Kutoka kwa Wasomaji Wetu
Upaji wa Krismasi Ile makala “Kitu bora Kushinda Upaji wa Krismasi” (Desemba 22, 1992, Kiingereza) ilishughulikia suala hilo linalobishaniwa kwa njia ya wazi, na kwa busara. Kwanzia mwanzo kabisa, ilikubaliwa na kila msomaji, awe wa kidini au asiwe wa kidini. Kwa kuongezea, haikushutumu vikali mambo yote yanayoshirikishwa na Krismasi. Utoaji huo unaofaa ulifurahisha kusoma na kwa kuutoa katika utendaji wetu wa kuhubiri.
T. T., Ujerumani
Makala hiyo ilinionyesha kwa kweli kile kilicho bora zaidi ya zawadi za Krismasi, yaani, upendo wa wazazi wangu na ile njia ambayo wao hutoa kutoka moyoni. Pia ninakabiliwa na tatizo la kueleza darasa langu sababu inayotufanya sisi Mashahidi wa Yehova tusisherehekee “Siku ya Mtakatifu Nicholas” na Krismasi. Kwa msaada wa makala hiyo, nitaweza kuwajibu ifaavyo.
S. H. S., Ujerumani
Waselti Makala yenu “Waselti—Uvutano Wao Bado Wahisiwa” (Septemba 8, 1992, Kiingereza) ilikuwa yenye kufurahisha sana. Ni jambo la kawaida sana leo [kwa waandikaji] kuona habari za tamaduni za kale kana kwamba watu wa wakati huo walikuwa na maisha bora na kwamba sisi sote tukirudia maisha ya kale, kila kitu kitakuwa sawa. Iliburudisha kusoma makala iliyofunua utamaduni kwa njia ya kupendeza kama hiyo bila kuwafanya waonekane kuwa bora zaidi wala kuwashusha mno.
L. Z., United States
Jinsia ya Mtoto Asanteni sana kwa ile sanduku yenye kichwa “Jinsia ya Mtoto Huamuliwaje?” iliyotokea katika makala “Wanawake—Je! Wanastahiwa Nyumbani?” (Desemba 8, 1992) Mnenifunza nisimlaumu dada yangu mkubwa kwa kuzaa wasichana watano katika kipindi cha miaka kumi na kukosa kuzaa mvulana. Kulingana na makala yenu, ikiwa kuna yeyote wa kulaumiwa, basi ni mume.
E. J. O., Nigeria
Ingawa ni shahawa ya mume inayoamua kama mtoto atakuwa mvulana au msichana, wala mume wala mke hapaswi kulaumiwa. Kama vile makala hiyo ilivyosema, hilo ni “jambo la uumbaji lisiloweza kutabirika” ambalo wala mume wala mke aweza kudhibiti.—Mhariri.
Mafumbo ya Kujaza Maneno Asanteni sana kwa mafumbo ya kujaza maneno! Hivi majuzi nilisoma sura moja juu ya kushuka moyo katika kitabu Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi. Ilidokeza kwamba ushiriki katika “utendaji unaokuletea raha,” kama vile kusuluhisha fumbo la kujaza maneno. Hilo ni dokezo bora sana kwa sababu nilijikuta nikicheka, nikiwa ninafurahia, na kupata habari mpya. Tafadhali endeleeni kuchapisha mafumbo ya kujaza maneno!
M. R., United States
Kitabu kinachorejezewa kinachapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc., watangazaji wa gazeti hili.—Mhariri.
Wazazi Wapotevu Niliposoma ile makala “Vijana Wanauliza . . . Namna Gani Ikiwa Mzazi Wangu Ametuaibisha?” (Oktoba 22, 1992, Kiingereza), machozi yalinibubujika kama gharika. Baba yangu alitengwa kutoka katika kundi la Kikristo miaka miwili iliyopita, na mama yangu nami tumepitia hali zenye kujaribu sana. Nimefanya vile makala hiyo inavyodokeza na kumfunulia mzee Mkristo aliye mkomavu, na nilipokea kitia-moyo kingi na utegemezo.
A. O., Japani
Baba yangu, ambaye wakati mmoja alikuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova, alikuja kuwa mwasi-imani. Amejaribu kukengeusha wengine kutoka katika kweli na hata hutoa hotuba katika makanisa. Wanamwita “askofu mkuu”! Nilisikia aibu kama nini! Makala hiyo ilinisaidia sana.
B. A., United States