya Kimbingu na Sababu Namba Hiyo Si ya Kitamathali (rs uku. 166, kichwa kidogo cha kwanza, na uku. 167, kichwa kidogo cha kwanza)
Na. 4: 144,00 Si Israeli wa Asili Pekee (rs kur. 166, kichwa kidogo cha pili)
Jul. 3 Kusoma Biblia: Malaki 1 hadi 4
Na. 1: Utangulizi kwa Nahumu (si kur. 158-9, maf. 1-7)
Na. 2: Malaki 3:1-10, 16-18
Na. 3: Baraka Ziko Akibani kwa Waokokaji wa Har–Magedoni (peSW sura 19, maf. 11-21)
Na. 4: Umati Mkubwa Mbele ya Kiti cha Ufalme cha Mungu, Lakini Si Katika Mbingu (rs uku. 167, kichwa kidogo cha pili)
Jul. 10 Kusoma Biblia: Mathayo 1 hadi 3
Na. 1: Nahumu 1:1 hadi 3:19 (si kur. 159-60, maf. 8-10)
Na. 2: Mathayo 3:1-17
Na. 3: Wajibu wa Kimbingu wa 144,000 (rs uku. 168, kichwa kidogo cha kwanza)
Na. 4: Biblia Huonyesha Wafu Hawasumbuliwi na Maumivu (rs uku. 169, vichwa vidogo cha kwanza na cha pili)
Jul. 17 Kusoma Biblia: Mathayo 4 na 5
Na. 1: Utangulizi kwa Habakuki (si uku. 161, maf. 1-5)
Na. 2: Mathayo 5:1-17
Na. 3: Tumaini la Ufufuo Katika Maandiko ya Kiebrania (peSw sura 20, maf. 1-4)
Na. 4: Biblia Huonyesha Kwamba Wema na Wabaya Pia Huenda Katika Hell Wanapokufa (rs uku. 170, vichwa vidogo cha kwanza hadi cha tatu)
Jul. 24 Kusoma Biblia: Mathayo 6 na 7
Na. 1: Habakuki 1:1 hadi 3:19 (si kur. 161-2, maf. 6-11)
Na. 2: Mathayo 6:1-14, 31-33
Na. 3: Watafsiri wa Biblia Husababisha Mvurugo Juu ya Helo (rs uku. 170, kichwa kidogo cha mwisho)
Na. 4: Waovu Waadhibiwa Milele Lakini Hawateswi Milele (rs uku. 171, kichwa kidogo)
Jul. 31 Kusoma Biblia: Mathayo 8 na 9
Na. 1: Utangulizi kwa Sefania (si kur. 163-4, maf. 1-6)
Na. 2: Mathayo 9:18-38
Na. 3: Mafufuo Yaliyorekodiwa Katika Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo (peSW sura 20, maf. 5-9)
Na. 4: Maana ya Mateso ya Milele Yaliyotajwa Katika Ufunuo (rs uku. 172, kichwa kidogo)
Ago. 7 Kusoma Biblia: Mathayo 10 na 11
Na. 1: Sefania 1:1 hadi 3:20 (si kur. 164-5, maf. 7-9)
Na. 2: Mathayo 10:5-15, 24-31
Na. 3: Ni Nini Gehena ya Moto Iliyotajwa na Yesu? (rs uku. 173, kichwa kidogo)
Na. 4: Kuadhibu Waovu kwa Mungu Hupatana na Utu Wake (rs uku. 174, kichwa kidogo cha tatu, na uku. 175, kichwa kidogo)
Ago. 14 Kusoma Biblia: Mathayo 12 na 13
Na. 1: Utangulizi kwa Hagai (si kur. 166-7, maf. 1-7)
Na. 2: Mathayo 13:34-52
Na. 3: Ni Nani Watafufuliwa? (peSW sura 20, maf. 10-18)
Na. 4: Fumbo la Maneno Juu ya Tajiri na Lazaro Hufundisha Nini? (rs uku. 174, kichwa kidogo cha mwisho)
Ago. 21 Kusoma Biblia: Mathayo 14 na 15
Na. 1: Hagai 1:1 hadi 2:23 (si kur. 167, maf. 8-12)
Na. 2: Mathayo 15:1-20
Na. 3: Ni Nini Kinachokanusha Kwamba Yesu Hakuzaliwa Desemba 25? (rs uku. 176)
Na 4: Ni Nani Waliokuwa Wanajimu Waliomtembelea Yesu? (rs uku. 177, kichwa kidogo cha kwanza)
Ago. 28 Pitio la Kuandika. Maliza Mika 1 hadi Mathayo 15
Sept. 4 Kusoma Biblia: Mathayo 16 na 17
