Ayubu
Wale wenye siku chache kuliko mimi,+
Ambao baba zao ningekataa
Kuwaweka pamoja na mbwa wa kundi langu.
3 Wao ni tasa kwa sababu ya upungufu na njaa,
Wanatafuna eneo lisilo na maji,+
Ambapo jana palikuwa na dhoruba na ukiwa.
4 Walikuwa waking’oa mmea wa chumvi kando ya vichaka,
Na mzizi wa miretemu ulikuwa chakula chao.
6 Wanalazimika kukaa kwenye mteremko wa mabonde ya mito,
Katika matundu ya mavumbi na katika miamba.
7 Walilia katikati ya vichaka;
Walisongamana pamoja chini ya upupu.
11 Kwa kuwa aliifungua kamba yangu ya upinde na kuninyenyekeza,
Nao waliifungua lijamu kwa sababu yangu.
12 Wanasimama upande wa mkono wangu wa kuume kama kundi la waovu;
Wameachilia miguu yangu,
Lakini wakajenga juu yangu vizuizi vyao vyenye kuleta msiba.+
14 Walikuja kana kwamba ni kupitia pengo pana;
Wamejiviringisha katika dhoruba.
15 Vitisho vya ghafula vimegeuzwa juu yangu;
Cheo changu cha heshima kinafukuzwa kama upepo,
Na wokovu wangu umepitilia mbali kama wingu.
17 Mifupa+ yangu imetobolewa usiku na kuanguka kutoka kwangu,
Na maumivu yanayonitafuna hayapumziki.+
18 Vazi langu linabadilika kutokana na wingi wa nguvu;
Linanifunga kama ukosi wa vazi langu refu.
19 Amenishusha chini katika udongo,
Hivi kwamba nimekuwa kama mavumbi na majivu.
22 Unaniinua kwenye upepo, unanifanya niupande;
Kisha unaniyeyusha kwa kishindo.
23 Kwa maana najua vema kwamba utanirudisha kwenye kifo,+
Na kwenye nyumba ya kukutania ya kila mtu aliye hai.
24 Ila tu hakuna yeyote anayeunyoosha mkono wake juu ya rundo la mabomoko matupu,+
Wala wakati wa kudhoofika kwa mtu hakuna kilio cha kuomba msaada kuhusu mambo hayo.
27 Matumbo yangu yalichemshwa wala hayakukaa kimya;
Siku za mateso zilinikabili.
28 Nilitembea huku na huku kwa huzuni+ wakati ambapo hakukuwa nuru ya jua;
Nilisimama katika kutaniko, nikaendelea kulia nipewe msaada.
30 Ngozi yangu ikawa nyeusi+ na kuanguka kutoka kwangu,
Na mifupa yangu ikawaka moto kutokana na ukavu.
31 Na kinubi changu kikawa cha maombolezo matupu,
Na zumari yangu kwa ajili ya sauti ya watu wanaolia.