Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 10/8 kur. 20-22
  • Ni Muhimu Sana Kuanza Mapema

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Muhimu Sana Kuanza Mapema
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Wajulishe Kuhusu Mabadiliko ya Mwili
  • Ngono Salama ni Ipi?
  • Maagizo ya Mungu Ni Ulinzi
  • Naweza Kuepukaje Kupata UKIMWI?
    Amkeni!—1993
  • Je, Wazazi Wanapaswa Kuwafundisha Watoto Wao Kuhusu Ngono?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Kusaidia Wale Walio na UKIMWI
    Amkeni!—1994
  • UKIMWI— Shida kwa Matineja
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 10/8 kur. 20-22

Ni Muhimu Sana Kuanza Mapema

WATOTO wadogo wana haki ya kupata maelezo kamili ya jinsi miili yao inavyofanya kazi na jinsi ya kujilinda na watu wasio na adili. Lakini maagizo hayo yapasa yaanze lini? Mapema zaidi ya vile wengi wanavyofikiri.

Ujana huanzia wakati wa kubalehe, umri ambao ishara za kukomaa kingono huanza kujitokeza. Huenda msichana akapata hedhi ya kwanza akiwa na umri wa miaka 10 au hata mapema zaidi au baadaye kufikia miaka 16 au baadaye zaidi. Mvulana aweza kupata mtoko wa kwanza wa shahawa usiku mapema kufikia miaka 11 au 12. Je! watoto wako watakuwa tayari kabla ya wakati huo, tuseme kufikia umri wa miaka tisa?a Je! kufikia umri huo mchanga, wao watajua pia umaana wa kudumisha ubikira wao?

Wajulishe Kuhusu Mabadiliko ya Mwili

Binti yako ana haki ya kujua mabadiliko yaliyopewa na Mungu yatakayotokea mwilini mwake. Mama anaweza kutaja kuhusu hedhi yake na kuacha binti yake aone aina ya ulinzi anayotumia. Anapaswa aeleze kwamba mabadiliko hayo ni tabia ya kawaida ya mwili. Kwa njia chanya kabisa, mama aweza kueleza kwamba mwili wa binti yake utakuwa ukijitayarisha wenyewe kwa wakati ambapo, miaka mingi tokea sasa, aweza kuolewa na kuwa mama. Mama aweza kumwelezea binti yake kwamba mwili hutayarishia mtoto katika tumbo la uzazi tishu la kipekee lililo laini, na lenye sifongo ambalo lina chembe nyingi za damu. Wakati mtoto hatungwi mimba, tishu hiyo huondolewa na kutokea kupitia uke, na tendo hilo linaitwa hedhi.

Kwa njia iyo hiyo, mwana wako apaswa ajue kimbele kuhusu mtoko wa shahawa usiku, au ndoto za maji-maji. (Kumbukumbu la Torati 23:10, 11) Anapaswa aelewe kuwa mtoko huo wa umaji-maji wenye utelezi, nyakati nyingine ukiambatana na ndoto, ni njia tu ya mwili ya kuondolea mbali mkusanyo wa shahawa. Wana na binti zenu pia wapaswa wajue kwamba hakuna jambo lolote lisilofaa kuhusiana na mabadiliko hayo ya miili yao. Miili yao inatayarishwa tu kwa uwezekano wa wakati ujao wa ndoa na uzazi.b

Mkiwa wazazi, mnapaswa kuchukua mambo hayo kwa uzito, kwa sababu ni mambo ya kimungu. Na nyinyi ndio mmewekwa na Mungu kuwa walimu.

Ngono Salama ni Ipi?

Miaka inaposonga na watoto wako kuwa matineja, ni lazima uhakikishe kwamba wanajua kwamba ngono kati ya watu wasiooana ni hatari, bila kujali yale yaliyo kinyume ambayo huenda wakasikia. Magonjwa yenye kuenezwa kingono, kutia na UKIMWI, yamekuwa pigo la ulimwenguni pote. Magonjwa kama hayo yanaweza kusababisha kutoweza kupata watoto, kuzaa watoto wenye kasoro, kansa, na hata kifo. Isitoshe, hayo yaweza kuenezwa na watu ambao hata hawajang’amua kuwa wameambukizwa.