Na. 1: Utangulizi kwa Zekaria (si kur. 168-9, maf. 1-7)
Na. 2: Mathayo 16:13-28
Na. 3: Yale Mafufuo Mawili (peSW sura 20, maf. 19-24)
Na. 4: Ni Nini Asili ya Upaji wa Krismasi (rs kur. 177, kichwa kidogo)
Sept. 11 Kusoma Biblia: Mathayo 18 na 19
Na. 1: Zekaria 1:1 hadi 7:14 (si kur. 169-70, maf. 8-17)
Na. 2: Mathayo 18:7-22
Na. 3: Sababu kwa Nini Wakristo Wasijihusishe Katika Sherehe za Krismasi? (rs uku. 178, kichwa kidogo)
Na. 4: Sababu kwa Nini Wakristo Wasisherehekee Ista au Mwaka Mpya? (rs uku. 179, kichwa kidogo, hadi 180, kichwa kidogo cha kwanza)
Sept. 18 Kusoma Biblia: Mathayo 20 na 21
Na. 1: Zekaria 8:1 hadi 14:21 (si kur. 170-1, maf. 18-22)
Na. 2: Mathayo 20:17-34
Na. 3: Ufufuo Ni Muujiza Kweli Kweli (peSW sura 20, maf. 25-27)
Na. 4: Ni Nini Asili ya Sherehe za Siku ya Nafsi Zote? (rs uku. 180, kichwa kidogo cha pili)
Sept. 25 Kusoma Biblia: Mathayo 22 na 23
Na. 1: Utangulizi kwa Malaki (si kur. 172-3, maf. 1-6)
Na. 2: Mathayo 22:15-33
Na. 3: Sababu kwa Nini Wakristo Hawashiriki Katika Sikukuu za Kilimwengu? (rs uku. 181, kichwa kidogo, hadi uku. 182, kichwa kidogo cha tatu)
Na. 4: Biblia Husema Nini Juu ya Ibada ya Mifano? (rs uku. 183, kichwa kidogo cha kwanza)
Okt. 2 Kusoma Biblia: Mathayo 24 na 25
Na. 1: Malaki 1:1 hadi 4:6 (si kur. 173-4, maf. 7-12)
Na. 2: Mathayo 24:3-22
Na. 3: Siku ya Hukumu Itakuwa Ndefu Kadiri Gani, na Ni Nani Watahukumu? (peSW sura 21, maf. 1-4)
Na. 4: Ibada ya Kweli Haihitaji Mifano Ikiwa Msaada (rs uku. 183, kichwa kidogo cha mwisho)
Okt. 9 Kusoma Biblia: Mathayo 26
Na. 1: Utangulizi kwa Warumi (si kur. 204-5, maf. 1-7)
Na. 2: Mathayo 26:1-5, 17-30
Na. 3: “Watakatifu” Hawawezi Kutumikia Wakiwa Waombezi (rs uku. 184)
Na. 4: Mungu Anaonaje Mifano Ambayo Ni Vitu vya Kuabudiwa? (rs uku. 185, kichwa kidogo cha pili)
Okt. 16 Kusoma Biblia: Mathayo 27 na 28
Na. 1: Warumi 1:1 hadi 8:39 (si kur. 205-6, maf. 8-12)
Na. 2: Mathayo 28:7-20
Na. 3: Sababu Siku ya Hukumu Si ya Kuhofiwa? (peSW sura 21, maf. 5-7)
Na. 4: Inatupasa Kuhisije Juu ya Mifano Ambayo Tuliabudu Wakati Mmoja? (rs uku. 186, kichwa kidogo)
Okt. 23 Kusoma Biblia: Marko 1 na 2
Na. 1: Warumi 9:1 hadi 12:21 (si kur. 206-7, maf. 13-15)
Na. 2: Marko 1:1-15
Na. 3: Kutumia Kwetu Mifano Kunaweza Kuwa na Tokeo Gani Juu ya Wakati Ujao Wetu? (rs uku. 187)
Na. 4: Kutupa Kando Viwango vya Kiadili vya Biblia Hakuleti Uhuru (rs uku. 187, kichwa kidogo cha mwisho, hadi uku. 188, fu. 2)
Okt. 30 Kusoma Biblia: Marko 3 na 4
Na. 1: Warumi 13:1 hadi 16:27 (si uku. 207, maf. 16-19)
Na. 2: Marko 4:21-34
Na. 3: Ni Nini Mafufuo Kwenye Uhai na Kwenye Hukumu? (peSW sura 21, maf. 12-14)
Na. 4: Kufuatia Vitu vya Kimwili Ni Kujishinda (rs uku. 189, fu. 3)
Nov. 6 Kusoma Biblia: Marko 5 na 6
Na. 1: Utangulizi kwa 1 Wakorintho (si kur. 208-9 maf. 1-7)?
Na. 2: Marko 6:30-44, 56
Na. 3: Lazima Wakristo Waepuke Mashirika Mabaya (rs uku. 188, fu. 2)
Na. 4: Shetani, Mchochezi Mkuu Dhidi ya Amri za Mungu (rs uku. 189, kichwa kidogo cha mwisho, hadi uku. 190, kichwa kidogo cha kwanza)
Nov. 13 Kusoma Biblia: Marko 7 na 8
Na. 1: 1 Wakorintho 1:1 hadi 7:40 (si kur. 209-10, maf. 8-13)
Na. 2: Marko 7:5-23
Na. 3: Ni Nini Watu Watahukumiwa Kwacho Katika Siku ya Hukumu? (peSW sura 21 maf. 15-18)
Na. 4: Ni Mielekeo Gani ya Kujitegemea Ambayo Lazima Wakristo Waepuke? (rs uku. 190, kichwa kidogo cha pili, hadi uku. 191, kichwa kidogo cha kwanza)
Nov. 20 Kusoma Biblia: Marko 9 na 10
Na. 1: 1 Wakorintho 8:1 hadi 11:34 (si kur. 210-11, maf. 14-17)
Na. 2: Marko 9:1-13
Na. 3: Jina la Mungu Litapatikana Wapi Katika Biblia Zinazotumiwa kwa Kawaida? (rs uku. 191, kichwa kidogo cha mwisho, hadi uku. 193, fu. 7)
Na. 4: Sababu Gani Tafsiri Nyingi Zinapuuza Jina la Mungu? (rs uku. 193, kichwa kidogo)
Nov. 27 Kusoma Biblia: Marko 11 na 12
Na. 1: 1 Wakorintho 12:1 hadi 16:24 (si uku. 211. maf. 18-22)
Na. 2: Marko 12:28-44
Na. 3: Jinsi Yehova Anavyoamua Ni Nani Wataandikwa Katika Kitabu cha Uhai (peSW sura 21, maf. 19-21)
Na. 4: Sisi Tunajuaje Waandikaji wa Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo Walitumia Jina la Yehova? (rs uku. 194)
Des. 4 Kusoma Biblia: Marko 13 na 14
Na. 1: Utangulizi kwa 2 Wakorintho (si uku. 213, maf. 1-4)
Na. 2: Marko 13:21-37
Na. 3: Sababu Sisi Tunapendelea “Yehova” Kuliko “Yahweh”? (rs uku. 195, kichwa kidogo)
Na. 4: Kwa Nini Ni Jambo la Maana Kujua na Kutumia Jina la Yehova? (rs uku. 196, kichwa kidogo)
Des. 11 Kusoma Biblia: Marko 15 na 16
Na. 1: 2 Wakorintho 1:1 hadi 7:16 (si kur. 213-14, maf. 5-12)
Na. 2: Marko 15:1-15
Na. 3: Ni Nani Wataokoka Siku ya Hukumu Iliyopo? (peSW sura 21, maf. 22, 23)
Na. 4: Yehova wa “Agano la Kale” Si Yesu wa “Agano Jipya” (rs uku. 197, kichwa kidogo)
Des. 18 Kusoma Biblia: Luka 1
Na. 1: 2 Wakorintho 8:1 hadi 13:14 (si kur. 214-15, maf. 13-17)
Na. 2: Luka 1:57-80
Na. 3: Sababu Sisi Tunaweza Kupenda na Kuogopa Yehova Pia (rs uku. 198, kichwa kidogo)
Na. 4: Itikadi Tatu Ambazo Hututenga na Dini Nyingine (zitegemeze kwa maandiko) (rs kur. 199-200)
Des. 25 Pitio la Kuandika. Maliza Mathayo 16 hadi Luka 1