Watoto wako wapaswa kung’amua kwamba hakuna njia yoyote ya vizuia-uzazi ambayo imethibitika kuwa na matokeo bora kabisa ama katika kuzuia mimba ama kuzuia kuambukizwa ugonjwa. Kwa kweli, idadi kubwa yenye kushangaza ya vijana wanaotumia aina-aina za vizuia-uzazi wametungwa mimba. Na hata ingawa kondomu (nyuo) zimesifiwa kuwa vizuizi dhidi ya kuambukizwa UKIMWI kutoka kwa mwenzi wa ngono aliyeambukizwa, jarida The New England Journal of Medicine liliripoti kwamba kondomu hushindwa kuzuia kuenezwa kwa vairasi ya UKIMWI kwa mara kama asilimia 17 kwa wakati.

Hivyo, mwandikaji wa safu za gazeti la New York Post Ray Kerrison alikanusha dai la kwamba kondomu ‘hupunguza sana hatari ya kuambukizwa UKIMWI’ kwa kuandika: “Eti hupunguza sana. Ukiweka risasi katika bastola, uzungushe kitundu na kucheza mchezo wa roleti kwa kufyatua bastola hiyo kichwani, kuna uwezekano wa moja kwa sita kwamba utajiua. Kuhusu kondomu, kuna uwezekano wa moja kwa tano kwamba utapata UKIMWI. Sasa tumeweza kupatia jina halisi la udanganyo huo wa kondomu-UKIMWI. Ni roleti ya kingono.”

Watoto wako wapaswa wajue kwamba suluhisho la tatizo la magonjwa yenye kuambukizwa kingono ni rahisi. Ni kukubali mpango wa Mungu wa utumizi wa zawadi ya kimungu, uzazi. Kwa kweli, utendaji wa kingono usio na madhara uko katika ndoa, katika muungano wa maisha yote na mtu mmoja kipenzi ambaye pia hajawa na mwenzi mwingine wa ngono.

Maagizo ya Mungu Ni Ulinzi

Biblia husema: “Mwanamume . . . ataambatana na mkewe.” “Usizini.” “Uasherati usitajwe kwenu kamwe.” “Hakuna mwasherati . . . aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.”—Mwanzo 2:24; Mathayo 5:27; Waefeso 5:3, 5.

Maagizo hayo si yenye kuonea. Badala yake, kuyafuata kutaongoza kwenye familia yenye furaha na yenye muungano. Yule mtoto asiyezaliwa bado ataandaliwa jambo ambalo ana haki kwalo—wazazi wawili, mama na baba. Kila mmoja ana sifa tofauti, na kila mmoja aweza kuchangia kwa maisha ya mtoto mambo ambayo yule mwingine hana.

Mkiwa wazazi, kwa mafundisho yenu na mfano wenu pia, ni lazima mkaze kikiki kanuni zenye msingi wa Biblia ndani ya moyo na akili ya mtoto. Ni lazima mjenge kwa vifaa vigumu—visivyoweza kuchomeka. Kama vile Biblia isemavyo: “Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.” Ukijenga kwa vifaa vigumu na kazi yako isimame, utathawabishwa sana.—1 Wakorintho 3:13.

Lakini swali la maana labaki: Wewe waweza kutiaje nguvu mazoezi hayo watoto wako wakuapo kupitia miaka ya utineja kuelekea kuwa watu wazima?

[Maelezo ya Chini]

a Dakt. Leon Rosenberg wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, katika Baltimore, Maryland, U.S.A., alisema: “Kufikia wakati mtoto ana umri wa miaka 9, wazazi wapaswa kuwa wameketi pamoja na kuwa na mazungumzo ya mambo mengi kuhusu ngono na adili. Kadiri watoto wapatavyo habari nyingi zaidi kutoka kwa wazazi wao, ndivyo ilivyo bora zaidi.”

b Habari zaidi yaweza kupatikana katika sura “Kuwa Mwanamume” na “Kuwa Mwanamke” katika kitabu Kupata Faida Zote za Ujana Wako, ambacho chaweza kupatikana kupitia watangazaji wa gazeti hili.

[Picha katika ukurasa wa 21]

Kutayarisha mtoto wako kwa mabadiliko ya kimwili ni kwa maana

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki